Watanzania wanapenda sana topic nyepesi

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,889
3,412
wakuu hili jambo nimelifatilia kwa muda mrefu sasa
wengi wetu hapa jf tunapenda sana zile topic nyepesi hasa za mapenzi,utani na jokes,dini na nyingine kama hizo
ikitokea topic ya kuumiza kuchwa kufikiri wachache sana wanajitokeza
hii inanifanya niukubali usemi wa rais mstaafu mkapa kwamba watanzania ni wavivu wa kufikiri
 
Nafikiri kuna tofauti ya Topic Nyepesi na Mtizamo wa Mstaafu Ben Mkapa!! Kuna topic nyepesi ambazo ZINAFIKIRISHA SANA!!
 
kwa ujumla "watanzania tunapenda starehe"
hatupendi kuumiza kichwa na hata kufanya kazi tunafanya kwa kutimiza wajibu, asilimia kubwa ni uvivu ndio umetawala katika kufanya kila kitu
watanzania walio wengi wanapenda kufanya kazi kidogo ila kupata faida kubwa na muda mwingi wa kustarehe
ndio maana mkuu unaona topics nyingi zinazoshambuliwa kwa wingi ni za mambo ya mapenzi, porojo za siasa, udaku, utani nk
hili lina athiri sana thamani ya JF coz hata jukwaa ambalo limetengwa kujadili mambo ya technology au afya unakuta watu wanaamua kuchangia mada husika katika hali ambayo wao itawafurahisha bila kujali umuhimu wa mada yenyewe.
 
Kutokana na uvivu wa kufikiri,tutaendelea kuichagua Magamba na baadae tunalamika lalamika ovyo
 
constructive arguments zilliishia wapi jamani? Naona hata mambo ya biashara na uchumi kumelala kabisa. Hivi kwa mwendo huu wa topic nyepesi tutafika kweli?
Something needs to be done kwa kweli.
 
Mkuu...unaweza kuwa sahihi..ila tambua kuwa kumekuwa na uchangiaji wa kishabiki zaidi kwenye mada nzito...unakuta hoja ipo ya msingi ila mtu ataipinga tu kwa kuwa haiendani na itikadi yake...
Utaona kuwa ukitaka Thread yako watu waipende andika pumba zozote kuiponda CCM...utaona likes kibao badala ya kujadili kwa kujenga.
 
Kufikiri kunachosha bwana. Tufikirie maisha bado tuje jeief napo tufikirie madude mazito.khaaa!
 
wakuu hili jambo nimelifatilia kwa muda mrefu sasa
wengi wetu hapa jf tunapenda sana zile topic nyepesi hasa za mapenzi,utani na jokes,dini na nyingine kama hizo
ikitokea topic ya kuumiza kuchwa kufikiri wachache sana wanajitokeza
hii inanifanya niukubali usemi wa rais mstaafu mkapa kwamba watanzania ni wavivu wa kufikiri
Mkuu hii topic yako tuiweke kwenye kundi gani naona kama NYEPESI vile.
Kujibu swali lako watu humu huja kwa madhumuni tofauti:
1.wanaokuja kujifunza kwa kusoma mada
2.wanaokuja kutoa dukuduku lao
3.wanaokuja kupoteza muda wao hapa
4.wanaokuja kupumzisha akili(mimi nikiwa mmoja wao)

Mara nyingi kule international na siasa napita kidogo lakini maskani yangu kuanzia Photo's kwenda chini.
 
Dah, Jamaa Mvivu Kufikiri Maana amesahau kuwa chema kinajiuza kibaya chajitembeza.
 
Hakuna ishu ya sijui topic nyeusi wala sijui topic ngumu humu JF kuna watu wa aina mbalimbali

1. Kuna members wao wanapenda michezo hauwezi kuwalazimisha waje kuchangia topic MMU
2. Kuna members wao wanapenda siasa hauwezi kuwalazimisha kwenda kuchangia topic kwenda Jukwaa la Michezo
3. Na mengineyo mengi

Pili una-judge vipi hii TOPIC ngumu au hii NYEPESI kila mtu ana uelewa tofauti wa mambo rahisi kwako kwa mwenzako ngumu, ngumu kwako kwa mwenzako rahisi
 
kwa ujumla "watanzania tunapenda starehe"
hatupendi kuumiza kichwa na hata kufanya kazi tunafanya kwa kutimiza wajibu, asilimia kubwa ni uvivu ndio umetawala katika kufanya kila kitu
watanzania walio wengi wanapenda kufanya kazi kidogo ila kupata faida kubwa na muda mwingi wa kustarehe
ndio maana mkuu unaona topics nyingi zinazoshambuliwa kwa wingi ni za mambo ya mapenzi, porojo za siasa, udaku, utani nk
hili lina athiri sana thamani ya JF coz hata jukwaa ambalo limetengwa kujadili mambo ya technology au afya unakuta watu wanaamua kuchangia mada husika katika hali ambayo wao itawafurahisha bila kujali umuhimu wa mada yenyewe.

mkuu unachosema nikweli! kuna jukwaa la afya watu kule mibnafsi huwa wananiboa sana! badala yakutupatia utalaamu wako tukaelimika mtu analeta utani!
 
Mkuu...unaweza kuwa sahihi..ila tambua kuwa kumekuwa na uchangiaji wa kishabiki zaidi kwenye mada nzito...unakuta hoja ipo ya msingi ila mtu ataipinga tu kwa kuwa haiendani na itikadi yake...
Utaona kuwa ukitaka Thread yako watu waipende andika pumba zozote kuiponda CCM...utaona likes kibao badala ya kujadili kwa kujenga.
Siyo lazima kila hoja iwe ya kisiasa. Kuna forum nyingi hapa JF kama za uchumi, teknolojia, elimu, n.k. Lakini siyo popular. Mimi ningetegemea kwenye teknolijia, kwa mfano, watu wawe wanapashana taarifa kuhusu concepts/ideas walizoziona au wanazofikiria ambazo zinaweza kutekelezwa katika mazingira yetu na kusaidia vijana kumpambana na ukosefu wa ajira na umasikini kwa ujumla. Badala yake watu wanapeana mbinu za kuchakachua gadgets, sofware, n.k. Kama wewe unao ujuzi kama huo kwa nini usiutumie in a positive way and make money in the process.
 
Mkuu utakubaliana na mimi kuwa sisi watanzania ni watu wepesi sana?je ndio maana tunashindwa kushindana na wakenya?
 
Majukwaa ni mengi na kila jukwaa lina wachagiaji wake.
Wewe kama utakuwa upendi kwenda kwenye jukwaa flani basi lazima utaona kule kuna topic nyepesi ujikite zaidi kwenye jukwaa lako ulilozoea ndio unaona kuna hoja nzito
 
Mkuu utakubaliana na mimi kuwa sisi watanzania ni watu wepesi sana?je ndio maana tunashindwa kushindana na wakenya?

Hii nayo umenzisha topic ingine, watanzania na wa kenya? Simpleeee! Leta ngumu tusumbue vichwa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom