Watanzania tunapenda mepesi mepesi!

Tumaini.. tatizo lako wewe huwezi kujaliana na watu bila kuwatukana na kuonesha dharau. Hoja haiwi na nguvu kwa sababu imeambatana na matusi na kejeli. Tunaposema tunabishana na kujadiliana haina maana ni lazima tutukanaane au kuitana majina ya uduni. Umeona juzi Warepablikani huko US wakijadiliana na Rais wao tena kwa uwazi kabisa bila kumtukana au kumuita mjinga na mpumbavu. Ni hoja tu.

Nadhani turudie ule msemo wangu wa mwanzo sana ambao naona siku hizi umepotea hapa Hoja Hujibiwa kwa Hoja, siyo Vioja!

Ha ha! Hakuna mahali mimi nimewahi kutukana yaani nianze kutukana NO! mpaka iwe namjibu aliyenituka (mimi naamini jino kwa jino) huwezi kuleta dharau zako eti nikuache not me!

Kuna watu hapa JF wanapenda maswali yasiende chadema au kwa viongozi wao au hawataki kusikia habari ambazo ni kweli (painfull truth) sasa ni shauri lao maana mimi siogopi kukuudhi kama unaona hoja ya yangu haikufahi usilete dharau..ukifanya hivyo mimi nalipa (jino kwa jino) ndio heshima itapatakana maana wabongo wamezoea kupendelewa na kubebelezwa haki haibembelezwi
 
MM

Unagonga msumari mwingine tena. Sisi sio wepesi wa kusahau au tunaopenda mambo rahisi, tatizo liko kwa vibaka hapa aka Vifisadi dagaa utaona vinaleta mambo ya udini au uzanzibari ili basi kuvuruga mada.

Hatujasahau na wala hatutasahau wale watoto waliokufa Tabora kwa Uzembe wa Dau na NSSF, hatutasahau uhuni wa serikali ya Chama Cha Majambazi wa kuachia BOT kufanya wanavyopenda na pesa ya walipa kodi kuanzia EPA nyumba ya Ndulu nk. hatutasahau mateso kwa watanzania wenzetu waliosombwa na mafuriko na wale wanaolala Temeke kwenye sakafu tena katika karne hii.

Ipo siku inakuja watetezi na makuwadi mafisadi watatetema na kufahamu kumbe kweli Tanzania ina wenyewe na wenyewe ni walipa kodi.
 
......Umeona juzi Warepablikani huko US wakijadiliana na Rais wao tena kwa uwazi kabisa bila kumtukana au kumuita mjinga na mpumbavu. Ni hoja tu.
Mzee Mwanakijiji, sina cha kuongeza manake makala yako imemulika madhaifu mengi niliyonayo. Ila naomba niulize manake mimi sina "interesti" na inteneshno politiksi, hivi Obama nae ameanza Kupruvu U-JK?
 
Mzee Mwanakijiji, sina cha kuongeza manake makala yako imemulika madhaifu mengi niliyonayo. Ila naomba niulize manake mimi sina "interesti" na inteneshno politiksi, hivi Obama nae ameanza Kupruvu U-JK?

absolutely.. niliandika month kabla ya mambo ya Tea Party kwamba he will face a revolt kwani ule umasiha utaisha. Na sitoshangaa (I have a tendency to be right on this) kwamba Obama anaweza kujikuta anapewa muhula mmoja tu. Ila siku hizi mbili tatu ameanza kujirudi. Kikwete hawezi kujirudi kwani hajui kama anaongoza vibaya.
 
absolutely.. niliandika month kabla ya mambo ya Tea Party kwamba he will face a revolt kwani ule umasiha utaisha. Na sitoshangaa (I have a tendency to be right on this) kwamba Obama anaweza kujikuta anapewa muhula mmoja tu. Ila siku hizi mbili tatu ameanza kujirudi. Kikwete hawezi kujirudi kwani hajui kama anaongoza vibaya.

Kuongoza vibaya ni subjective term ndugu waweza kuona wewe anaongoza vibaya lakini prof. Mbele ameona tofauti sana na wewe hivyo hivyo watanzania wengine

Chama muhimu ni culture ya kusema huwezi, hufai, hujui moja kwa moja usoni itaanza lini..bado sana na huko CCM wana culture mwenyekiti ana miaka yake 10 period!
 
Ni vizuri ukaishi katika maisha yatakayofaya umma usianze kuwaza kama (wewe) una akili timamu au zimeruka kidogo!

Umma upi? na akili timamu kwa mujibu wa nani? agh! JF na wapambe wake ni umma then you are kidding!

Mimi nakuona wewe ni mzembe wa kufikiri
 
Watu wanakuja JF na kukandya kwamba JF imepoteza muelekeo, lakini hawafanyi lolote katika kuchangia positively (wanapenda vizuri vilivyoundwa, kuviunda hawataki.)

Ukiuliza maswali magumu lakini yaliyo relevant kuhusu kuwako kwa mungu anayeruhusu maovu duniani unaonekana mtu wa ajabu. By the way unaweza kuona kama nachomekea issue isiyo relevant, lakini matatizo yetu 99% unaweza kuya trace back kwenye hili, the 1% is just for the sake of uncertainty principle and the second law of thermodynamics, nothing is 100%, even nothing is not 100% nothing.

Kila mtu analalamikia serikali wakati book definition ya serikali ni watu wenyewe. Siku ya kupiga kura ikifika less than 50% of eligible voters wana vote.

Kila mtu mtaalam, wanaojua wachache.

Watu wanaongea sana bila kufikiri, wanaoweza kufikiri hawaongei.

Mkuu Kiranga,

Hapo nilipo highlight kwa blue ndio picha halisi tunayoipata kwa watanzania tulio wengi, iwe wanasiasa, makanisani, taasisi za elimu, makazini etc!

Hatuna ule utamaduni wakutulia kusikiliza michango ya wataalam, na kama inakasoro, hatuikosoi kitalaam, tunakosoa kwa kukebehi, kisiasa zaidi! Hapa

JF penyewe unaweza liona hili, watu hawapitii michango ya wenzao kuona wamecomment nini ili waongeze nini, huishia kudandia thread ilipoishia na kuharibu mwelekeo wa thread, tu kwa sababu watu hatuchukui muda wakutosha kupitia michango ya wenzetu! Hii ina maana kwamba isingekuwa kuiandika hapa hii michango badala yake tungekuwa kwenye jukwaa la kuongea moja kwa moja, kuna watu wangechagua kukaa kimya, maana wangezimwa na waliowengi ambao hawajali michango ya wengine!

Labd tu nimalizie hiyo sentensi yako ya mwisho......! Watu wanaongea sana bila kufikiri, wanaoweza kufikiri hawaongei, wakiongea hawasikilizwi, wakisikilizwa, hawayafanyii kazi yaliyozungumzwa, wakiyafanyia kazi, wanaharibu......!
 
Mada nzuri na michango inatia moyo. Naomba kila mmoja wetu aeleze hapa jamvini ataifanyia nini nchi yetu mwaka huu wa 2010.
 
Mkuu Kiranga,

Labd tu nimalizie hiyo sentensi yako ya mwisho......! Watu wanaongea sana bila kufikiri, wanaoweza kufikiri hawaongei, wakiongea hawasikilizwi, wakisikilizwa, hawayafanyii kazi yaliyozungumzwa, wakiyafanyia kazi, wanaharibu......!


Na mimi nimalizie sentensi yako wakiharibu hawajali kitu they dont even bother.....
 
Na mimi nimalizie sentensi yako wakiharibu hawajali kitu they dont even bother.....

...inaweza kuwa na mwendelezo huu.... kama wamepewa dhamana, mwisho wa mhula wanarudi tena kuomba dhamana na wanapewa kwasababu wanaweza kuongea sana......then the cycle goes on and on.....!
 
Sisi ni wavivu wa kufikiria, nani anataka kuumiza akili zake bwana wakati hakuna mtu wa kumhoji chochote (kumbana) endapo atafanya jambo la kipuuzi? mambo ya rahisi rahisi tu - unasign contract ya taifa bila hata kuangalia exit clause, inakuhusu nini hiyo wakati 30% ipo mezani? mtu anathubutu kuiuza Tanganyika kwa vipande vya pesa? nani wa kukuhoji?


hii ni changamoto imeletwa kwetu, hili ni tatizo kubwa sana, naapa bila kubadili hii dhana ya kuchekelea chekelea bila kufikiri why and how hatufiki popote watanzania. Asante MM endelea kutufumbua macho tupo gizani bado.

Na nyie waandishi msikubali kubali tu, uliza - uliza - uliza hadi wakufukuze ofisini kwao, YES. sisi tunakutegema wewe ndiye mjumbe wetu hii pia ni changamoto kwenu kama kweli mna nia njema na taifa hili linazozidi kumongonyoka kila kukicha. Andikeni ukweli au na nyie mnataka kuiuza Tanganyika kwa vipande vya pesa?

Naogopa sana, watoto wetu watakuja kurithi magofu tu ya Tangayika, nchi itakuwa imeshachukuliwa na mabeberu - yaani itakuwa imefyonzwa ibebakia mafupa mitupu - let us start acting on this NOW!
 
" In any country there must be people who have to die. They are the Sacrifices any nation has to make to achieve law and order" -Idi Amin
 
Back
Top Bottom