Watanzania ambao hawapendi kusoma hawahitaji shahada (Miaka 3) kujua katiba

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Raisi Samia sasa ameanza kuwa myeyushaji na mpotoshaji na hili ni la kusikitisha sana. Watanzania wamekuwa na hii katiba zaidi ya miaka 30 lakini ni zaidi ya miaka 10 sasa tunaongelea katiba mpya. Bunge la katiba liliundwa, maoni ya katiba mpya yalikusanywa kwa gharama kubwa na leo unataka kutupotezea muda na pesa nyingi kwa mradi mwingine usio na tija wa kuelimisha kwa miaka mitatu katiba ambayo ndiyo inaenda kubadilishwa. Sababu kubwa ni kunufaisha wachache tu na wewe binafsi badala ya kufikiria ni jinsi gani utaipeleka Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa.

Lakini cha ajabu kwenye mkutano wako umejaribu kutuelezea EA kwamba nchi zina demokrasia tofauti! hii ni kupotosha nchi pekee yenye demokrasia ni Kenya. Uganda na Rwanda sio demokrasia kabisa! na kitendo cha kusema nchi hizi ni za kidemokrasia ni kujaribu kujifurahisha na kuhalalisha kwamba sisi demokrasia yetu ni hii ya kuiba kura na kuwa na mikutano kila siku isiyo na tija. Hii serikali inasikitisha sasa inaaanza kuwa serikali ya uongo.

Inawezakana vipi unasema mkatiba ni ya wote lakini serikali ndiyo inataka pekee kutoa maelekezo ya mchakato wa katiba! Kwa hili umesikitisha sana na usikokuwa makini utakuwa umepoteza muda na utasaulika mapema sana kwenye historia yako. Kuna sera za uchumi unafanya vizuri lakini kama katiba bora itakushinda legacy yako itakuwa mbaya kuliko ya Kikwete.

Fanya katiba bila kujali chama bali unatakiwa kujali nchi. Watanzania ambao huu mtaba tu wa DP world hawajaweza kuusoma wataweza vipi kusoma katiba na kuielewa?

Hizi umuhimu wa kujua katiba ni wakati wa kutaka kubadilisha au wakati inatumika? Kwanini hakukuwa na education miaka yote
 
Hakuna Mtawala wa CCM atakayeridhia Katiba Mpya, kitendo cha kuridhia Katiba Mpya ina maanisha wameridhia kuondoka Madarakani.

Na kwa hali ilivyo sioni CCM ikiridhia kuondoka madarakani iwe leo ama kesho.

Njia ya kupatikana Katiba mpya ni Wananchi wenyewe kuipigania, vinginevyo haitokaa ipatikane abadani
 
EA countries zote zinademocracy sema zinatofautinia kimazingira hili uelewe.

Kuhusu swala la kuelimisha watu hii katiba ambayo watu tunataka ibadirike HAPA SAMIA KACHEMKA NAUNGA MKONO HOJA
 
EA countries zote zinademocracy sema zinatofautinia kimazingira hili uelewe.

Kuhusu swala la kuelimisha watu hii katiba ambayo watu tunataka ibadirike HAPA SAMIA KACHEMKA NAUNGA MKONO HOJA

Demokrasia gani !! Yaani Yoweri Museveni katawala kuanzia 1984 halafu anamuandaa mtoto wake mwanajeshi achukuwa nafasi yake hiyo ndiyo demokrasia? labda tunahitaji elimu ya demokrasia kwanza kabla ya kupoteza muda kwenye katiba ambayo hakuna mtu zaidi ya wanasheria watailewa
 
Absolutely true

Back
Top Bottom