Serikali msizuie mkaa, kuni mkitaka misitu ipone ni lazima bei ya gesi ishuke angalau kujaza iwe 10,000

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,732
2,082
Nawasalimu ..Tuchepuke kidogo na bandari halafu turudi.

Hakuna namna misitu itakwisha tu bila kuweka mbele kipau hiki cha nishati..madhara yake hatuwezi kuyaona leo na utakuta ikifika kiangazi ndio tunaanza kulialia na mvua tunaanza vikao na mikutano ya kujadili hali ya hewa..mvua zikianza tunaacha..

Ile kamati ya kujadili hili suala la nishati sijui imefikia wapi.

Tuache siasa kwenye mambo ya msingi jamani tutakwisha..Sàsa unazuia mtema kuni asikate kuni atapikia nini..unazuia asikate miti kuchoma mkaa umempa mbadala gani wa hiyo nishati yake ya asili.

Sitaki kuandika mengi suala linaeleweka formula inaeleweka wachumi wapo tusifanye siasa siku hizi hakuna kata mti panda mti
tusidanganyane sàsa hivi ni kata miti kwa kwenda mbele fagia misitu.

Bei ya angalau 10,000 kwa mtungi mdogo kujaza gesi wananchi walio wengi wanaweza kumudu angalau kupunguza tatizo na sio kumalizia kabisa wakati huo misitu inapona..

Tumeanza kiangazi ikifika mwezi wa kumi balaa linaanza mara tanesco mgao mara dawasco nao wanafanya yao sijui nani wengine..hasa jiji la Dar ndio shida sana.Majenereta mtaani kelele tupu utafikiri tupo kiwandani.Sasa hivi tumesahau hizi shida.

Dunia ya leo kuwashiwa umeme kwa kupangiwa ni aibu sana..

Nawakumbusha tu mwezi wa kumi sio mbali.Tujipange mapema kabla ya kuanza kulialia.
 
Gas asilia ili iwe efficient na cheaper lazima iwe piped na miundombinu yetu na kukweka infrastructure huko sidhani kama ni investment ambayo tunataka kufanya....

Unaposema kujaza iwe 10k unajua kwamba hio LPG tunaagiza na huku inajazwa (sasa unajua faida ya muagizaji; anayejaza anayasafirisha na mwisho wa siku vendor wa mwisho kabisa makato na faida yao ni ngapi )? Sababu kabla haujasema bei iwe kiasi fulani lazima ujue cost ni kiasi gani (Unless unasema iwekwe ruzuku hence mlipa kodi alipie difference...

Binafsi suala hili kwa muda mrefu njia ni moja tu..., Ongeza Production ya Umeme (Solar, Gas na Vyanzo vyote pamoja na Bwawa) unganisha kwenye Grid...

Tayari tuna infrastructure ya umeme mpaka kwenye kila nyumba; Shusha bei ya umeme ni the minimum watu waache kutumia oven zao kama makabati na kuanza kupikia (efficiency ya umeme ya sasa katika kupika na induction cooking is top notch same or even better than gas); And how can Tanesco Manage that; You might ask...., By waking the Sleeping Giant... is the only answer

Gas asilia ili iwe efficient na cheaper lazima iwe piped na miundombinu yetu na kukweka infrastructure huko sidhani kama ni investment ambayo tunataka kufanya....
Bei ya kuweka umeme inachezewa sana.Kwa sàsa ndio imemuelemea kabisa mwananchi hafurukuti..na kuhusu uhakika wa upatikanaji massa 24 sijui huko ulipo mtakuwa mashahidi.
 
Bei ya kuweka umeme inachezewa sana.Kwa sàsa ndio imemuelemea kabisa mwananchi hafurukuti..
na kuhusu uhakika wa upatikanaji massa 24 sijui huko ulipo mtakuwa mashahidi.
Kama nilivyosema hapo juu; kutegemea LPG ambayo ni mafuta na hatutengezi tunaagiza lazima kutakuwa kuna Kiwango fulani ambacho bei haiwezi kupungua chini ya hicho kiwango....

Kutumia Energy Mix ambayo itakusanywa na Tanesco na kusambazwa kwa kila muhusika kutumia Network ya Tanesco ndio the only practical way... Tungeweza kwenda Piped (yaani gesi kwenye mabomba ) ila kumwaga huo mtandao na uzembe wetu huenda leakage ikawa kubwa (na tunavyouza nchi sina uhakika hio gesi ni yetu kwa kiwango gani)

Kwahio umeme ukishuka (na kwanini usishuke kama uzalizashaji utaongezeka maradufu) kwanini watu wasitumie majiko ya UMEME.....; Je ni rahisi kwa kutumia Nishati tunayoagiza kutoka nje au ambayo tunazalisha naturally nchini ?
 
Idea nzuri kazi ipo huko sàsa na ngoja tuone bwawa la nyerere litakuwa na effect gani au litaleta mabadiliko gani then hiyo idea yako inaweza ikaonekana dhahiri.
 
Idea nzuri kazi ipo huko sàsa na ngoja tuone bwawa la nyerere litakuwa na effect gani au litaleta mabadiliko gani then hiyo idea yako inaweza ikaonekana dhahiri.
Bwawa la Nyerere litakuwa halina effect sababu huenda wakauza kila kitu kwa watendaji au nafuu katika uzalishaji ikaenda katika GAWIO la Serikali na Matumbo ya Watu..., Issue sio kwenye kuwezekana au kutokuwezekana Issue ni Ulafi na Tamaa ya watu wachache wenye Myopic Thinking..... (Sadly watu hao ndio Policy Makers)
 
Hilo ni tatizo letu na ndio tutaendelea na hizi hadithi zetu za kila kunapotokea tatizo ndio tunatafuta solution ya muda mfupi then tunasahau kesho tatizo linarudi tunazunguka hapo hapo kila mwaka.Tatizo la afrika maendeleo yanajikokota sana tofauti na muda tulionao inachukua muda mrefu sana kutoka hatua moja kwenda nyingine.Binadamu utajilimbikizia mali utakufa utaziacha wanafaidi wengine.
 
Back
Top Bottom