Tanzania tumepewa mali na tukanyimwa akili

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Tanzania ni nchi nzuri iliyobarikiwa kila kitu.

Imebarikiwa kijiografia kwa kuwekwa mahali pazuri kwenye lango kuu la bahari ambayo ni tegemeoa la nchi takriban sita. Nazo ni Zambia, Congo DRC, Malawi, Burundi, Rwanda, Zimbabwe.

Tunayo kila aina ya madini muhimu duniani - Almasi, Dhahabu, Tanzanite, Nickel, Uranium, Chuma nk!

Tunayo milima na mabonde yenye rutuba yaliyosheheni nchi nzima. Pia Tunayo maziwa na mito maarufu Duniani.

Lakini tumelaaniwa kwa kunyimwa akili ya kujitambua na kuthamini vitu vyetu. Tumelaaniwa kwa kuwa taifa la wanafiki, Wezi na wabinafsi... hususan wale wanaopata nafasi za kutuongoza wanapoutumia ujinga wetu kujineemesha wao binafsi na walioko karibu yao pekee.

Mfano huu wa mkataba wa ovyo kuwahi kutokea nchini wa DP-WORLD.

Kinachoendelea ni wajanja au wezi wachache huko serikalini kutumia baadhi ya wajinga wachache, ili kutugawa Watanzania kwa muktadha wa kidini.

Badala ya kuuchambua mkataba na ubovu wake, wao wanakazania neno uwekezaji. Ilhali hakuna Mtanzania anayekataa uwekezaji, bali Watanzania wanakataa uwekezaji wenye mikataba mibovu ya kinyonyaji kama huu wa DP-WORLD.

"Nafikiri tunachanganya sana mambo, sijui ni kwa makusudi au ni kwa kutoelewa, hakuna sehemu kwenye waraka wa Maaskofu iliyotaja mashekhe wala Uislam, bali hoja yao ni mkataba kuhusu bandari. Nafikiri wanaowapinga Maaskofu wapinge kwa hoja kama wao siyo kuleta swala la udini."

"Kwani waraka wa TEC unamaamuzi gani? Wewe pinga au kataa. Ila mababa Askofu, wanachokipinga ni mikataba mibovu itakayo tuingiza kwenye hasara. Dini zingine wakubali au wapinge mkataba,ni haki yao wafanye wanavyoviona."

Mungu inusuru Tanzania
 
Nchi tuna wajinga wengi sana,leo hii waislam wanatukana maaskofu wa RC badala watukane walichoandika. UJINGA Huundo mtaji wa ccm wanautegemea sana.
Kweli kabisa na umelenga kwenye Jackpot kabisa.
 
Tukubari, tukatae, ukweli utabaki kua Mzungu kabarikiwa maarifa na akili, Muafrika kabarikiwa nguvu kazi basi
 
Tanzania ni nchi nzuri iliyobarikiwa kila kitu.

Imebarikiwa kijiografia kwa kuwekwa mahali pazuri kwenye lango kuu la bahari ambayo ni tegemeoa la nchi takriban sita. Nazo ni Zambia, Congo DRC, Malawi, Burundi, Rwanda, Zimbabwe.

Tunayo kila aina ya madini muhimu duniani - Almasi, Dhahabu, Tanzanite, Nickel, Uranium, Chuma nk!

Tunayo milima na mabonde yenye rutuba yaliyosheheni nchi nzima. Pia Tunayo maziwa na mito maarufu Duniani.

Lakini tumelaaniwa kwa kunyimwa akili ya kujitambua na kuthamini vitu vyetu. Tumelaaniwa kwa kuwa taifa la wanafiki, Wezi na wabinafsi... hususan wale wanaopata nafasi za kutuongoza wanapoutumia ujinga wetu kujineemesha wao binafsi na walioko karibu yao pekee.

Mfano huu wa mkataba wa ovyo kuwahi kutokea nchini wa DP-WORLD.

Kinachoendelea ni wajanja au wezi wachache huko serikalini kutumia baadhi ya wajinga wachache, ili kutugawa Watanzania kwa muktadha wa kidini.

Badala ya kuuchambua mkataba na ubovu wake, wao wanakazania neno uwekezaji. Ilhali hakuna Mtanzania anayekataa uwekezaji, bali Watanzania wanakataa uwekezaji wenye mikataba mibovu ya kinyonyaji kama huu wa DP-WORLD.

"Nafikiri tunachanganya sana mambo, sijui ni kwa makusudi au ni kwa kutoelewa, hakuna sehemu kwenye waraka wa Maaskofu iliyotaja mashekhe wala Uislam, bali hoja yao ni mkataba kuhusu bandari. Nafikiri wanaowapinga Maaskofu wapinge kwa hoja kama wao siyo kuleta swala la udini."

"Kwani waraka wa TEC unamaamuzi gani? Wewe pinga au kataa. Ila mababa Askofu, wanachokipinga ni mikataba mibovu itakayo tuingiza kwenye hasara. Dini zingine wakubali au wapinge mkataba,ni haki yao wafanye wanavyoviona."

Mungu inusuru Tanzania
Jamani ..mambo ni mazito
 
Mateka aliyefungwa Kwa minyororo gerezani kamwe asilaumiwe kukosa akili.

Aliye huru na asijisifu, apambane kuhakikisha wafungwa wanafunguliwa.

Amen
 
Back
Top Bottom