Watanzania milioni 60 tunaamka asubuhi kila siku tunakula chakula kinachopikwa kwa mkaa na kuni is a Terrible.Ni uharibifu mkubwa wa mazingira

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,730
2,082
Weekend ikiwa inaishia nawasalim.

Wakati mjadala wa bandari ukiendelea basi tusitingwe sana kiasi cha kusahau mambo mengine muhimu

Ukiona unakula umeshiba ujue kuna mti umedondoka uko porini na kufanya idadi kupungua na kufanya nafasi tupu kuonekana ambayo hatutegemei kama itazibwa na mti mwingine kwa kipindi kifupi.
Sàsa kwa siku inaporomoka miti mingapi ili watu wale.

It is so primitive and old stone age life mtanzania kuamka kila siku kukoka moto na kuni ili uweze kula.Ni upotevu wa muda mkubwa wa kazi za ujenzi wa taifa kwa dunia ya leo kuhangaika kila siku na mkaa na kuni na ni uharibifu mkubwa sana wa mazingira ambayo huko mbele tutakuja juta.

Hakuna mtu atakwepa hili balaa lltakalokuja kwa uharibifu wa mazingira hata uwe na pesa kiasi gani umejiwekea benk..hata uwe na cheo gani katika dunia hii ..balaa la hali ya hewa likianza litasambaratisha kila mtu hakuna kupona ni zaidi ya bomu la nyuklia.

Tutakosa mvua tutakosa maji baa la njaa mazao ukosefu wa mazao au chakula nk.. Tutakosa umeme gharama zitapanda viwanda vitayumba uchumi utayumba itakuwa vurugu tupu na mambo kuwa zig zag.

Hii hali ya hewa inayoyumba yumba leo ni matokeo ya uharibifu wa mazingira ya miaka kumi ishirini thelathini iliyopita ..leo ndio tunaona madhara yake.Kuna sehemu za mito na vijito sàsa hivi hazifiki maji tofauti na zamani ambapo ulizoea kuona maji yakititirika.Hali ya hewa ya sàsa haina mpangilio kabisa inaweza kuja mvua kubwa ya muda mfupi au jua kali la Muda mrefu likaunguza kila kitu halafu badae inakuja mvua robo ya nguvu nayo inaharibu kila kitu basi ilimradi ni shida tupu na anaeumia ni huyu binadamu.

Na mwaka huu pia kuna dalili ya kuwa na jua kali sana.

Ushauri ..Serikali ijaribu kutilia mkazo hili suala la kupata unafuaa au punguzo la kutosha kwenye matumizi mbadala wa nishati za kupikia hasa nishati ya gesi.Serikali Isifanye mchezo na suala hili tutakwisha.

Mfano kama Kodi ikipunguzwa au kuondolewa kabisa kwenye vyanzo vyote vinahusika na nishati ya gesi ya kupikia,,kwa mkoa wa Dar na moro tunaweza PATA gesi kujaza mtungi mdogo kwa 5000 tz sh.

Serikali haiwezi kushindwa kufidia hili punguzo lakodi kupitia vyanzo vingine vya mapato ni suala la kujipanga tu.
Ushauri mwingine mnaweza kuongezea ...alamsiki.
 
So sisi wafanya Biashara wa mkaa unataka tuishi vipi?
Swali zuri..fursa zitatokea zingine sema kwa sàsa umejikita sana huko..mlango mmoja ukifungwa mwingine unafunguka..halafu sio kama fursa hiyo ya mkaa itakatika ghafla..hapana itaenda taratibu wakati huo unajipanga kwa sababu sio kwa mara moja watu wote watatumia nishati nyingine.......Haya wengine wataongezea majibu hapo
 
Back
Top Bottom