Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Hatupendi mambo ya kugonganisha vichwa; hatupendi kubishana na kuhojiana hadi mtu akubali kushindwa kwa hoja; tunapenda mambo mepesi mepesi. Angalia Bungeni, mambo yakianza kupamba moto mara Spika anaingilia kati na kutuliza "jazba". Kiongozi akija mbele na kuzungumza na waandishi wa habari badala ya kumbada hadi asikie kizunguzungu tunaona huruma na hatutaki kumuabisha kwa kumbana; tunapenda mepesi mepesi.
Wakati watu kwa maelfu wanazungumzia mambo ya Muro na Kova, bado hatujagusa mambo muhimu ya taifa letu. Tumeshasahau suala la Ndulu na majumba yake; hatujaangalia masuala ya wanafunzi 130 walionusurika kuungua kwa bweni lao (kwa mara nyingine)huko Kilimanjaro; hatujajiuliza hali ya wahanga wa mafuriko imefikia wapi; tunapenda mepesi mepesi.
Tunasikia serikali imelipa watumishi "hewa" shilingi bilioni 7 na ushee na wakati huo huo wametenga bilioni 7 nyingine kwa kombe la dunia (bilioni 14 zimenyweza hizo) huku wanakinga mikono bila haya kuomba bilioni 15 kwa ajili ya miundo mbinu iliyoharibiwa na mafuriko; tunashindwa kuwauliza mbona bajeti yake walisema ni bilioni 7 tu? Tunapenda mepesi mepesi.
Hatupendi kuchukizana. Hatupendi mtu kubishiwa hadi akubali kwamba hoja yake ni ya kipuuzi. Mtu mwenye akili timamu na jina kubwa akisema kitu cha kijinga hatutaki kumuonesha hilo badala yake tunajaribu kumpepea pepea kama waganga wa kienyeji.
Mtu akitokea akisema sana na akizungumza kwa jazba na hoja za nguvu tunakimbilia na kusema "anajiona anajua sana". Na tukiona anatusumbua tunakimbilia kudai kuwa "anatumiwa". Tunapenda mambo mepesi mepesi.
Matokeo yake hata inapokuja mijadala kwenye nafasi zetu za kazi kuhusu miradi au mipango fulani hatutaki kuzama; tunazungumza juu juu tu tukitoka hapo ndio tunazungumza "unajua pale tungefanya hivi" tunabishania pembeni na si vikaoni; hatutaki kumuudhi bosi.
Tunaogopa kuambiwa "tunahatarisha amani na mshikamano"; tunaogopa kuambiwa ati ni "wachochezi". Tukisema mafisadi wote wanyongwe watu wataruka juu kwamba hayo mambo makali; tukisema Kikwete asigombee tena tunaonekana tunapendekeza mbingu kuanguka! Hivyo tunaamua kukaa kimya na kufikiria tu kile tunachotamani.
Matokeo yake tunaburuzwa; tunasukumwa sukumwa tunatikiswa tikiswa na wale wenye uwezo; tunanabakia kama alivyosema mtawala wetu mkuu "kufuata mkumbo". Kwa maneno mengine siye tupo tupo tu.
Nasema tufunguke fikra zetu na mawazo yetu yaachiliwe huru; tufungue vinywa vyetu na kuwapinga watawala wetu. Ukisikia sijui "serikali imesema" usifungue mdomo kama kinda la ndege na kupokea tu bila kuuliza "je ina mantiki, je ni halali, je ina msingi, je je je". Usiende kulalamika pembeni.
Kama wewe ni mwandishi, usitosheke na majibu ya kwanza; tafuta majibu ya pili, angalia kujipinga, angalia kutisha tisha. Tafuta maelezo zaidi; rudi tena na uliza tena hadi wakutimue kwenye ofisi zao! Kama ni mwananchi usikubali kupiga makofi kushangili kitu ambacho hakipo. Ati mnaambiwa mtajengewa mabarabara ya juu kwa juu watu wanachekelea! Ndio maana leo watu bado wanafurahia tu kupiga picha kwenye daraja la pale Manzese kwani wanajiona kidogo imefanana na majuu! Hakuna anayeuliza zile takataka pembeni zitaondolewa vipi!
Tunaambiwa ati tutapewa matreni yanayoenda kwa kasi, wabunge wetu wanaruka ruka kwa furaha kuwa sasa na sisi tumefika. Hawaulizi kesi ya ATCL na Airbus yake imefikia wapi!
Tunapenda mambo mepesi mepesi, tunapenda majibu mepesi mepesi. Ndio maana sasa najua kwanini ilikuwa vigumu sana kwa watu kumshinda Nyerere kwa hoja hadi kufikia kudai kuwa "haambiliki". Kumbe walikuwa ni wepesi wepesi. Si tunawaona leo jamani!
Tuamke!