Watanzania tulipotembelea nchi za kigeni na kuwaeleza asili yetu, walifurahi sana wakatutania wajukuu wa Mwl Nyerere

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,541
Reaction score
916
Watanzania tunapotembelea nchi za kigeni na kuwaeleza asili yetu, wanafurahi sana nakututania wajukuu wa Mwl Nyerere na hii ndiyo sababu kubwa inayonifanya niheshimu sana nchi ya Tanzania na nishindwe kamwe kukosea adabu Chama Cha Mapinduzi cha Babu yetu Mwl Nyerere

Ni vigumu sana kutamka Chama Cha Mapinduzi pasipokutamka baba wa Taifa

Inawezekana ningekosa adabu labda kama nisingekuwa nimesafiri kwenda nchi za Kigeni lakini kwa heshima ya wageni wanayotupatia na hasa wakigundua sisi ni Watanzania hakika inatugusa sana

Safari yangu ya mwisho ya Afrika katika nchi ya Rwanda ilinigusa sana kwasababu raisi wa Rwanda Paul Kagame alimzungumzia Mwl Nyerere kwa hisia kubwa akilenga namna gani Tanzania imekuwa nchi ya kuigwa mfano hasa wanapokumbuka undugu na ujamaa kati yetu

Wakati mwingine tunapofika Wiingereza na Marekani tunatokwa na machozi kwasababu Wazungu wanatueleza historia ya uhusiano wao na baba wa Taifa Mwl Nyerere na hasa Chama cha Mapinduzi wakitueleza jinsi baba wa Taifa alivyokuwa akiwasumbua wakati akiomba uhuru

Tulipokuwa Wiingireza Wazungu walituonesha sare za Chama cha Mapinduzi za mwaka 1995 kwakweli tukapigwa butwaa

Walitueleza baba wa Taifa aliwapa sare hizo kama zawadi ili wajionee hatua za maendeleo ya Chama chake na Tanzania kwa ujumla

Kwakweli kitendo hicho kilitutoa machozi kila mmoja wetu, akina dada tuliokuwa nao walilia sana hata tukashindwa tufanyaje

Na hii ndiyo sababu pekee katika maisha yangu inayonifanya niheshimu sana Chama Cha Mapinduzi nikiamini kuwa napaswa kumpa baba yetu wa Taifa heshima yake

Kwahiyo binafsi naheshimu CCM kwasababu ya heshima ya baba wa Taifa na sio uchawa kama baadhi ya Watanzania wanavyonituhumu

Naamini kuwa baba wa Taifa anapaswa kupewa heshima yake na hasa katika mambo yake yote aliyoanzisha hasa Chama Cha Mapinduzi na miradi ya Taifa la Tanzania

Labda kama vijana tungekuwa na Chama chetu cha kisela sela tungeweza kudhalilishana humo na kukabana koo lakini Chama cha Mwl Nyerere kamwe sithubutu, mtanisanehe!

Babu apewe heshima yake!

Vijana mkianzisha Chama cha kisela sela niiteni lakini cha Mwl Nyerere CCM tukipe heshima yake
 
Watanzania tulipotembelea nchi za kigeni na kuwaeleza asili yetu, walifurahi sana wakatutania wajukuu wa Mwl Nyerere na hii ndiyo sababu kubwa inayonifanya niheshimu sana nchi ya Tanzania na nishindwe kamwe kukosea adabu Chama Cha Mapinduzi cha Babu yetu Mwl Nyerere

Ni vigumu sana kutamka Chama Cha Mapinduzi pasipokutamka baba wa Taifa

Inawezekana ningekosa adabu labda kama nisingekuwa nimesafiri kwenda nchi za Kigeni lakini kwa heshima ya wageni wanayotupatia na hasa wakigundua sisi ni Watanzania hakika inatugusa sana

Safari yangu ya mwisho ya Afrika katika nchi ya Rwanda ilinigusa sana kwasababu raisi wa Rwanda Paul Kagame alimzungumzia Mwl Nyerere kwa hisia kubwa akilenga namna gani Tanzania imekuwa nchi ya kuigwa mfano hasa wanapokumbuka undugu na ujamaa kati yetu

Wakati mwingine tulipofika Wiingereza na Marekani tulitokwa na machozi baada ya Wazungu kutueleza historia ya uhusiano wao na baba wa Taifa Mwl Nyerere na hasa Chama cha Mapinduzi wakitueleza jinsi baba wa Taifa alivyokuwa akiwasumbua wakati akiomba uhuru

Tulipokuwa Wiingireza Wazungu walituonesha sare za Chama cha Mapinduzi za mwaka 1995 kwakweli tukapigwa butwaa

Walitueleza baba wa Taifa aliwapa sare hizo kama zawadi ili wajionee hatua za maendeleo ya Chama chake na Tanzania kwa ujumla

Kwakweli kitendo hicho kilitutoa machozi kila mmoja wetu, akina dada tuliokuwa nao walilia sana hata tukashindwa tufanyaje

Na hii ndiyo sababu pekee katika maisha yangu inayonifanya niheshimu sana Chama Cha Mapinduzi nikiamini kuwa napaswa kumpa baba yetu wa Taifa heshima yake

Kwahiyo binafsi naheshimu CCM kwasababu ya heshima ya baba wa Taifa na sio uchawa kama baadhi ya Watanzania wanavyonituhumu

Naamini kuwa baba wa Taifa anapaswa kupewa heshima yake na hasa katika mambo yake yote aliyoanzisha hasa Chama Cha Mapinduzi na miradi ya Taifa la Tanzania

Labda kama vijana tungekuwa na Chama chetu cha kisela sela tungeweza kudhalilishana humo na kukabana koo lakini Chama cha Mwl Nyerere kamwe sithubutu, mtanisanehe!

Babu apewe heshima yake!

Vijana mkianzisha Chama cha kisela sela niiteni lakini cha Mwl Nyerere CCM msiniite kwasababu namheshimu sana
Nyerere alikuwa mpuuzi mmoja tu
 
CCM ilikuwa imejifia tayari baada ya Mwalimu kuondoka madarakani... Mtu pekee alirudisha imani kwa CCM kuheshimiwa tena ni Magufuli..
 
Hizi nchi za Kigeni wakigundua wewe ni mtanzania wanakutania Jukuu la Mwl Nyerere pia CCM wanaifahamu sana kwasababu ya baba wa Taifa
Afadhali waendelee kukijenga wasikubali kiharibike mana historia yake ni kubwa sana
 
Sasa hivi tumekuwa watoto wa mama wa kambo
Wasikubali mambo yaharibike kwasababu macho yanayotazama Tanzania ni mengi sana na yanatokana na baba wa Taifa
 
yalishaharibika, hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujifanya hayapo
 
Hivi huko hakuna comrade mwendawazimu anyooshe mambo ili heshima juu ya CCM irudi
 
Mimi mwenyewe nilikua nafikiri hivyo kuhusu Tanzania inavyoonwa nchi za wenzetu,ila ukweli ni kwamba watu wengi hata hawajui kama Kuna nchi inaitwa Tanzania
 
Ukitaka wakufahamu haraka pita nchi zote alizopita Nyerere hasa Wiingereza

Wiingereza ukisema CCM ya Mwl Nyerere wanakuelewa haraka

Au sema tu Mwl Nyerere
 
Huyu nae ni nyumbu umeleta maharisho gani hapa, au hukumsikia huyo mzee akisema ccm si baba yangu wala mama yangu, unafikiri kwa hiyo kauli alikuwa na maana gani?
 
Mwl Nyerere au? Nikumbushe
 
Mwl Nyerere au? Nikumbushe
Ndiyo ni Mwl, kwa kauli hiyo alimaanisha kwamba japo ccm ni chama chake na yeye ni miongoni mwa waasisi wa ccm hapo awali TANU, endapo kitakiuka haki za binadamu na kutoheshimu misingi ya wananchi, hana budi hata yeye kukikataa maana chama hicho si baba yake wala mama yake na yeye alikuwa anapigania uhuru wa wananchi na si uhuru wa chama kimoja pekee, wewe ni nani uendelee kukaza fuzu, namana ukosefu wa haki na umwagaji damu unao endelea nchini hauoni hata kama ni kipofu nako husikii?
 
upuuzi mtupu
usilete upupu wako hapa, mzungu akae na jezi ya mbogamboga aifaunyie nini
Kwanza UK na US hata hawamjui huyo nyerere wala ccm na narudia hawamjui na wala hawataki kujua...
 
Kumbe akizungumza hayo siyo nashukuru sana kwa kunikumbusha
 
upuuzi mtupu
usilete upupu wako hapa, mzungu akae na jezi ya mbogamboga aifaunyie nini
Kwanza UK na US hata hawamjui huyo nyerere wala ccm na narudia hawamjui na wala hawataki kujua...
Nitakuwa muongo kukupotosha kuwa Wiingereza na Marekani hawamfahamu Mwl Nyerere
 
Back
Top Bottom