Ninapendekeza yafuatayo ili kuwezesha Wananchi wengi kuijua katiba yao

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,300
Ninaandika huu uzi bila kuweka itikadi yangu ya kisiasa huku nikiwa na huzuni. Siku chache tumetaarifiwa kupitia wizara ya katiba na sheria kuwa 51% ya watanzania hawajui chochote kuhusu katiba ya sasa. Kwa hesabu za haraka ni kuwa karibu kila familia nusu ya wanafamilia hawajui katiba ya JMT. Ni huzuni.

Hii inamaanisha kwamba kuna watanzania wengi hawajui wajibu wala haki zao kama raia wa Tanzania. Na hata wengi wanaopiga kelele kwamba wanataka katiba mpya hawajui nini kitolewe kwenye katiba iliyopo na kitu gani kipya kiwekwe. Pia wale wanaoonekana kuijua katiba huwa wanajua machache yenye maslahi nao.

Kwa mfano Chama Cha Mbowe huwa wanajua katiba imetoa haki ya kuandamana na uhuru wa kutoa maoni. Mambo mengine hawajui. Madhara ya wananchi wengi kutoijua katiba yao hata kidogo ni makubwa zaidi. Hii inasababisha raia kutowajibika kwa nchi yao na pia baadhi ya wajanja wachache kuminya haki za wajinga wengi wa katiba.

Ninaipongeza wizara kwa kutamka kuwa itatoa mafunzo ya miaka mitatu kuhakikisha wananchi wengi wanaijua katiba yao kwanza kabla ya kutengeneza katiba mpya. Binafsi ninapendekeza yafuatayo ili kuchochea wengi zaidi kujua;

1. Ninashauri serikali kupitia wizara ya elimu ipeleke somo maalum la katiba kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.

2. Vyama vya siasa navyo viwahamasishe wanachama wao kununua vitabu vya katiba ili wajisomee kiundani.

3. Viongozi wa dini nao wahamasishe waumini wao kuijua katiba ya nchi yao.

4. Kila familia ihakikishe kila mwanafamilia ana kitabu cha katiba na kukisoma.

5. Wapenzi waanze kupeana zawadi za vitabu vya katiba. Kwenye birthday parties mpeane vitabu vya katiba. Kila slay queen akiwa na kitabu cha katiba tutakuwa tumegusa kundi kubwa. Ifikie sehemu mtu ukiona msg inayosema "baby nikuambie kitu?" uhisi baby anataka kuuliza kitu kuhusu katiba na sio hela.

6. Kila mwananchi aguswe kuhamasisha walio karibu nae kujisomea kitabu cha katiba....
 
Ninaipongeza wizara kwa kutamka kuwa itatoa mafunzi ya miaka mitatu
Hakuna mbogamboga wa kupinga hili hata kama halina mantiki! Mzee WARIOBA ni mzalendo alietukuka ingawa ni mwanaccm yeye huona ambayo hayafai na husema wazi!! Ila hawa sasa wazee wa bahasha 🤣🤣🤣🤣wao ni kushangilia na kupiga meza makofi kisawaswa!!
 
Ser
Ninaandika huu uzi bila kuweka itikadi yangu ya kisiasa huku nikiwa na huzuni. Siku chache tumetaarifiwa kupitia wizara ya katiba na sheria kuwa 51% ya watanzania hawajui chochote kuhusu katiba ya sasa. Kwa hesabu za haraka ni kuwa karibu kila familia nusu ya wanafamilia hawajui katiba ya JMT. Ni huzuni.

Hii inamaanisha kwamba kuna watanzania wengi hawajui wajibu wala haki zao kama raia wa Tanzania. Na hata wengi wanaopiga kelele kwamba wanataka katiba mpya hawajui nini kitolewe kwenye katiba iliyopo na kitu gani kipya kiwekwe. Pia wale wanaoonekana kuijua katiba huwa wanajua machache yenye maslahi nao.

Kwa mfano Chama Cha Mbowe huwa wanajua katiba imetoa haki ya kuandamana na uhuru wa kutoa maoni. Mambo mengine hawajui. Madhara ya wananchi wengi kutoijua katiba yao hata kidogo ni makubwa zaidi. Hii inasababisha raia kutowajibika kwa nchi yao na pia baadhi ya wajanja wachache kuminya haki za wajinga wengi wa katiba.

Ninaipongeza wizara kwa kutamka kuwa itatoa mafunzi ya miaka mitatu kuhakikisha wananchi wengi wanaijua katiba yao kwanza kabla ya kutengeneza katiba mpya. Binafsi ninapendekeza yafuatayo ili kuchochea wengi zaidi kujua;

1. Ninashauri serikali kupitia wizara ya elimu ipeleke somo maalum la katiba kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.

2. Vyama vya siasa navyo viwahamasishe wanachama wao kununua vitabu vya katiba ili wajisomee kiundani.

3. Viongozi wa dini nao wahamasishe waumini wao kuijua katiba ya nchi yao.

4. Kila familia ihakikishe kila mwanafamilia ana kitabu cha katiba na kukisoma.

5. Wapenzi waanze kupeana zawadi za vitabu vya katiba. Kwenye birthday parties mpeane vitabu vya katiba. Kila slay queen akiwa na kitabu cha katiba tutakuwa tumegusa kundi kubwa. Ifikie sehemu mtu ukiona msg inayosema "baby nikuambie kitu?" uhisi baby anataka kuuliza kitu kuhusu katiba na sio hela.

6. Kila mwananchi aguswe kuhamasisha walio karibu nae kujisomea kitabu cha katiba....
Serikali ya CCM haikuwa na haipo tayari kutoa elimu ya katiba Ili wananchi waijue. Wamefanya hivyo siku zote Ili wananchi wasitambue haki zao kikatiba na kuiwajibisha serikali. CCM wanajua siku wananchi wakiwa na uelewa mkubwa kuhusu katiba,mambo yao mengi yataharibika.
 
Back
Top Bottom