Watanzania tunapenda mepesi mepesi!

Mada nzuri na michango inatia moyo. Naomba kila mmoja wetu aeleze hapa jamvini ataifanyia nini nchi yetu mwaka huu wa 2010.

Act yangu ya kwanza ni kwenye box la kura naapa hapo simchagui kiongozi mbumbumbu, kibaka na asiye na huruma kwa watanzania maskini.
 
OK. Kwa kuanzia, Watawala wetu wapendwa wamesaini mkataba wa EAC, ambao wananchi hatuutaki.

Is there anything we can do to stop it?
 
Majority ya Watanzania hatutaki Tanzania iwemo kwenye huu mkataba wa EAC.

1. Wachache wanaotaka, big proportion yao ni kutaka waonekane nao "wamekucha"; siyo "waoga" kama sisi majority tunaokataa EAC;
2. wengine wao hawajui kilichoko kwenye huo mkataba wa EAC, wanadhani ni muendelezo wa "ulaji" uliositishwa mwaka 1977,
3. waliobakia ama ni Watanzania kwa paspoti tu, au wananufaika binafsi na mchakato wa EAC.

Sijui wewe Mwanakijiji unaangukia fungu lipi katika hao wanaounga mkono Tanzania kuwemo kwenye EAC.

If you think you have meaningful reason ya kusapoti EAC, na siyo iliyotajwa hapo juu, then post it here!

Mlenge
 
Lakini hata tukiumiza kichwa hakuna linalofanyika ndo maana tumeamua kukaa kimya na kuangalia ...
Mwisho sijui itakuwaje ???
 
Lakini hata tukiumiza kichwa hakuna linalofanyika ndo maana tumeamua kukaa kimya na kuangalia ...
Mwisho sijui itakuwaje ???

Tatizo la Tanzania ni kwamba kila anayejaribu kuumiza kichwa na kushauri lililo jema anaonekana hafai mbele ya wata wala wa CCM. Fikiria mwalimu nyerere aliumiza kichwa na kuanzisha azimio la arusha ili kupunguza rushwa lakini matokeo yake mwinyi na vibaraka wake wakalivunja, leo tunalitamani tena.

Lakini kwa sasa japo wengi tutaumia naona tukiwa na kundi kama la niger delta tunaweza kufanikiwa.
 
We are screwed every where!! The government and its agencies are simply compromised!!
 
Lakini hata tukiumiza kichwa hakuna linalofanyika ndo maana tumeamua kukaa kimya na kuangalia ...
Mwisho sijui itakuwaje ???

Hapana Firstlady1, itakuwa tunaendelea kufanya makosa sana kukaa kimya na kusubiri uamuzi wa mahakama, lazima tusimame na tujitete - watu kama kina MM na wengineo wapo hapa kutupa guidance. sisi walau tuna mwamko tuwasaidie watanzania wenzetu wasiojua lolote linaloendelea katika nchi yetu.

lazima tuamke na tupike makelele - kidogo kidogo yatawaamsha na hao ndugu zetu walioko vijijini.
 
Hatupendi mambo ya kugonganisha vichwa; hatupendi kubishana na kuhojiana hadi mtu akubali kushindwa kwa hoja; tunapenda mambo mepesi mepesi. Angalia Bungeni, mambo yakianza kupamba moto mara Spika anaingilia kati na kutuliza "jazba". Kiongozi akija mbele na kuzungumza na waandishi wa habari badala ya kumbada hadi asikie kizunguzungu tunaona huruma na hatutaki kumuabisha kwa kumbana; tunapenda mepesi mepesi.

Kama wewe ni mwandishi, usitosheke na majibu ya kwanza; tafuta majibu ya pili, angalia kujipinga, angalia kutisha tisha. Tafuta maelezo zaidi; rudi tena na uliza tena hadi wakutimue kwenye ofisi zao!

Tunapenda mambo mepesi mepesi, tunapenda majibu mepesi mepesi. Ndio maana sasa najua kwanini ilikuwa vigumu sana kwa watu kumshinda Nyerere kwa hoja hadi kufikia kudai kuwa "haambiliki". Kumbe walikuwa ni wepesi wepesi. Si tunawaona leo jamani!

Tuamke!
Mzee Mwanakijiji, nimekutana na hii thread katika pita pita yangu, nakubaliana na wewe tunapenda mepesi mepesi sana, hivyo nakushauri kuelekea 2015, rejea nyumbani angalau tupate magumu magumu na mazito mazito!.

By the way, nilikuwa nayatafuta mahojiano yako Dr. Slaa uliyoyaposti humu jf, sikuweza kuipata ile thread.
Kwenye google nimepata haya

  1. [h=3]Mahojiano ya Mwanakijiji na Dk Wilbroad Slaa | Facebook[/h]MICHUZI: Mahojiano ya Mwanakijiji na Dk Wilbroad Slaa
    Mbeya Yetu: MAHOJIANO YA MWANAKIJIJI NA DR.WILBROAD SLAA


  2. More videos for Mahojiano ya Mwanakijiji na Dk Wilbroad Slaa »
    Next Page - PodOmatic | Podcast - KLH News - MAHOJIANO YA DR ...
    Next Page - PodOmatic | Podcast - KLH News - MAHOJIANO YA DR ... ...
    Permalink - PodOmatic | Best Free Podcasts
    Episodes from Sauti ya Mwanakijiji (The Voice of the Villageman ...

    Swali ninalojiuliza, ile thread ya mahojiano haya humu jf, imekwenda wapi?.

    Pasco.
 
Pasco,
Mwanakijiji akirudi kuelekea 2015 ndiyo atawajengea watanzania uwezo wa ghafla?
Mkuu Pasco,katika kuleta hizi clip hapa ni kwa kuwa imekugusa wewe kama mmojawapo wa waandishi wa habari ama? Mzee kama ndivyo hii thread ya leo nahisi hautakua objective
 
Pasco,
Mwanakijiji akirudi kuelekea 2015 ndiyo atawajengea watanzania uwezo wa ghafla?
Mkuu Pasco,katika kuleta hizi clip hapa ni kwa kuwa imekugusa wewe kama mmojawapo wa waandishi wa habari ama? Mzee kama ndivyo hii thread ya leo nahisi hautakua objective
Mkuu Ben, ndio maana nimemshauri MMKJ arudi!, sometimes ni rahisi zaidi kuucheza mpira ukiwa mtazamaji kuliko ukiingia uwanjani!. Kwenye hizo clips kuna kitu natafuta ili kufanyia reference kwenye ile thread humu jf, leo nimeitafuta sijaipata!.
 
Back
Top Bottom