Watanzania 27 wanamiliki mabilioni Uswisi

Hivi ina maana haiwezekani kabisa kumkokota mkulu mbele ya haki jamani!? ama kweli tunahitaji katiba mpya haraka sana ili tuwachape bakora hawa majambazi.
 
mwanzisha uzi inaonekana anapenda sana udaku?? Kwanin usitaje majina??? Au swala lipo mahakaman haliluhusiwi kujadiliwa??
 
Kiingozi wa juu serikalin? Kwa uelewa wangu rais ndio kiongozi wa juu serikalin
 
mwanzisha uzi inaonekana anapenda sana udaku?? Kwanin usitaje majina??? Au swala lipo mahakaman haliluhusiwi kujadiliwa??

mwanzisha thread kaitoa habari mwananchi, huyo mwandishi wa mwananchi ilipaswa ataje majina.
 
I cant believe, tunaomba serikali ithibitishe hili, nimemkumbuka Nyerere alisamee pension yake kwa kuwa nchi ni maskini, kumbe kuna nyang'au walikuwa wanasubiria aondoke waanze kuamisha hizi fedha. Mimi nawaomba wananchi tuamke nakulipigania hili. Hata kama serikali itakataa kuwataja na kuwachukulia hatua kali ikiwemo kufilisiwa, sisi tukutane jangwani kuelekea ikulu kumshinikiza rais arudishe hizo fedha au ajiuZulu. Currently we are talking inflation which is 20%+ shame on CCM

Serikali ipi ithibitishe?

Wakuu tuanze kwa kutaja majina ya wanaoshakiwa; na baadaye tuyapigie kura.
Kiongozi wa juu serikalini, no doubt
1. JK wa sasa, then
2.
3.
 
Wanabodi,

Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanya biashara, imebainika kuwa ndio wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni) mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni). Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ambao wanamiliki Dola 500,000 kwa kila mmoja.

Miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.

SOURCE: MWANANCHI AGOSTI 18 2012

Hao mafisadi watkwisha lini kila siku wanaiba tu
 
Hii nchi kweli shamba la bibi mpaka wakati wa Nyerere napo watu wamefanya ufisadi, tatizo muandishi kaficha majina.

Mkuu umesahau vita ya uhujumu uchumi? Hata hivyo mwandishi hakusema kuwa mawaziri hao waliiba na kuficha hizo noti wakati huo. Soma vizuri.
 
Wanabodi,

Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanya biashara, imebainika kuwa ndio wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni) mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni). Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ambao wanamiliki Dola 500,000 kwa kila mmoja.

Miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.

SOURCE: MWANANCHI AGOSTI 18 2012

Tuna Jeshi la Polisi,TAKUKURU,USALAMA wa TAIFA na vyombe vingine vingi vya Usalama lakini haya madudu yanatendeka nchini kwetu!?
 
kama watu wanajua mpaka na kiasi cha fedha kilichofichwa na wahusika , inakuwaje wanashindwa kutaja majina? Au kile kile kitendo cha serikali kulifungia mwanahalisi kimeweza kufanikisha nia ya serikali ya kuwatia woga wamiliki wa vyombo vya habari?

Hoja hii imeungwa mkono mkuu.
 
Kumbe Chenge aliposema za kwake alizonazo ni vijisenti tu alikuwa anajua kwamba wapo walioficha nyingi zaidi ya za kwake!!!! It is matter of time watawekwa hadharani tu kama sio leo au kesho basi itakuwa keshokutwa!!!!

Tiba
 
Tukumbuke hata moto huaza kwa ujiti wa kiberiti lakin .....

Muda ukiwadiwa wafuatao hawatasalimika japo ni lini sifaham vema

1. Benjamin mkapa.
Ameuza mali zetu ovyo na zingine akajimilikisha

2. Jakaya m kikwete.

Anakashifa nyingi za kifisadi ikiwemo richmond
-Ametuchochea na kutugawa kwa din, ameiweka rehan aman yetu nk.

3. Chenge na wenzake-rada

4. Mawaziri baadhi, hususan waliopitia wizara za madin, viwanda na biashara pia maliasili na utalii

Hakika hatatoka mtu labda aanze mapema kwa mnyaazimungu othewise ya gadhaf na chiluba yatawapata.
 
Ni bahati nzuri sana mleta thread hajui kwamba thread hii inazidi kukiangamiza chama chake!

TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),

tumbiri@jamiiforums.com

Tatizo lako wewe ni Chadema Addicted kila sehemu unaleta ushabiki wa vyama unadhani watanzania wote ni wafuasi wa vyama vya siasa hapa tunaongelea maslahi ya Taifa.
 
Watajeni jamani....mmepataje idadi ya watu kuwa na list ya watu?......huu ni ubabaishaji kabisa. Tuwataje kila mtu na kiasi anachomiliki km tulivyojua mzee wa vijisenti alikuwa anamiliki kabilioni kamoja tu
 
Back
Top Bottom