Watanzania tusikubali nchi yetu kuwa inaibiwa na wachache wanaodhania kuwa wao wana akili nyingi. Hii nchi sio mali ya WanaCCM wachache.

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Tukubaliane kabisa kuwa CCM imepewa madaraka kuongoza nchi kwa niamba ya watanzania mil 60 bila kujali itikadi zao.

CCM kuwa madarakani sio sababu ya wanaCcm wachache ambao walishakuwa viongozi kujifanya wao na familia zao wanajua sana kupiga madili makubwa na kunufaisha matumbo yao.

CCM kuwa madarakani isiwe sababu ya kujiona kuwa ni chama cha kifalme ambacho kinaweza kuwaona watanzania ni mazoba hivyo viongozi wake wanaweza kufanya wanavyotaka.

Tumesikia kuwa mazungumzo juu mradi wa Bandari ya Bagamoyo yameresume. Ni jambo jema. Lakini je, yatakuwa na tija kwa taifa na watu wake?

Mazungumzo haya yanayolazimishwa kwa udi na uvumba sio kwa manufaa ya watu wachache? Yatakuwa yanawekwa wazi ili kila mtu ajue nini kinaendelea?

Kama mazungumzo haya ni kwa manufaa ya WanaCCM wachache ambao walishajenga tabia ya kuliibia hili taifa huu ni wakati wa kuwapinga kwa kila namna. Watanzania tuwe tayari kulinda taifa letu dhidi ya mafisadi kwa kila namna. Njia pekee inayofaa ni kuingia barabarani na kuig'oa CCM kama yalivyofanyika Tunisia kama ikitokea wataleta dharau za kuliibia taifa letu.
 
Mkuu tuingie barabarani kuing'oa serikali halali INAYOTAMBULIWA NA KATIBA?!!!

Mkuu Watanzania hawajafikishwa huko. Watanzania kwa UMOJA WAO wa vijijini na mijini HAWAJAFIKISHWA HUKO.

Mkuu ni wanasiasa tu wachache ndio wanaosukuma uasi wa aina hiyo.

SUALA LA BANDARI mbona linaongeleka vyema tu?!!!

Bunge ni mali yetu WANANCHI na linasema serikali iliyotangulia ILIPOTOSHWA kuhusu suala la bandari ya BAGAMOYO sasa tunashangaa nini ?!!!

Mbona mh.JAKAYA KIKWETE alishawahi kusema kuwa "anadanganywa" na "kupotoshwa" na watendaji wake WACHACHE?!!!!

Mbona watendaji wachache wameshawahi kumpotosha kipenzi chetu hayati JPM pale "AIRPORT"?!! UMESAHAU ?!!!!

Tumpe nafasi mh.Rais SSH na serikali yetu adhimu isimamie MASLAHI YETU KUNTU.....!!!

#NchiKwanza
#KaziIendelee
#JMTKwanza
 
Mkuu tuingie barabarani kuing'oa serikali halali INAYOTAMBULIWA NA KATIBA?!!!

Mkuu Watanzania hawajafikishwa huko...
Serikali halali kutambuliwa na katiba ndio iwe sababu ya kutuibia? Ndio iwe sababu ya rais kudanganywa. Kama imeshakuwa mazoea kutuibia sasa ni wakati wa kutumia umma kuwaondoa.
 
Serikali halali kutambuliwa na katiba ndio iwe sababu ya kutuibia? Ndio iwe sababu ya rais kudanganywa. Kama imeshakuwa mazoea kutuibia sasa ni wakati wa kutumia umma kuwaondoa.
Ushahidi wa kuibiwa uko wapi mkuu?!!

Hivi Bunge liseme MRADI huo halali.....halafu utegemee USIWE msafi ?!!!!

Mkuu isije ikawa ni "pereche" za siasa hasimu tu.....!!!

Unakubali kuwa VIONGOZI wameshawahi kupotoshwa huko nyuma ?!!!

Unakataa hili ?!!

#KaziIendelee
#JMTKwanza
 
Kwa utumbo uliopost hapa sioni sifa ya kujadiliana na wewe.
Sawa mkuu....

Ila watanzania kwa UMOJA WAO si wajinga wa KUANDAMANA dhidi ya serikali Yao halali.....

Hayo ni mambo ya wanasiasa wachache tu....waliotaka KUANDAMANA mwaka jana kutokea UBUNGO na WAKAKOSA wananchi wenye KUJITAMBUA.....

#KaziInaendeleaKwaKasiYaKutisha
#JMTKwanza
 
Acha upuuzi wako bandari ya bagamoyo ni muhimu mno kwa future generation ubinafsi ni kujiangalia wewe pekeyako bila kuangalia vijukuu vyako vya baadae vitaishije (mwenyekiti wa CHAMA cha wafanyabiashara jana alizungumzia suala VIZURI sana itafute hotuba yake uisikilize)
umetafakari kipengere cha mchina kuhodhi ardhi miaka 99 alichosema JPM?hicho nacho ni kwa future genneration accomplishment au
 
Acha upuuzi wako bandari ya bagamoyo ni muhimu mno kwa future generation ubinafsi ni kujiangalia wewe pekeyako bila kuangalia vijukuu vyako vya baadae vitaishije (mwenyekiti wa CHAMA cha wafanyabiashara jana alizungumzia suala VIZURI sana itafute hotuba yake uisikilize)
Jitu linalotaka maamuzi ya kitaalamu ya kitaifa yafanyike kisiasa na kuwa siri ya watu ama familia chache, halifali kuwa miongoni mwetu. Wewe hufai kuwa kati kati ya Watanzania . Pumbavu sana.
 
Kuna watu wanajitoa ufahamu utasema wao ndio waadilifu sana na mtu akiwa mwizi basi anadhani kila mtu mwizi. nchi haiendeshwi na opinion za watu ila kwa facts.

Hawa wanaojifanya hawaelewi iko siku wakiona shughuli za kiuchumi ukubwa wake kwa kuchochewa na Bandari watakaa kimya. wako watu wanapinga mpaka SGR ila mimi nasema SGR ni mradi muhimu huko mbeleni. JPM alipigania kwa nguvu zake SGR akiamini unafaida wako wanapinga mpaka leo bila kuwa na solution.

Bandari JPM hakupinga ila kama mradi ila terms and condition Mama anaweka mambo sawa kwa hiyo hakuna anayebisha Bandari ni muhimu tena sana tuache serikali ifanye kazi ya majadiliano ila mradi lazima ufanyike utaleta tija kubwa sana katika ukanda huu wa pwani na nchi kwa jumla.
 
Jitu linalotaka maamuzi ya kitaalamu ya kitaifa yafanyike kisiasa na kuwa siri ya watu ama familia chache, halifali kuwa miongoni mwetu. Wewe hufai kuwa kati kati ya Watanzania . Pumbavu sana.
Busara ni mkataba uwe wa wazi na ikimpendeza MH.RAIS mkataba ujadiliwe na bunge letu kwa parameter zote, that's the point.
#Mradi_ huu_ni_muhimu_sana.
 
Tukubaliane kabisa kuwa Ccm imepewa madaraka kuongoza nchi kwa niamba ya watanzania mil 60 bila kujali itikadi zao.

Ccm kuwa madarakani sio sababu ya wanaCcm wachache ambao walishakuwa viongozi kujifanya wao na familia zao wanajua sana kupiga madili makubwa na kunufaisha matumbo yao...
Mmeanza kuona umuhimu wa Nguvu ya Taasisi badala ya Nguvu za viongozi? Nikuombe tujadili bila jaziba umuhimu wa nguvu za wananchi badala ya nguvu za nchi kuwekwa kwa mtu mmoja.

Kama katiba yetu ingekuwa nzuri na inayotoa nguvu kwa jumuia kuamua mambo ya nchi, haya yasingejitokeza. Mbunge mmoja tu kwa niaba ya Wananchi angeanzisha hoja ya kujadili hili na tungeona mjadala wenye Afya kwa maslahi mapana ya Taifa.

Lakini kwa Bunge lipi tunapata faida hiyo? Hili ambalo Wabunge wanakwenda Dodoma wakatokea Dar bila kupitia majimboni kwao kupata maoni ya Wapiga kura? Hili la Spika mbinafsi asiyependa wengine wapate? Huyu aliyezawadiwa Study Tour ya Guangzhou ili aje awe mpiga debe wa mradi wa Bagamoyo bila kutuambia ndani ya mkataba kuna nini? Ukimuuliza tupe mazuri yaliyomo, anasema Rais alipotoshwa ili yaliyomo yamo.

Tukiwa na katiba inayowatambua na kuwathamini watanzania wote kama wamiliki wa nchi hata haya maoni yako yatapata nguvu na hata ukiungwa mkono na watu 10 mnajua kwa uchache wenu mtasikilizwa hata kama hamtashinda lakini mtaeleweshwa kwa nini hoja yenu imeshindwa.
 
Kwa Magufuli haukujadiliwa kwa Mama ujadiliwe?
Ndio,ikiwezekana hakuna ubaya yule jamaa alikuwa anazipiga juu kwa juu,na alikuwa hashauriki yeye alikuwa anajua kila kitu ndani ya dunia hii.
RAIS WETU WA AWAMU YA SITA ANASHAURIKA,NAYE PIA ANAJICHO ANGAVU SANA SHE IS INTELLIGENT ENOUGH,
 
H
Tukubaliane kabisa kuwa Ccm imepewa madaraka kuongoza nchi kwa niamba ya watanzania mil 60 bila kujali itikadi zao.

Ccm kuwa madarakani sio sababu ya wanaCcm wachache ambao walishakuwa viongozi kujifanya wao na familia zao wanajua sana kupiga madili makubwa na kunufaisha matumbo yao...
Hapo kwenye paragraphs ya pili na ya tatu, kwa hio na wewe unataka upige madeal? Unawaonea CCM wivu unataka CCM kitoke madarakani ili na wewe chama chako kipige madeal ili mshibe matumbo yenu?

Naomba nikuulize, kwani hii bandari ya Bagamoyo inajengwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza ama Uwanja CCM Samora Iringa?
Ushauri wa Bure, kama kweli una hasira na CCM na una uhakika Kwamba CCM ndio inakufanya uwe maskini, basi pitia njia ya Samora - FRELIMO , Museveni - NRM, Mandela - ANC , Kagame - RPF, Augustine Neto- MPLA, nk ingia mstuni/ polini anzisha mchezo ili ukiondoe CCM madarakani halafu uanze kula madeal kama walivyo wenzio wa CCM.
 
Hakika mwanasiasa ndiye Mungu wa nchi hii. Magufuli alipinga mambo waliyoyataka wenzake, lakini akachukua pesa za umma na kwenda kujenga kwao. Nao watu wa Bagamoyo na pwani vivyo walitamani kujengwe kwao. Na sisi Mbeya ile Barabara nzuri ikaishia Igawa. Na sisi mtu wa kusukuma ujenzi wa Barabara ije kwetu hatuna.

Barabara ya hapa Mwanjelwa inazidiwa na magari kila siku nani wa kutuona. Ni sahihi kwamba ili mufikiriwe ni mpaka muwe na mgombea uraisi au raisi?Mpaka lini sisi huku kwetu itakuwa ni mikoa ya kuombea kura tu?
 
Ndio,ikiwezekana hakuna ubaya yule jamaa alikuwa anazipiga juu kwa juu,na alikuwa hashauriki yeye alikuwa anajua kila kitu ndani ya dunia hii.
RAIS WETU WA AWAMU YA SITA ANASHAURIKA,NAYE PIA ANAJICHO ANGAVU SANA SHE IS INTELLIGENT ENOUGH,
sawa
 
Projects zozote kubwa huwa zina changamoto zake na Wakati mwingine huwenda ni MASHINIKIZO KUTOKA NDANI AMA NJE NA YASIYO MASHIKO YOYOTE YALE:

1)MWALIMU NYERERE HEPP
**************************

Ikumbukwe mradi huu ulipingwa mno na BAADHI YA VYAMA VYA UPINZANI na hata baadhi ya wabunge wa CDU wa bunge la ujerumani (Bundestag) kwa kisingizio cha UHARIBIFU WA MAZINGIRA PALE SELOUS ilihali shirika la mazingira duniani lilisharidhika na hatua stahiki zilizoainishwa na kuchukuliwa na SERIKALI ya Tanzania......

Ikumbukwe UJERUMANI ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na VIWANDA VINGI BARANI ULAYA.....

2)Mradi wa SGR
**************

Ulipingwa sana na baadhi ya wanasiasa wa ndani kwa kigezo cha kuwa unabeba GHARAMA kubwa ya KODI ZA WATANZANIA kuliko uhalisia wa uchumi tuliokuwa nao.....hapa haikuangaliwa "SACRIFICE" katika kuyafikia MAENDELEO MAKUBWA....sijajua iwapo pia kuna MASHINIKIZO YA NCHI JIRANI AMA HATA UGHAIBUNI juu ya ununuzi na uagizaji wa MAGARI YA MIZIGO na mfanano wake.......

#KaziIendelee
#JMTKwanza
 
Back
Top Bottom