Zawadini
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 3,048
- 2,267
Unaelekea huujui hata huu muungano kiasi kwamba unazungumza lugha za ajabu, na iwapo unaujua huu muungano basi unazungumza lugha za chuki.Kwahiyo Mzanzibari anaweza kuwa Rais zanzibari na Tanganyika pia? Ila Mtanganyika hawezi kuwa Rais wala Raia wa Zanzibari sio? Kwahiyo sasahivi taifa lenye watu million hata tatu hawafiki wamepata Rais kwao na kwenu Tanganyika alafu ninyi watu zaidi ya Milion 65 mmeshindwa hata kupata Rais kwenu?
Mmeona kinachoendelea sasa? Mnaongozwa na Rais mgeni ambae hapa sio kwao? Mnaona anachowafanya? You do too much singing. It is a time to stop singing and start swinging, badilisha namna ya kufikiri. Muungano ulikuwa na maana kipindi kile cha mawindo sio sasa hivi! Matokeo yake ndio haya mpo kwenu ila mnaishi kama wakimbizi!
Hivi ni sawa kwa Mtanganyika kuitawala Zanibar - akina Mwinyi mkubwa na Mwinyi mdogo na Jumbe? Ila si sawa kwa Mtanzani aliyetoka Zanzibar kutawala Tanzania?
Hivi ni sawa kwa Mtanzania aliyeyoka Tanganyika kuitawala Tanzania ila si sawa kwa yule aliyetoka Zanzibar? Hivi mtu akisema ama wewe ni mbaguzi au mwenye kujenga chuki, usiyejua unalolifanya anakosea?
Sasa basi, ni wakati wa nyinyi kufanya maamuzi ya huu muungano kwani sisi tulipojaribu tuliadhibiwa vikali, tena na Watanganyika kwa kutishwa na vivuli vyao. Binafsi huu muungano siutaki. Naomba saidieni katika hili tutulie; vinginevyo tuna haki ya kuwa viongozi katika JMT na hakuna wa kuiondoa haki hiyo katika muundo wa sasa hadi pale mutakapojitambua na kufanya maamuzi ya busara. Idumu JMT; idumu SMZ.
Mkuu sisi tupo na tutaendelea kuwepo. Wewe endelea kulilia kwenye keyboard.