Watanganyika wanaoitetea DP World wana matatizo ya akili?

Watanganyika wanaoitetea DP World wana matatizo ya akili?

Serikali haipaswi kuacha mipango ya kuleta mwekezaji bandarini , suala la mapungufu ya mkataba yaangaliwe.

Hoja kwamba nchi yenye watu milion 60 kushindwa kuendesha Bandari NI hoja mufilisi kabisa na ni hoja ya mtu asiye na uelewa kuhusu Bandari.

Bandari si stand ya Magufuli au Nyegezi kwamba inahudumia Zaid mabasi ya mkoani.

Bandari inaangaliwa kuhudumia Dunia au mataifa kadhaa.

Nani au kampuni gani ya Kitanzania utaipa iendeshe Bandari Kwa ufanisi wa kushindana kidunia?

Hakuna Mtanzania au kampuni yoyote ina msuli wa kuweza kuisimamia Bandari ikaweza kuleta ushindani Duniani.

Hatuna Mtanzania yeyote anayeweza kuingia top 1000 ya matajiri Duniani ,, iweje tuwe na kampuni yenye uwezo huo?
Sidhani kama kuna Mtanganyika yeyote aliyeukataa uwekezaji! Kinachopigiwa kelele ni mapungufu yaliyopo kwenye huo mkataba. Kama mapungufu yatarekebishwa, mwekezaji anakaribishwa kwa mikono miwili. Kinyume na hapo, bora tubaki na bandari yetu.
 
Haya yote hawayaoni.. Inafika mahali unajiuliza je wana matatizo ya akili?[emoji419][emoji375]
 
Unamkuta mtu mmoja ana kichwa kikubwa kabisa, anasema DPW wapewe bandari kwakuwa bandari imekuwa ikiendeshwa bila ufanisi.

Mtu mjinga kama huyo ameshindwa kabisa kufikiri na kuona aibu kwamba nchi yenye watu zaidi ya million 60 inakosa watu wa kusimamia bandari ifanye kazi kwa ufanisi na anashangilia ibinafsishe kwa Nchi ya ugenini.

Nchi hii ina watu wajinga sana, pengine kwa ujinga Duniani sisi tunashika nafasi ya kwanza, pili na ya tatu.
kabisa mkuu , mm nmeishi afrika mashariki ila sisi tuna ujinga mwing sana
 
Sidhani kama kuna Mtanganyika yeyote aliyeukataa uwekezaji! Kinachopigiwa kelele ni mapungufu yaliyopo kwenye huo mkataba. Kama mapungufu yatarekebishwa, mwekezaji anakaribishwa kwa mikono miwili. Kinyume na hapo, bora tubaki na bandari yetu.
Kuna wanaosema taifa lenye watu milion 60 linakosaje watu wa kuendesha Bandari?

Hatuna kampuni au shirika lolote lenye uwezo wa kushindana kidunia.

Bandari inahitaj Vifaa vya kisasa vya matrilion kitu ambacho hatuna Tahir mwenye uwezo huo wala serikali haina msuli huo.
 
Wewe katazame mwaka huu uliopita imeendeshwa na TPA imeleta gawio la billion 200 tu. Hata Kiwanda cha cement tena kwa ubia wa hisa kidogo tu za serikali imewapiku gawio lake.

Wakati bandari inatakiwa ichangie japo nusu ya bajeti ya Tanzania.

Hatuwezi wenyewe, bado sana muda wetu.
Mimi hili la kusema hatuwezi wenyewe ndio napingana. Mnaona hatuwezi wenyewe kwasababu ya uzembe na ubadhilifu. Uzembe wa kutochukua hatua na usimamizi mbovu. Usimamizi mbovu ni matokeo ya kupeana nafasi za kiutendaji kwa kujuana juana.

Tukianza kuwapa watu nafasi za kiutendaji kwa kuangalia sifa stahiki na tukachukua hatua kali pale unapotokea ubadhilifu, hakuna sehemu itakosa ufanisi.
 
Uwezo kifedha Mzee.

Hatuna msuli wa kushindana kidunia, hatuna msuli wa kuafford teknolojia ya kisasa bandarini

Bakhressa mwenyewe Camera Tu za Viwanjan zinamshinda ndio nan tumpe Bandari?
 
Ndo shida yenu. Mnahamasisha demokrasia alafu hamjui hata maana ya demokrasia. Mnahamasisha haki za kikatiba alafu hamjui hata maana yake. Nyie mnataka kila mtu awaze kama nyie alafu ndo mnajifanya wanademokrasia.

Kwa kifupi nyie ni wapuuzi tu! Tunaounga mkono mkataba wa Tz na Dubai tuna hoja na kama nyie mnadhani mna hoja endeleeni na hoja zenu.
kuna vitu haviitaj akili kubwa , unaunga mkono kitu hujui ukomo wake , hujui maslai yetu , umeoneshwa mpk conditions za mwekezaj bado unasema unaunga mkono , kama sio mwehu tukuiteje? hata waarab tukigeuza huu mkataba wao watupe bandari ya kwa mkataba huu sio waarab tu dunian kote hawataukubali km Yemen , Djibout na Somalia , ila bongo ndo tunawakuta wajinga kama nyiny mnadai mna hoja [emoji23][emoji23][emoji23] ebu lete hoja zenu
 
Yes! Here iam.

Mwanasheria makini mwenye hoja makini ambaye hadi sasa hakuna ufipa aliyeweza kunijibu hoja zangu juu ya mkataba huu.

Nasema tena naunga mkono mkataba huu wa ushirikiano baina ya Tz na Dubai kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Bandarini.
andika hoja zako ambazo hazijajibiwa [emoji23][emoji23][emoji23] hii bongo wehu ni weng sana
 
Mimi hili la kusema hatuwezi wenyewe ndio napingana. Mnaona hatuwezi wenyewe kwasababu ya uzembe na ubadhilifu. Uzembe wa kutochukua hatua na usimamizi mbovu. Usimamizi mbovu ni matokeo ya kupeana nafasi za kiutendaji kwa kujuana juana.

Tukianza kuwapa watu nafasi za kiutendaji kwa kuangalia sifa stahiki na tukachukua hatua kali pale unapotokea ubadhilifu, hakuna sehemu itakosa ufanisi.
Umenikumbusha jambo fulani!

Wakati fulani mkubwa fulani alimteua kada fulani wa Chama fulani kuwa Katibu tawala wa Mkoa fulani. Lakini muda mfupi baada ya uteuzi wake, huyo mkubwa aliubatilisha tena uteuzi wake. Tetesi zilizotoka ni kuwa aliyenusurika kuwa Katibu tawala alikuwa ni kada tu, lakini hakuwa ameshule kisawasawa. Kiwango cha kisomo chake kilikuwa kidato cha Nne.
 
kuna vitu haviitaj akili kubwa , unaunga mkono kitu hujui ukomo wake , hujui maslai yetu , umeoneshwa mpk conditions za mwekezaj bado unasema unaunga mkono , kama sio mwehu tukuiteje? hata waarab tukigeuza huu mkataba wao watupe bandari ya kwa mkataba huu sio waarab tu dunian kote hawataukubali km Yemen , Djibout na Somalia , ila bongo ndo tunawakuta wajinga kama nyiny mnadai mna hoja [emoji23][emoji23][emoji23] ebu lete hoja zenu
Ndo mana nakwambia wewe ni mjinga kama sio mpumbavu

Ukomo umesemwa utawekwa kwenye mikataba mahsusi ya uwekezaji wewe shida yako nini?

Mkataba huu ibara ya 1 sehemu ya pili imesema kutakuwa na mikataba mahsusi ya uwekezaji itakayoweka haki na wajibu wa kila upande alafu unadai mkataba hauelezi tutapata nini??

Polee sana
 
Kweli kabisa
Mwaka 2000 nikiwa Malaysia kwenye kongamano la dini ya Buddha pale Malaysia university nilikutana na mhindi mmoja tajiri aliyewahi kuishi na kutajirikia bongo.

Kwa utani unaouma na kuakisi ukweli akasema usipotajirika Tanzania ni ngumu kutajirika pengine Niliumia sana naye aliyaona maumivu yangu lakini huo ndio ulikuwa ukweli

Mkataba mbovu wa bandari zetu zote na kampuni kubwa ya DPW umeshapigiwa kelele na kila kaliba ndani ya taifa hili lakini bado kuna mazuzu wajinga wachache wanaona unafaa

Kati ya hao kuna wale walioko mamlakani ambao wamepata chochote ili kuutetea.. Hawa kwangu ni wahaini na wasaliti wakubwa na hukumu yao kuna siku itafika

Ninaowahurumia ni hawa wafuata mkumbo kwasababu za kiimani, itikati za kisiasa jinsia na wote wenye fikra finyu kwamba nwafrika hawezi kitu bila msaada wa ngozi nyeupe ama manjano..

Kinachopiganiwa ni kwa maslahi ya watoto, vijukuu, vitukuu na vining'ina vya taifa hili la Tanganyika.. Bila kujali
Imani zao
Rangi zao
Itikadi zao nk

Haya yote hawayaoni.. Inafika mahali unajiuliza je wana matatizo ya akili?
 
Back
Top Bottom