Waafrika tumefikia kwenye hatua mbaya sana. Baadhi ya wachungaji wa kilokole wamejipa uungu mtu, wanapenda kutukuzwa, kuabudiwa na kusujudiwa

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Makala hii iliandikwa kwa kiingereza na Mwandishi Kay Musonda na kuchapishwa na jarida la Modern Ghana, toleo no.215 la April 1 mwaka huu. Nimefanya tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili pengine tutapata la kujifunza.

____________

Afrika kwa sasa inashuhudia aina mpya ya utumwa kupitia Ukristo (ulokole). Aina hii ya utumwa wa imani imewafanya watu wengi kuwa wavivu wa kufikiri na uwezo wa kutafakari mambo umedumazwa.

Baadhi ya wachungaji wa kilokole wamejipa uungu mtu. Wanapenda kutukuzwa, kuabudiwa na kusujudiwa. Wanajituza wao zaidi kuliko kumtukuza yule wanayemhubiri.

Wachungaji wa aina hii hawawezi kuongelea mafanikio ya watu weusi kama Barack Obama, Serena Williums, na Usain Bolt. Hawawezi kuongelea wagunduzi waliosaidia kutransform dunia kama kina Albert Einstein, Steve Jobs na wengine. Hawawezi kuongelea Wanasayansi waliodedicate maisha yao na wengine kufia maabara wakitafuta dawa za kutibu magonjwa mbalimbali yanayoisumbua Afrika.

Hawawezi kuongea kuhusu wanafasihi vijana kama Chimamanda Ngozi na Ben Okri, au wakongwe kama Chinua Achebe na Ngugi wa Thiong'o.

Kila pembe ya dunia kuna watu waliofanikiwa kutokana na maarifa, bidii, ubunifu, na weledi. Wapo wafanyabiashara, wanasiasa, wanafasihi na hata wanasayansi wanaofanya mambo makubwa ya kuisaidia dunia yetu. Lakini wachungaji wa Afrika hawatawaongelea watu wa aina hii.

Wao wataongelea mtu aliyepata kazi kimiujiza licha ya kukosa sifa za kupata kazi hiyo, kwa sababu tu aliombewa na kupewa mafuta ya upako siku ya interview ya kazi.

Wataongelea kuhusu kijana aliyetoa mshahara wake wote kwa miezi mitatu mfululizo kwa Mchungaji wake kama mbegu ya mafanikio, baadae akawa 'Boss' kazini.

Au wataongelea kuhusu kijana aliyefeli sekondari lakini baada ya baba yake kumalizia ukarabati wa nyumba ya Mchungaji, alipokea barua ya kupata 'admision' chuo kikuu bila hata kurudia mitihani.

Wachungaji hawa hutumia 'miujiza na shuhuda feki' kama njia ya kuwafumba akili wafuasi wao. Kule Afrika kusini kuna Mchungaji alidanganya kufufua mtu. Hata alipoomba msamaha bado kuna waumini wanaendelea kumuamini na kumsujudu.

Wachungaji hawa wamegundua haya ndio mahubiri yanayopendwa sana huku Afrika. Hawataki kuhubiri kuhusu Aliko Dangote alivyoanza biashara na magumu aliyopitia.

Wanahubiri kuhusu mama Janeth aliyekua mama Ntilie huko Enugu, lakini alipotumia mtaji wake wote wa shilingi laki 5 kununua mafuta ya upako kwa Nabii fulani, ghafla biashara yake ikakua na sasa anamiliki mahoteli makubwa pande zote za nchi. Yani bila mtaji, bila business plan, bila timeline ghafla tu akamiliki mahoteli. Na waumini watashangia kwa kusema Ameen.

Aina hii ya ukristo imepanda mbegu ya uvivu wa kufikiri kwa vijana wengi wa Afrika ambao wanalazimishwa kumuona Mungu kama Mfadhili wa wavivu, au wasiostahili. Kwamba mwanafunzi hata asiposoma anajua akipewa mafuta ya upako atafaulu tu siku ya mtihani. Mfanyabiashara hata asipokua mbunifu anajua akienda kwa 'baba wa miujiza' biashara yake itapanuka ghafla bin vuu. Mfanyakazi hata asipowajibika kazini anajua akitoa fungu la kumi kwa 'Dokta Upako' atapanda cheo.

Kwa baadhi ya makanisa Afrika namna pekee ya kufanikiwa ni kufanya kile wanachokiita kupanda mbegu, kupaka mafuta ya upako au kunyunyuziwa maji ya baraka. Eti wanaofanikiwa haraka ni watu 30 wa mwazo wanaokimbilia mbele ya kanisa kila mmoja akiwa ameshika noti ya dola 100.

Aina hii ya mahubiri inawafanya watu waamini kwamba Mungu hawapendi wanaojituma na kuwa wabunifu katika kazi, badala yake anawapenda zaidi wanaotoa zaka, sadaka, malimbuko na fungu la 10 hata kama ni wavivu. Hii sio sawa hata kidogo kwa sababu Biblia inakataa uvivu kwa nguvu zote (Mithali 12:27)
_
Watu wanaaminishwa kwamba ukishatoa sadaka kanisani unaweza kuamka kila siku asubuhi ukapayuka 'Mimi ni Milionea' halafu ukavuta shuka na kuendelea kulala fofofo, ukisubiri sadaka uliyotoa ikupe muujiza wa kuokota hela, ili upate mtaji wa biashara unayoiwaza.

Mtu huna kazi, huna biashara wala wazo la biashara, huna ujuzi, huna elimu, lakini kila siku unashinda kanisani kumsikiliza Mchungaji anayesema kesho utakua milionea na wewe unasema "Baba napokea/Dady I receive". Huu ni utani.

Waambieni wanaofanya utani huu kwa kofia za Uchungaji, Uaskofu, Unabii au Utume kwamba wanamkosea Mungu. Waambieni Mungu wetu ni Mungu wa kanuni, na hana kanuni ya kuwabariki wavivu. Tuache kufundisha waumini wetu kwamba uvivu unalipa kupitia miujiza.

Mafanikio ni matokeo ya bidii, ubunifu na weledi. Biblia inazungumzia kuhusu karama. Hebu kila mtu atumie karama alizopewa kwa bidii, ubunifu na weledi aone kama hatafanikiwa. Sio sahihi kuwaambia watu wabweteke tu na kusubiria mafanikio kama kusubiria daladala kituoni kwa sababu tu wamepakwa mafuta ya upako.

Mungu alishatubariki tangu wakati wa uumbaji wetu. Ni wajibu wetu kujibidisha katika yale tufanyayo ili baraka zake ziambatane nasi (Kumb 28:6).

Wazungu na Wachina wanazidi kushindana katika kuitawala dunia kwenye mambo mbalimbali kuanzia viwanda, biashara, sayansi na teknolojia. Sisi tuko 'busy' kununua maji ya upako tukiamini yatatufanya tuwe kama Jack Ma au Bill Gates. Upuuzi.

Tumeumbwa kuitawala hii dunia (Mwanzo 1:28). Tutumie vipawa na karama tulizopewa ili kutimiza kusudi hilo la Mungu. Tusiruhusu Askofu, Mchungaji, Nabii, mtume au kiongozi mwingine yeyote wa dini atutawale akili zetu kwa kutuhubiria mafanikio ya miujiza. Wao wanaishi kifahari kwa sadaka za waumini wao, huku waumini wakiendelea kuwa mafukara wa kutupwa.

Biblia inasema kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa (Mithali 1:7). Tutafute maarifa, tufanye kazi kwa bidii, na tumuabudu Mungu katika roho na kweli. Kwa kufanya hivyo tutapata MAFANIKIO katika mambo yote tuyafanyayo.
 
Inaudhi sana kiongozi wangu hawa mitume,manabii na makuhani wa miaka hii wanawafanya waumini wao kuwa wajinga
Mimi ni mlokole mzuri tu na ni mzee wa kanisa TAG ila huwa napingana sana na baadhi ya mafundisho na mifumo ya vyuo vya biblia jinsi vinavyo wa shape watu wao. Huwa nawaukiza watu ni kwanini walokole wengi ni masikini? Wale walokole wafukutwa tofaut sana na wakristo huko KKKT au RC MAFUNDISHO ni tatizo sana.

Yan huwa time nyingine unamwangalia mchungaji af unamoima unaona kabisa hapa hamna usalama huko tunapopelekana.
NB

Nimezaliwa Moravian nimekulia UKWATA.
 
Mafanikio hayatokani na bidii tu, yanatokana na bidii iambatanayo na roho wa mafanikio

Sio kila masikini hana bidii, kuna watu wanabidii ya kazi, ubunifu, na nguvu lakini bado ni masikini

Ukiambatana na roho wachafu, wabaya, hata usomeje, ubunije, ujibidisheje, hutoboi
 
Mafanikio hayatokani na bidii tu, yanatokana na bidii iambatanayo na roho wa mafanikio

Sio kila masikini hana bidii, kuna watu wanabidii ya kazi, ubunifu, na nguvu lakini bado ni masikini

Ukiambatana na roho wachafu, wabaya, hata usomeje, ubunije, ujibidisheje, hutoboi
Jaribu kusoma bila kuhukumu utaelewa makala imemaanisha nini, lakini pia tukumbuke kuwa "roho wachafu" tunawaruhusu wenyewe kwani tumepewa nguvu ya kuwashindi ila tu tunakosa maarifa kwa fikra tegemezi
 
Kwa lugha rahisi ni kwamba, kila tendo ulitendalo kwa hiari yako linatokana na mawazo yako! Mawazo si kitu yabisi kwa maana twaweza kuyaona, mawazo yapo ktk ufahamu, akili ambazo nazo huwezi kuziona wala kuzigusa!

Mawazo, akili tunavitaja lakini lazima tujue vipo kwa viumbe hai, kuimbe hai maana yake kuna roho wa uhai kwa kiumbe huyo!

Kwa lugha nyingine tena ni kuwa, roho wa uhai hamaanishi kutenda kazi zote jinsi mtu anaenenda, zipo roho zingine zimwongozayo mtu kufikiri kwa akili yake ili kupata mawazo ambayo hupelekea mtu kutenda jambo ambalo twaweza kuona kwa macho!

Kwa maana hiyo, kama kiumbe, tuseme mtu, anaweza kuwa na roho nyingi kadri iwezekanavyo zinazomfanya aenende tuonavyo matendo yake!

Roho hawa wakizidi na wasielewane kwa mtu mmoja, mtu huo anaweza kuenenda kwa matendo yasiyoeleweka, tuseme chizi, kichaa au mwehu!

Sasa, ktk karama Mwenyezi Mungu ametugawa, wapo watu kweli wenye karama ya kuona roho mbali mbali na wana mamlaka wa kuwaamuru roho hao watende sawa kadri ya nguvu ya amri wazitoazo!

Ndio maana wapo watumishi unakuta anaamuru roho kadhaa kumwachia mtu ili mtu awe huru na mtu anapokuwa huru, mtumishi anaamuru tena roho wa wema, uzima, uzuri, mafanikio, ulinzi nk waambatane na mtu huyo!

Ukiambatana na roho wa uzima, afya njema, bidii, mafanikio, ubunifu, elimu nk lazima mtu atoboe!

Nikukumbushe tena, roho hawa wanaweza kuishi kufuata uzao, kizazi kwa kizazi ndio maana kutoboa wakati kwenu kote kuanzia mababu zako hakuna aliyetoboa kunahitaji mtu mmoja mwenye mamlaka ya kuona roho wabaya ndani yako na kuwaamuru wakutoke na uwe huru na ukishakuwa huru, aamuru uanze kuambatana na roho wa wema, roho wa kiungu!

Bila shaka tumeelewana, kama una swali, karibu!
 
Kwa maelezo yako haya yote, bila shaka wewe ni mhubiri ama mchungaji wa kilokole and the like!

Kada ambayo ndiyo imeongelewa sana na mtoa mada.

Kwa muktadha huo, kiustaarabu kabisa, wewe haukustahili kuchangia chochote, ulipaswa kuwa ni muangaliaji tu wa kinachojadiliwa na wanabodi ili ujifunze usiyoyajua, sababu elimu haina mwisho.

Lakini kuendelea kutulisha tango pori lilelile chungu kwa kulipaka sukari ni tabia ya kudekeza ubishi usiokuwa na manufaa yoyote.
 
Elimu haina mwisho, nakubali na nakubali kujifunza, tatizo lipo kwa anayetoa mada akiamini makala ya inahitimisha elimu!

Natoa Rai, someni vyanzo vingi vya maarifa ili msiwe vipofu na kudhani uwazavyo juu ya ufahamu wako ndio mwisho wa elimu!

Unataja watu maarufu kiuchumi, kisiasa, kisayansi nk unadhani watu maarufu kidini hakuna? Huu ni upofu!

Someni juu ya mambo ktk ulimwengu wa mwili na nyama pia na mambo ktk ulimwengu wa roho!

Tambua tu kuwa, viumbe hai visivyoonekana huzungumziwa zaidi ktk ulimwengu wa roho, vinginevyo itokee tu kuwa mtu huamini kama kuna viumbe hai visivyoonekana!

Elimu ni Pana, msijipofushe!
 
Dini zote na madhehebu yote yanapumbaza waumini.

Uzuri wa dini inawapumnaza waumini wake wote halafu mnabaki kuchekana, mlokole anaona mkatoliki anaibiwa, mkatoliki anaona mlokole anatapeliwa, wote mnakua kazi yenu ni kuchekana.

Vile vile msabato atamcheka na kumshangaa mlutheri ama mtu anaedali jumapili na mtu wa jumapili ataona mtu anaesali jumamosi kama amechanganyikiwa, yote hii inatokana na dini kuwapumbaza wote kwa kiwango kile kile.

Haya mambo ya dini ni utapeli kama utapeli mwingine, mungu wala shetani hawapo.
 
Back
Top Bottom