Ninaomba sana Serikali yetu na vyombo vinavyo husika na michezo Tanzania tupunguze matamko Bali tujikite kwenye Sheria

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,267
33,871
TANZANIA NI TAIFA HURU LINAKOFUATA SHERIA ZA NCHI NA KANUNI ZILIZOKUBALIKA

Mimi ni kiongozi wa Kiroho katika Daraja la Uaskofu

Majina yangu ni Rev Liberatus W Sasabo

Nipo Mkoani Iringa Nyanda za Juu Kusini Nchini Tanzania

Pia na Mimi Ni mdau wa Soka hapa Tanzania na Mwanachama ya Timu ya Yanga Sports Club

HAYA NI MAWAZO YANGU

Ninaomba sana kueleweka Vizuri na Siyo Vibaya;

Ninaomba sana Serikali yetu na vyombo vinavyo husika na michezo Tanzania tupunguze matamko Bali tujikite kwenye Sheria, kanuni na Mwongozo wa Soka Duniani (FIFA)

Jana nimemsikiliza Sana Mbunge na waziri Mkuu Mh Majaliwa Kassim Majaliwa

Akiagiza Bungeni kuwa wahusika waangalie kupanga tarehe nyingjne ya kurudiwa mchezo wa Yanga na Simba

MASWALI YANGU

(1) Kwani mchezo urudiwe?

(2) Nani alisababisha kutokuchezwa Mechi huyo?

(3) Alipata maelezo kutoka kwa Nani?

(4) Je alikuwa hajui la Kanuni na Sheria za kuendesha Soka Duniani?

(5) Ilikuwa Ni kwa manufaa ya Nani na kwa nini?

(6) Kwa nini tunataka Mechi huyo irudiwe tu kwa faida ya nani na kwa Kanuni ipi hapo sasa?

(7) Kwa Nini tutoe hukumu ya Pili kabla ya hukumu ya Kwanza?

(8) Unarudia Mchezo kwa Kanuni ipi na kwa kosa gani hapo?

(9) Kila Timu iliingia uwanjani kwa mda wake kulingana na Kanuni za Soka Duniani; na Maelekezo ya Wakubwa wavunja Kanuni za Soka Duniani;

(A) YANGA Saa 11:00 Jioni kwa Kanuni za kuendesha ligi ya Vodacom Tanzania:

(B) SIMBA Saa 1:00 Usiku kwa Maelekezo ya Wakubwa Bodi ya Ligi Tanzania na TFF

(1) Hapa ni Nani alikosea na kwanini amekosea?

(2) Hapa ni Nani Yuko sahihi na kwanini Yuko sahihi?

(3) Je kwanini wote wapewe adhabu ya kurudia Mchezo je hakuna Kanuni ya kutuongoza mpaka tungojee Matamko ya Wana Siasa kweli je siyo kwenda kinyume na Shirikisho la Soka Duniani FIFA:

WADAU WA SOKA TANZANIA

Hapa daima kumbukeni kuwa wadau wa Soka Tanzania hawajaomba kabisa kurudishiwa garama zao kama Vile mnavyoonekana kujionyesha kama Kunakujali Sana hizo Garama

Mbona mnaongelea Garama Moja tu ya Kiingilio:

(1) Kiingilio cha uwanjani

(2) Watu walikodi Magari kutoka Mikoani

(3) Watu walikula Hotel na kulala Nyumba za wageni

Kama kweli mnania njema ongeleeni Garama zote

WADAU WA SOKA TANZANIA WANATAKA KUJUA YAFUATAYO

(1) Kulikuwa na Dharula gani Saa hizo?

(2) Hiyo Dharula ilipatikana Saa ngapi?

(3) Ni Nani alitoa Agizo la kusogeza mbele Mchezo huo?

(4) Alitoa kwa Nani na kwa njia ipi?

(5) Ni Nani alipokea Agizo Hilo na kusogeza mbele Mchezo huo?

(6) Alitumia Kanuni gani kusogeza mbele Mchezo huo?

(7) Anangoja Nini kujiuzuru kistaraabu kama Mwana Michezo?

(8) Wanangoja Nini na Nani kumpa Haki yake katika Timu iliyokidhi Vigezo vya kanuni ya kuendesha ligi ya Vodacom Tanzania?
 
Ukitumia akili kdogo tu utagundua kuwa ALIYEHARIBU mchezo ni SERIKALI ndio maana HAKUNA SABABU ZILIZOTOLEWA MPAKA SASA. Zaidi ya kusema WALIKUWA NA NIA NZUR KUSOGEZA MUDA WA MECHI MBELE. Kwa hio wewe kandamiza tu. WAPE UKWELI SERIKALI, USIWAOGOPE kama wafanyavyo hao WAANDISHI na WACHAMBUZI TAKATAKA
 
Back
Top Bottom