Mbunge Cherehani: Tutumie Nishati ya Gesi Badala ya Kuni na Mkaa Ili Kulinda Mazingira

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,901
944

Mbunge Cherehani: Tutumie Nishati ya Gesi Badala ya Kuni na Mkaa Ili Kulinda Mazingira

Wananchi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kutumia nishati ya Gesi badala ya kutumia mkaa na kuni katika shughuli za mapishi ili kutunza na kulinda mazingira.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita katika tukio la kugawa mitungi ya Gesi kutoka kampuni ya 'ORYX 'kwa mama lishe lililofanyika katika kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi Manispaa ya Kahama.

Cherehani amesema ni vyema kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kampeni ya kumtua mama kuni kichwani ambapo ameipongeza kampuni hiyo kwa jitihada za kusaidia wajasiliamali hali itakayopunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Wakizungumza na Gold FM baadhi ya mama lishe waliopokea mitungi hiyo Veronika Emanuel,na Ireen Mtui wameishukuru Serikali kuimarisha ushirikiano na Kampuni ya Oryx kwani imerahisisha kufanya shughuli zao ambapo awali walikuwa wanapata shida kiafya kwasababu ya matumizi ya nishati ya kuni na mkaa.

Nae meneja wa kampuni hiyo Kanda ya ziwa Izaack Leon amesema lengo la kutoa mitungi hiyo ni kusaidia serikali katika kupambana na utunzanji wa mazingira kwakuwa gesi ni njia itakayo punguza ukataji wa miti inayotumika kwaajili ya kuni na mkaa na kwamba amekubali ombi la kupeleka huduma ya Gesikwa shule za msingi na Sekondari kwa kufuata muongozo wa serikali kadili itakavyo pendekeza.

Awali akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Orxy kupitia wakala mkuu Kagori Enterprise Wilayani Kahama Rehema Buluba amesema, licha ya kutoa mitungi 600 kwa wajasiliamali ambao ni mama lishe kwa halmashauri zote za wilaya ya Kahama, lakini amemuomba meneja wa Kanda kutoa msaada kwa taasisi za Serikali kama Magereza na kwa shule za msingi na Sekondari ili kuondoa changamoto ya matumizi ya Kuni na Mkaa.

Katika tukio hilo waliopata mitungi hiyo ni mamalishe 400 wa Manispaa, 100 wa Ushetu na 100 mama lishe wa Msalala ikiwa zoezi hilo limehudhuiwa na viongozi mbalimbali akiwemo, Sindano William Naibu meya Manispaa ya Kahama na Matrida Msomi Diwani wa Kata ya Ikinda Halmshauri ya Msalala.
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.10.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.10.jpeg
    50.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.11.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.11.jpeg
    39.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.11(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.11(1).jpeg
    46.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.12.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.12.jpeg
    45.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.12(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.12(1).jpeg
    45 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.12(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-03 at 00.32.12(2).jpeg
    45.9 KB · Views: 1

Mbunge Cherehani: Tutumie Nishati ya Gesi Badala ya Kuni na Mkaa Ili Kulinda Mazingira

Wananchi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wametakiwa kutumia nishati ya Gesi badala ya kutumia mkaa na kuni katika shughuli za mapishi ili kutunza na kulinda mazingira.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita katika tukio la kugawa mitungi ya Gesi kutoka kampuni ya 'ORYX 'kwa mama lishe lililofanyika katika kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi Manispaa ya Kahama.

Cherehani amesema ni vyema kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kampeni ya kumtua mama kuni kichwani ambapo ameipongeza kampuni hiyo kwa jitihada za kusaidia wajasiliamali hali itakayopunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Wakizungumza na Gold FM baadhi ya mama lishe waliopokea mitungi hiyo Veronika Emanuel,na Ireen Mtui wameishukuru Serikali kuimarisha ushirikiano na Kampuni ya Oryx kwani imerahisisha kufanya shughuli zao ambapo awali walikuwa wanapata shida kiafya kwasababu ya matumizi ya nishati ya kuni na mkaa.

Nae meneja wa kampuni hiyo Kanda ya ziwa Izaack Leon amesema lengo la kutoa mitungi hiyo ni kusaidia serikali katika kupambana na utunzanji wa mazingira kwakuwa gesi ni njia itakayo punguza ukataji wa miti inayotumika kwaajili ya kuni na mkaa na kwamba amekubali ombi la kupeleka huduma ya Gesikwa shule za msingi na Sekondari kwa kufuata muongozo wa serikali kadili itakavyo pendekeza.

Awali akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Orxy kupitia wakala mkuu Kagori Enterprise Wilayani Kahama Rehema Buluba amesema, licha ya kutoa mitungi 600 kwa wajasiliamali ambao ni mama lishe kwa halmashauri zote za wilaya ya Kahama, lakini amemuomba meneja wa Kanda kutoa msaada kwa taasisi za Serikali kama Magereza na kwa shule za msingi na Sekondari ili kuondoa changamoto ya matumizi ya Kuni na Mkaa.

Katika tukio hilo waliopata mitungi hiyo ni mamalishe 400 wa Manispaa, 100 wa Ushetu na 100 mama lishe wa Msalala ikiwa zoezi hilo limehudhuiwa na viongozi mbalimbali akiwemo, Sindano William Naibu meya Manispaa ya Kahama na Matrida Msomi Diwani wa Kata ya Ikinda Halmshauri ya Msalala.
Sawa hakuna shida
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom