Watanzania tujikite kwenye uzalishaji tupunguze uchuuzi na biashara za ujanja ujanja

twende kazi

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,520
459
Wakuu salaamu,
Kichwa cha habari kinahusika.Ukisoma kwenye kijitabu cha muongozo cha kituo cha uwekezaji Tanzania 2013-2014(Tanzania investment guide book 2013-2014) utaona kwamba nchi yetu ina maeneo mengi sana mazuri kwa ajili ya shughuli za kilimo na nyenginezo.Nanukuu toka kwenye kijitabu'

Potential irrigable
farmland in Tanzania is approximately 29
million hectares, out of which only 280,000
hectares are under irrigation farming'.

Lakini watu wengi wamejikita katika shughuli za uchukuzi,za kiujanja ujanja na utapeli mara sijui thailand mara china sijui uganda wakati Bongo hii fursa kibao.Nina uhakika kama tutaamua kuwekeza nguvu kubwa kwenye kuitumia ardhi iyo bila shaka tungekuwa mbali sana.Tatizo kubwa ni uthubutu.Tutafakari.
 
Vijana sasa hivi wanajua maisha ni Udereva pikipiki na kufanya uchuuzi kwenye stand za basi. Kuna ubunifu unakosekana, lakini serikali yetu haisaidii vijana kabisa. Kwa hali hii itakuwa rahisi vijana kwenda msituni/uhasi iwapo atapatikana mfadhili
 
kweli kabisa bado serikali hawaja toa ushirikiano wa kutosha ktk kusaidia watu wanaoingia ktk kilimo
 
Hilo Ndo Tatizo kubwa kwa Wabongo, Tumejikita kufanya uchuuzi, kuuza Bidhaa za nje, Na ukijaribu kumsoma Aliko Dangote anakuambia moja ya biashara ambazo zinaweza kukufanya uwe tajiri basi ni kazi za Procesing, na si ku chuuza, Huwezi ukafanya uchuuzi halafu uwe tajiri hata siku moja
 
Vijana sasa hivi wanajua maisha ni Udereva pikipiki na kufanya uchuuzi kwenye stand za basi. Kuna ubunifu unakosekana, lakini serikali yetu haisaidii vijana kabisa. Kwa hali hii itakuwa rahisi vijana kwenda msituni/uhasi iwapo atapatikana mfadhili

Mkuu Kakende sio kwamba napingana na hoja yako ila nafikiri ni vizuri tuchangamkie fursa zilizopo kama mleta uzi huu anavyotuasa. Kwa mtazamo wangu tuache kujifariji kwa kuitupia serikali lawama. Hata serikali ingetusaidia vipi kama mtu huna juhudi binafsi ya kujiongeza huwezi kufanikiwa. Vijana wenzangu tuchangamke. Wakati wa kutenda ni sasa.
 
Wakuu salaamu,
Kichwa cha habari kinahusika.Ukisoma kwenye kijitabu cha muongozo cha kituo cha uwekezaji Tanzania 2013-2014(Tanzania investment guide book 2013-2014) utaona kwamba nchi yetu ina maeneo mengi sana mazuri kwa ajili ya shughuli za kilimo na nyenginezo.Nanukuu toka kwenye kijitabu'

Potential irrigable
farmland in Tanzania is approximately 29
million hectares, out of which only 280,000
hectares are under irrigation farming'.

Lakini watu wengi wamejikita katika shughuli za uchukuzi,za kiujanja ujanja na utapeli mara sijui thailand mara china sijui uganda wakati Bongo hii fursa kibao.Nina uhakika kama tutaamua kuwekeza nguvu kubwa kwenye kuitumia ardhi iyo bila shaka tungekuwa mbali sana.Tatizo kubwa ni uthubutu.Tutafakari.

Mkuu em tupatie taarifa zaidi kuhusu hiyo guide mana mi ndo naiskia kwako,,ni kitu gani na mchakato wake kwa ujumla ukoje?
Wengine roho za uthubutu tunazo ila ndo hatukutani na fursa za kueleweka
 
Wakuu salaamu,
Kichwa cha habari kinahusika.Ukisoma kwenye kijitabu cha muongozo cha kituo cha uwekezaji Tanzania 2013-2014(Tanzania investment guide book 2013-2014) utaona kwamba nchi yetu ina maeneo mengi sana mazuri kwa ajili ya shughuli za kilimo na nyenginezo.Nanukuu toka kwenye kijitabu'

Potential irrigable
farmland in Tanzania is approximately 29
million hectares, out of which only 280,000
hectares are under irrigation farming'.

Lakini watu wengi wamejikita katika shughuli za uchukuzi,za kiujanja ujanja na utapeli mara sijui thailand mara china sijui uganda wakati Bongo hii fursa kibao.Nina uhakika kama tutaamua kuwekeza nguvu kubwa kwenye kuitumia ardhi iyo bila shaka tungekuwa mbali sana.Tatizo kubwa ni uthubutu.Tutafakari.

Ndugu yangu mwakajana watu tuliwekeza kwenye kilimo mfano wilaya ya kilombero tulizalisha mpunga kiasi kikubwa sana watu wakawa wana sema sasa umaskini bai!!!!! Cha ajabu serikali ikaruhusu makampuni makubwa walete mchele toka theiland na ukafurika na wakafunga mipaka mchele wa Tanzania usiuzwe nje wakati watu huko Ethiopia wananjaa. Sasa mpunga umebaki umelundikana hakuna pa kupeleka watu tunalia tumekata mitaji hivi unadhani serikali hii inania njema na wakulima? Kwa hali hii bado utamshawishi mtu awekeze kwenye kilimo?
 
Vijana sasa hivi wanajua maisha ni Udereva pikipiki na kufanya uchuuzi kwenye stand za basi. Kuna ubunifu unakosekana, lakini serikali yetu haisaidii vijana kabisa. Kwa hali hii itakuwa rahisi vijana kwenda msituni/uhasi iwapo atapatikana mfadhili

dah,mkuu iyo avatar yako vp?
 
Ndugu yangu mwakajana watu tuliwekeza kwenye kilimo mfano wilaya ya kilombero tulizalisha mpunga kiasi kikubwa sana watu wakawa wana sema sasa umaskini bai!!!!! Cha ajabu serikali ikaruhusu makampuni makubwa walete mchele toka theiland na ukafurika na wakafunga mipaka mchele wa Tanzania usiuzwe nje wakati watu huko Ethiopia wananjaa. Sasa mpunga umebaki umelundikana hakuna pa kupeleka watu tunalia tumekata mitaji hivi unadhani serikali hii inania njema na wakulima? Kwa hali hii bado utamshawishi mtu awekeze kwenye kilimo?

Uliyosema ni kweli kabisa. Kuna mtu moja liwahi kuniambia kuwa kwa Tanzania ukiitwa Mkulima ni sawa na kukutukana kuwa huna akili.

Serikali yetu (yaani wanasiasa wa chama tawala) inadhani ina hisa katika kila jasho la mkulima. Wanachofanyiwa wakulima wadogo mara nyingi ni ukatili wa hali ya juu kabisa. Serikali inazuia kuuza mazao ya wakulima nje lakini haiyanunui. Nasikia kule Songea serikali ilichukua mazao ya wakulima na kukaa nayo kwa muda halafu baadaye waliambiwa wakayachukue serikali haina pesa.

Kila mkulima analima ili apate pesa za kujikwamua kwenye mambo kama ada za shule, nguo, nk. Serikali haioni hilo. Huko mkoani utakuta tu Mkuu wa Mkoa au Wilaya anatangaza kuwa hakuna kuuza mahindi mabichi kwa kuwa amesikia mavuno yatapungua, n.k.

Kinachotakiwa ni vyama vya wakulima kama TCCIA kupigania haki ya kila mkulima kuuza jasho lke bila kujali wapi kuna njaa Tanzania. Ili serikali kujinusuru na tatizo litakalojitokeza basi serikali inunue mazao kutoka kwa wakulima kila mwaka na ijenge maghala (silos) makubwa ambayo yatahifadhiwa.
 
Back
Top Bottom