Waziri Dkt. Ndumbaro - Zaidi ya Asilimia 50 ya Watanzania Hawaifahamu Katiba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

WAZIRI DKT. DAMAS NDUMBARO - ZAIDI YA ASILIMIA 50 YA WATANZANIA HAWAIFAHAMU KATIBA, ELIMU YA KATIBA KUTOLEWA KWA MIAKA MITATU

"Kuna tafiti kadhaa zimefanyika na kubaini zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania hawaifahamu katiba na wengine wanasema hata hawajawahi kuiona hiyo katiba, hatari yake ni kwamba kwa kuwa hawaifahamu watachukulia yale ambayo wanaambiwa na ambayo siyo ya kweli kuhusiana na katiba na wataamini." - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria

"Mwaka jana bei za vyakula zilipanda sana, msomi mmoja ambaye anaelewa mambo, wakati akiongea na vyombo vya habari alisema bei za vyakula zimepanda tatizo ni katiba, hivyo wanataka katiba mpya ili bei za vyakula zishuke, sisi wenye uelewa tunaweza tusikubaliane na hilo lakini wapo Watanzania wataamini ugumu wa maisha na bei za bidhaa kupanda inatokana na katiba, mtu kama huyo atataka katiba mpya akiamini kwamba katiba mpya itashusha bei za bidhaa" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria

"Ni jukumu letu Wizara ya Katiba na Sheria kutoa elimu juu ya katiba ili Watanzania wajue katiba ni nini? majukumu yake ni nini na ina umuhimu wake katika jamii" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria

"Yako mambo ambayo watu wanayaongea na kudai kwa minajili ya katiba lakini kumbe ni mambo ambayo yanapaswa kuelezewa kwenye sheria mbalimbali, ndio maana mkakati huu (wa kutoa elimu ya katiba) tumeupa msukumo mahususi na tutakwenda nao kwa miaka mitatu na kuhakikisha kwamba Watanzania wote wanaijua katiba" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria
 

Attachments

  • F4oJSknW4AIzC0E.jpg
    F4oJSknW4AIzC0E.jpg
    22.9 KB · Views: 7

Similar Discussions

Back
Top Bottom