Watanzania tunapenda mepesi mepesi!

  • Thread starter Mzee Mwanakijiji
  • Start date

Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,898
Likes
8,105
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,898 8,105 280
Hatupendi mambo ya kugonganisha vichwa; hatupendi kubishana na kuhojiana hadi mtu akubali kushindwa kwa hoja; tunapenda mambo mepesi mepesi. Angalia Bungeni, mambo yakianza kupamba moto mara Spika anaingilia kati na kutuliza "jazba". Kiongozi akija mbele na kuzungumza na waandishi wa habari badala ya kumbada hadi asikie kizunguzungu tunaona huruma na hatutaki kumuabisha kwa kumbana; tunapenda mepesi mepesi.

Wakati watu kwa maelfu wanazungumzia mambo ya Muro na Kova, bado hatujagusa mambo muhimu ya taifa letu. Tumeshasahau suala la Ndulu na majumba yake; hatujaangalia masuala ya wanafunzi 130 walionusurika kuungua kwa bweni lao (kwa mara nyingine)huko Kilimanjaro; hatujajiuliza hali ya wahanga wa mafuriko imefikia wapi; tunapenda mepesi mepesi.

Tunasikia serikali imelipa watumishi "hewa" shilingi bilioni 7 na ushee na wakati huo huo wametenga bilioni 7 nyingine kwa kombe la dunia (bilioni 14 zimenyweza hizo) huku wanakinga mikono bila haya kuomba bilioni 15 kwa ajili ya miundo mbinu iliyoharibiwa na mafuriko; tunashindwa kuwauliza mbona bajeti yake walisema ni bilioni 7 tu? Tunapenda mepesi mepesi.

Hatupendi kuchukizana. Hatupendi mtu kubishiwa hadi akubali kwamba hoja yake ni ya kipuuzi. Mtu mwenye akili timamu na jina kubwa akisema kitu cha kijinga hatutaki kumuonesha hilo badala yake tunajaribu kumpepea pepea kama waganga wa kienyeji.

Mtu akitokea akisema sana na akizungumza kwa jazba na hoja za nguvu tunakimbilia na kusema "anajiona anajua sana". Na tukiona anatusumbua tunakimbilia kudai kuwa "anatumiwa". Tunapenda mambo mepesi mepesi.

Matokeo yake hata inapokuja mijadala kwenye nafasi zetu za kazi kuhusu miradi au mipango fulani hatutaki kuzama; tunazungumza juu juu tu tukitoka hapo ndio tunazungumza "unajua pale tungefanya hivi" tunabishania pembeni na si vikaoni; hatutaki kumuudhi bosi.

Tunaogopa kuambiwa "tunahatarisha amani na mshikamano"; tunaogopa kuambiwa ati ni "wachochezi". Tukisema mafisadi wote wanyongwe watu wataruka juu kwamba hayo mambo makali; tukisema Kikwete asigombee tena tunaonekana tunapendekeza mbingu kuanguka! Hivyo tunaamua kukaa kimya na kufikiria tu kile tunachotamani.

Matokeo yake tunaburuzwa; tunasukumwa sukumwa tunatikiswa tikiswa na wale wenye uwezo; tunanabakia kama alivyosema mtawala wetu mkuu "kufuata mkumbo". Kwa maneno mengine siye tupo tupo tu.

Nasema tufunguke fikra zetu na mawazo yetu yaachiliwe huru; tufungue vinywa vyetu na kuwapinga watawala wetu. Ukisikia sijui "serikali imesema" usifungue mdomo kama kinda la ndege na kupokea tu bila kuuliza "je ina mantiki, je ni halali, je ina msingi, je je je". Usiende kulalamika pembeni.

Kama wewe ni mwandishi, usitosheke na majibu ya kwanza; tafuta majibu ya pili, angalia kujipinga, angalia kutisha tisha. Tafuta maelezo zaidi; rudi tena na uliza tena hadi wakutimue kwenye ofisi zao! Kama ni mwananchi usikubali kupiga makofi kushangili kitu ambacho hakipo. Ati mnaambiwa mtajengewa mabarabara ya juu kwa juu watu wanachekelea! Ndio maana leo watu bado wanafurahia tu kupiga picha kwenye daraja la pale Manzese kwani wanajiona kidogo imefanana na majuu! Hakuna anayeuliza zile takataka pembeni zitaondolewa vipi!

Tunaambiwa ati tutapewa matreni yanayoenda kwa kasi, wabunge wetu wanaruka ruka kwa furaha kuwa sasa na sisi tumefika. Hawaulizi kesi ya ATCL na Airbus yake imefikia wapi!

Tunapenda mambo mepesi mepesi, tunapenda majibu mepesi mepesi. Ndio maana sasa najua kwanini ilikuwa vigumu sana kwa watu kumshinda Nyerere kwa hoja hadi kufikia kudai kuwa "haambiliki". Kumbe walikuwa ni wepesi wepesi. Si tunawaona leo jamani!

Tuamke!
 
N

Nyauba

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2008
Messages
1,098
Likes
12
Points
135
N

Nyauba

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2008
1,098 12 135
Umegusa ukweli mtupuuu..

Tufanyeje sasa kuondokana na hili kwa haraka ikiwezekana..? umetoa njia sahihii ya kutokutosheka kuhojiii,,namii naanza sasa kuanzia ngazi ya familia hadi kijamiii.

wabunge wetu ndo wanaoiniudhiii zaidiii jamaniiii...ni wepesi, wanafiki, waoga, malimbukeni wa kupigania maendeleo ya wapiga kura wao..Mfumoo mbovuu unaolea kwa nguvuu tabia hiyoooo..wachache bungeni (wapinzani) wameonyesha njia na wanaojiita wapiganaji wa vita ya ufisadi kumbe wenyewee rohoniii ndo mafisadiii zaidii basii tuu kutaka umaarufuuuuu kupitia media nyepesiii tulizonazoooooo..

Inaniuuma sana kiongozi wa serilaki anapohojiwa na waandishii huku wakimpa maswali ya kumpamba na kujipendekezaaaa......

inaniuumaa sana wanaojiita wapiganajii wa ufisadii ili hali wakiendeleaa kubaki chamani ambako uhai ni UFISADIIIII..

Inaniuumaa sana naposhindwaa kuwa jasirii kwa wakati na kupinga yale yotee nisiyopendezwaaa nayoooo...
 
P

Petu Hapa

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2008
Messages
714
Likes
3
Points
0
P

Petu Hapa

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2008
714 3 0
Ufungwaji wa kauli unatengenezwa toka nyumbani. Mtoto akiwa mdogo akijieleza kwanini hataki kufuata maji badala ya dada yake aliyekaa afuate, atagombezwa na kuambiwa anatabia mbaya. Akisema, mama mimi sipendi ukinigombeza, atapewa atafinywa. Akisema sitaki kwenda shule, atalazimishwa sio kuulizwa kwanini! Tunafundisha ukimya, wakati udasisi na misimamo ya nafsi toka utoto inakandamizwa... wakati tunaendelea kusema hayo, tupanue uwigo wa ushiriki toka -- kama katika--- familia tupo hakuna maongezi ya uwazi, katika taifa ndio kabisa.

Uliza watoto juu ya ufisadi-- watakuambia-- wajenge hao-- you will be suprised the change you can make in few years.
 
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Messages
2,505
Likes
32
Points
135
Gembe

Gembe

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2007
2,505 32 135
Ndiyo ;

Tunapenda mapesi mepesi kwa kuwa tumekuwa tunapewa mambo mepesi mepesi na viongozi wetu na tunawakubalia.

Kuna suala la Mkurugenzi wa TANESCO mpaka sasa hajulikana ataanza lini;hatuhoji atuulizi na watu wanaendelea kusafiri kwenda ugaibuni bila kukamalisha yalliyo mepesi.

Wakati mwingine huwa nafikiria tumelogwa ;la hasha inawezekana labda ni kwa bahati mbaya tuna akili ya kusahau mapema?

Je tuwazilie Nchi au tuanze upya?

Mwanakijiji check PM
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,745
Likes
2,035
Points
280
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,745 2,035 280
Hatutaki kuumiza vichwa kabisa. Tumeridhika na yale yanayotuzunguka hata kama kila siku moja inapoondoka hali zetu zinazidi kuwa mbaya.
Kuamka kwetu hakutakuja bila ya kujua umuhimu wa kuanza kutumia vichwa vyetu kufikiri ipasavyo katika kutatua matatizo yanayotuzunguka. Tuachane na tabia mbaya ya kuwa kina yes men katika kila kitu for no good reasons.
 
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2008
Messages
3,158
Likes
22
Points
135
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2008
3,158 22 135
Mkuu,

Matatizo yanayolikumba taifa hili ni mengi mno, tunashindwa sasa tuanze na lipi, tushike lipe, tukamatane na lipe, tuachane na lipi. Ukimata hili, unaona lile nila moto zaidi, unaangusha lililopo na kulikimbilia lile, ukishika hilo, lingine linaibuka........! ndo maana tumebaki kutapatapa na kutafuta sehemu ya kufia......!
 
bht

bht

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
10,335
Likes
215
Points
160
bht

bht

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
10,335 215 160

Binamu kukugongea nimeona haitoshi nasemea hapa "thanks"...............

Tushike lipi tuache lipi??????? mwisho wake ndo huuuu tumeachia yote. liwalo na liwe!!!!!!!!!!! ndo tulipofikia!!!!!!!!!!
 
M

Mundu

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2008
Messages
2,720
Likes
34
Points
145
M

Mundu

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2008
2,720 34 145
Tuanze kwenye hii forums, waanzisha mada na wachangiaji wawe wamejiandaa na si kukurupuka. Watu waweze kuzipitia lakini si kuchangia changia tu. Tunataka ubunifu wa mawazo na fikra zilizozama, yasiwe mambo ya kishabiki na kufuata mkumbo.

Kama hujaweza changia, subiri katafakari, kasome, kabukue, utakuja changia kesho.

Mapinduzi ya kweli yatapatikana tu kama watu watafanya kazi, na kazi yenye tija. Kazi yenye tija yahitaji fikra dodoso (proactiveness), haihitaji kukurupuka (Reactiveness). Tukifanya mambo yetu vilevile siku zote, hatuwezi kupata mafanikio tofauti.

Tusikubali kila kitu. let us challenge the status quo.
 
GY

GY

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Messages
1,280
Likes
0
Points
133
GY

GY

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2009
1,280 0 133
Tukipenda magumu magumu:-

  • Tunabambikiwa kesi na kupoteza muelekeo wa maisha hivyo kuwaletea tabu wanaotutegemea (familia n.k)
  • Tunakuwa kwenye imaginary world ambayo haiko supported na any system iliyopo nchini, hivyo tunakuwa si sehemu ya chochote kinachotokea
  • Tunatengwa, tunanyanyapaliwa, tunasengenywa, tunaadhibiwa.
  • Tunakuwa kisiwa (sio Zanzibar)
  • Tunakuwa wagumu, wakati mwingine hata wa kuelewa na kubadilika
  • Tunatofautiana na watawala (CCM) na hivyo kujenga uadui na wenye nchi na wenye dola, athari zake kila mtu anazijua
  • Tutakuwa wagumu wagumu
 
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2008
Messages
3,158
Likes
22
Points
135
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2008
3,158 22 135
Binamu kukugongea nimeona haitoshi nasemea hapa "thanks"...............

Tushike lipi tuache lipi??????? mwisho wake ndo huuuu tumeachia yote. liwalo na liwe!!!!!!!!!!! ndo tulipofikia!!!!!!!!!!
Umeona mpwazz eeeh?.....!

Yaaani kuna miissue mingi acha tu! kwa mfano after Muro's Sagga....ningependa nikomae na huyu Michael Wage....ambaye hapo Moro ana Mihotel, Lodges every where ana alikuwa a mere Government employee......ikagundulika amefuja mali kule Bagamoyo, akatimuliwa na PM.

Je, adhabu ya Michael Wage inaishia kutumuliwa tu au inatwakiwa hayo Ma-GWAMI Hotels ya Morogoro yafilisiwe including his unfished 6 storey building Morogoro? Kuna watu wa TISS wanafuatilia hili au waandishi wa habari wanafuatilia hili au wakamatana kwanza na hili jepesi la kumhoji Muro na Wage tu imetoka?

....yaani mambo ni mengim, mengi......!sijui hata tunatokaje huko!
 
Kimbweka

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Messages
8,609
Likes
56
Points
145
Kimbweka

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2009
8,609 56 145
Tufanyeje Watanzania ili tubadilike tusipende Mepesi mepesi na vizazi vyetu vijavyo, Vyepesi vyepesi vyaelea havina nguvu ya kuzama ndani na kujua yaliyomo, tusipende vyepesi vyepesi......................
 
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
1,492
Likes
285
Points
180
Mwalimu

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
1,492 285 180
Mabadiliko lazima yaanze na mtu mmoja mmoja binafsi, kila mmoja wetu aamue kubadilika kifikra, tuamue kubadilika kuanzia ngazi ya chini kabisa ya kaya. Watu lazima wawe na mwamko wa kusema hiki nataka na hiki sitaki hata kwa fimbo! Tusikubali unyonge wetu utufanye tuwe tunakubali mambo kama kondoo.
-Tunapakiwa kwenye hiace abiria wanne mbele pamoja na dereva tunakaa kimya,
-Tunapakiwa abiria wawili au hata watatu kwenye pikipiki (mshikaki) tunakaa kimya,
-Dereva wa basi la abiria akiendesha hovyo tunakaa kimya tunaogopa tukisema tutaambiwa tupande teksi
Ikiwa mambo madogo haya yanatushinda sembuse hayo makubwa?
Bila sisi wenyewe kusimama ngangari na kuwa na guts za kusema hili ni sawa na hili halikubaliki lazima tutaendelea kuwa wanyonge wa kutupwa!
 
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Messages
12,286
Likes
65
Points
145
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2009
12,286 65 145
mimi naomba niendelee na haya ''mepesi mepesi'' KWA AFYA YANGU TAFADHALI,lol...!

waliopenda mazito mazito tathmini zinaonyesha kuwa:
-WAMEPROVE FAILURE

-WENGINE IMAWAGHARIMU MAISHA(wameuawa/wamekufa kwa mazingira ya kinamna namna)

lol!
muhudumu niongezee kinywaji tafadhali....!:D
 
bht

bht

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
10,335
Likes
215
Points
160
bht

bht

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
10,335 215 160
mimi naomba niendelee na haya ''mepesi mepesi'' KWA AFYA YANGU TAFADHALI,lol...!

waliopenda mazito mazito tathmini zinaonyesha kuwa:
-WAMEPROVE FAILURE

-WENGINE IMAWAGHARIMU MAISHA(wameuawa/wamekufa kwa mazingira ya kinamna namna)

lol!
muhudumu niongezee kinywaji tafadhali....!:D
heheeeee mtarajiwa. maisha burudaaaaaaaaaaaaaaaani!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Utamaduni

Utamaduni

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Messages
1,215
Likes
220
Points
160
Utamaduni

Utamaduni

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2007
1,215 220 160
Nakumbuka usemi wa kondakta wa daladala aliyekuwa anataka kupigana na abiria wakati anadai nauli yake alisema......

TANZANIA HII HAKUNA AMANI, UKITAKA AMANI DAI CHAKO

akiunganisha kwamba, kulikuwa na amani katika daladala kwasababu hakudai nauli, lakini alipoanza kudai amani ikatoweka kutokana na baadhi ya abiria kutotaka kumlipa.

Na hii inaendana kabisa na ukweli wa nchi yetu ilivyo, watanzania ni waoga sana kudai haki zetu kwa kuwa tunataka kulinda AMANI ambayo ipo katika maandishi na maneno ya watu tu, tunaletewa stori kila leo ili kusahau stori iliyopita na tusijisumbue kuuliza mwisho wake, tazama kuanzia sakata la RICHMOND, CHENGE KUUA WALE WADADA WAWILI KWA AJALI YA GARI (sijui iliishia wapi, kesi bado ipo) etc etc etc,

Yote hii ni kutupoteza maboya tu..... na sisi tunakubali yaishe ili "AMANI" inayoongelewa izidi kuwepo
 
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2008
Messages
7,495
Likes
104
Points
160
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2008
7,495 104 160
Tumelelewa na Viongozi waasisi wa Taifa hili kufikiri kwa niaba yetu; kutenda kwa niaba yetu; kuamua kwa niaba yetu;.....
Tumefundishwa kuitikia "ndio mzee" kwa kila tutakalohojiwa!
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,745
Likes
2,035
Points
280
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,745 2,035 280
Tumelelewa na Viongozi waasisi wa Taifa hili kufikiri kwa niaba yetu; kutenda kwa niaba yetu; kuamua kwa niaba yetu;.....
Tumefundishwa kuitikia "ndio mzee" kwa kila tutakalohojiwa!
Yes men people..ndio mzee culture vimechangia kuwa na watu wanafiki wasio kifani. Tumeweka mazingira ya bora niseme yes niendelee kukua kikazi na nipate kipato changu cha kutosha.
 
Kisoda2

Kisoda2

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2008
Messages
1,773
Likes
433
Points
180
Kisoda2

Kisoda2

JF-Expert Member
Joined May 30, 2008
1,773 433 180
Hatupendi mambo ya kugonganisha vichwa; hatupendi kubishana na kuhojiana hadi mtu akubali kushindwa kwa hoja; tunapenda mambo mepesi mepesi. Angalia Bungeni, mambo yakianza kupamba moto mara Spika anaingilia kati na kutuliza "jazba". Kiongozi akija mbele na kuzungumza na waandishi wa habari badala ya kumbada hadi asikie kizunguzungu tunaona huruma na hatutaki kumuabisha kwa kumbana; tunapenda mepesi mepesi.

Wakati watu kwa maelfu wanazungumzia mambo ya Muro na Kova, bado hatujagusa mambo muhimu ya taifa letu. Tumeshasahau suala la Ndulu na majumba yake; hatujaangalia masuala ya wanafunzi 130 walionusurika kuungua kwa bweni lao (kwa mara nyingine)huko Kilimanjaro; hatujajiuliza hali ya wahanga wa mafuriko imefikia wapi; tunapenda mepesi mepesi.

Tunasikia serikali imelipa watumishi "hewa" shilingi bilioni 7 na ushee na wakati huo huo wametenga bilioni 7 nyingine kwa kombe la dunia (bilioni 14 zimenyweza hizo) huku wanakinga mikono bila haya kuomba bilioni 15 kwa ajili ya miundo mbinu iliyoharibiwa na mafuriko; tunashindwa kuwauliza mbona bajeti yake walisema ni bilioni 7 tu? Tunapenda mepesi mepesi.

Hatupendi kuchukizana. Hatupendi mtu kubishiwa hadi akubali kwamba hoja yake ni ya kipuuzi. Mtu mwenye akili timamu na jina kubwa akisema kitu cha kijinga hatutaki kumuonesha hilo badala yake tunajaribu kumpepea pepea kama waganga wa kienyeji.

Mtu akitokea akisema sana na akizungumza kwa jazba na hoja za nguvu tunakimbilia na kusema "anajiona anajua sana". Na tukiona anatusumbua tunakimbilia kudai kuwa "anatumiwa". Tunapenda mambo mepesi mepesi.

Matokeo yake hata inapokuja mijadala kwenye nafasi zetu za kazi kuhusu miradi au mipango fulani hatutaki kuzama; tunazungumza juu juu tu tukitoka hapo ndio tunazungumza "unajua pale tungefanya hivi" tunabishania pembeni na si vikaoni; hatutaki kumuudhi bosi.

Tunaogopa kuambiwa "tunahatarisha amani na mshikamano"; tunaogopa kuambiwa ati ni "wachochezi". Tukisema mafisadi wote wanyongwe watu wataruka juu kwamba hayo mambo makali; tukisema Kikwete asigombee tena tunaonekana tunapendekeza mbingu kuanguka! Hivyo tunaamua kukaa kimya na kufikiria tu kile tunachotamani.

Matokeo yake tunaburuzwa; tunasukumwa sukumwa tunatikiswa tikiswa na wale wenye uwezo; tunanabakia kama alivyosema mtawala wetu mkuu "kufuata mkumbo". Kwa maneno mengine siye tupo tupo tu.

Nasema tufunguke fikra zetu na mawazo yetu yaachiliwe huru; tufungue vinywa vyetu na kuwapinga watawala wetu. Ukisikia sijui "serikali imesema" usifungue mdomo kama kinda la ndege na kupokea tu bila kuuliza "je ina mantiki, je ni halali, je ina msingi, je je je". Usiende kulalamika pembeni.

Kama wewe ni mwandishi, usitosheke na majibu ya kwanza; tafuta majibu ya pili, angalia kujipinga, angalia kutisha tisha. Tafuta maelezo zaidi; rudi tena na uliza tena hadi wakutimue kwenye ofisi zao! Kama ni mwananchi usikubali kupiga makofi kushangili kitu ambacho hakipo. Ati mnaambiwa mtajengewa mabarabara ya juu kwa juu watu wanachekelea! Ndio maana leo watu bado wanafurahia tu kupiga picha kwenye daraja la pale Manzese kwani wanajiona kidogo imefanana na majuu! Hakuna anayeuliza zile takataka pembeni zitaondolewa vipi!

Tunaambiwa ati tutapewa matreni yanayoenda kwa kasi, wabunge wetu wanaruka ruka kwa furaha kuwa sasa na sisi tumefika. Hawaulizi kesi ya ATCL na Airbus yake imefikia wapi!

Tunapenda mambo mepesi mepesi, tunapenda majibu mepesi mepesi. Ndio maana sasa najua kwanini ilikuwa vigumu sana kwa watu kumshinda Nyerere kwa hoja hadi kufikia kudai kuwa "haambiliki". Kumbe walikuwa ni wepesi wepesi. Si tunawaona leo jamani!

Tuamke!
Mkuu nimekugongea kale ka thenks.
Ngoja nikaperuzi ndo nije changia.
 
Abunwasi

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Messages
4,051
Likes
1,802
Points
280
Abunwasi

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2009
4,051 1,802 280
Mzee anasema tusitafute majibu rahisi kwa matatizo yetu. Amenena amenena amenena ugonjwa huu ndiyo chanzo cha matatizo yetu yote[kuanzia kwa wanasiasa,wasomi,wataalam,wananchi etc etc].
 
TANMO

TANMO

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Messages
8,958
Likes
338
Points
180
TANMO

TANMO

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2008
8,958 338 180
Kwa asili huwa hatuna uwezo wa kubeba mambo mengi kichwani kwa wakati mmoja ndiyo maana kila jambo jipya linaloibuka hutusahaulisha kabisa kuhusu tulilokuwa tunalishughulikia, ndiyo maana hata miradi mingi huwa inaishia hewani au hutulazimu kuimaliza haraka haraka ili turukie miradi mingine, ubora kwetu hauna umuhimu sana bali kumaliza jukumu ndiyo lengo letu.

Pia usisahau kuwa kwa asili sisi ni walalamikaji zaidi hata kwa mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wetu huwa tunalaumu wenzetu kwa kutukwamisha kuyafanya. Mahosiptali yetu hayana madawa wala vifaa na mashule yetu hayana madawati kwa sababu wafadhili wanatucheleweshea pesa za misaada, tukizipata yanakuwa yameshaibuka mengine ya kushughulikia kwa wakati huo, rais wa nchi anaweza kuwa mgonjwa hivyo hutubidi tumpeleke nje kwenda kutibiwa hivyo pesa tulizopaswa kununulia vifaa vya hosiptali hutulazimu kuzielekeza kwenye matibabu. Raisi wa nchi anaweza kuhitaji mapumziko kutokana na kazi ngumu anayoifanya kutumikia wananchi wake hivyo hutulazimu kumpeleka akabembee kidogo ili arifreshi akili na mwili. Au muda wa kuanza kwa kombe la dunia unakuwa umewadia hivyo inatubidi tutenge fungu la kuitangaza nchi na faida tutakayopata baada ya hapo tunaweza kuielekeza kwenye ununuzi wa madawati hivyo wanafunzi wetu wavumilie kama miaka mitano ijayo wataweza kufikiriwa angalau kukalia madawati, akina mama wanaojifungua waendelee kuvumilia kwa kushea vitanda mahospitalini muda si mrefu kila mmoja atalalia kitanda chake iwapo tu pesa zitapatikana na kutakuwa hakuna jambo la kuzifanyia kwa wakati huo.

Pia Bwana Mwanakijiji usisahau kuwa hatuna tena haja ya kufikiri kwa sababu kuna wazungu ambao siku zote huwa wanafikiri kwa niaba yetu, hata wanapopitisha bajeti zao siku zote kuna fungu kwa ajili yetu nchi masikini.
 
Forum statistics

Threads 1,250,458
Members 481,354
Posts 29,733,803