Idara za CHADEMA zimekufa, chama kipo hoi

NecZec

Member
Jan 23, 2019
23
36
CHADEMA ya sasa inazidi kuwa goigoi japo mpira uko upande wao ila gori hawalioni wafunge gori, iwe makusudi au kwa bahati mbaya.

Kazi anazofanya mwenezi wa mbogamboga ndio kazi ilitakiwa kufanywa na cdm tangu waruhusiwe kufanya mikutano ila cha ajabu walizuga tu wakarudi mijni kimyakimya.

Kero kwa wananchi zimekuwa nyingi na majibu ya serikali yamekuwa mepesi lkn cdm wanashindwa kujenga hoja juu ya kero hizi, idara za chama zimekufa. Kuna mtu pale HQ anaitwa Mrema wanadai eti ndio mwenezi ila ni mweupe mno.

CHADEMA hamna mtu anaeutaka urais, tundulisu amepooza amekuwa sio mtu wa agenda tena,ule moto aliouwasha hadi deep state ikatetemeka kipindi kile leo hii ameuweka benki, chama kinakufa hivyo.

CHADEMA imalisheni idara ndani ya chama chenu kama idara uenezi, idara ya ulinzi na usalama,idara ya fedha na mipango n.k ili mpate watu mahiri ktk idara hizi wakisaidie chama.

Basi endeleeni kuripoti ziara za mwenezi wa mbogamboga.
 
Back
Top Bottom