Muungano: Saa ya ukombozi imewadia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano: Saa ya ukombozi imewadia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHIBUU, May 24, 2012.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,183
  Likes Received: 700
  Trophy Points: 280
  Kwanza tuanze kwa kusema wazi wazi kwamba HAKUNA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR, badala yake kilichopo ni TAANGANYIKA KUITAWALA ZANZIBAR. Najua kwamba nikisema hivyo nazitonesha nyoyo za watawala wetu, yaani wa Tanganyika na Vibaraka wao waliopo zanzibar. Nasema hivyo kwa sababu utawala wa Tanganyika kwa Zanzibar ulikua tofauti na ule wa wakoloni weupe pamoja na kua utawala wa Tanganyika ulikuja baada ya uvamizi unaoitwa MAPINDUZI uliofanywa 1964 ukiongozwa na Julius Kambarage Nyerere kwa kutumia jeshi la kukodi lililoongozwa na John Okelo (Mkenya) alieishia Uganda. Uvamizi huo ulifanyika mara baada ya uhuru wa Zanzibar uliopatikana mwaka 1963. Sioni sababu ya kueleza hapa vipi mapinduzi (Uvamizi) yalifanyika lakini ningeshauri vizazi vya leo visome kitabu cha Marehemu Abrahmani Babu (Komred) kiitwacho MAPINDUZI AU UVAMIZI, kinajieleza vya kutosha.

  Kwa kua uvamizi na ukoloni huu wa Tanganyika ulikuja kwa mbinu za kuwadanganya wazanzibari eti wanawakomboa kwenye utawala wa kisultani kumbe wanawaingiza katika utwala wa mabavu wa wakoloni Weusi wa akina Nyerere na wenziwe. Kwa mbinu na unafiki wake Nyerere alimpa kilemba cha ukoka mzee wetu Abeid Amani Karume kua rais wa miezi 4 tu na Baadae akamgeuza Gavana bila mwenyewe kujua wala wazanzibari, ingawa wasomi wetu walilijua hilo na ndio maana yakawakuta yalio wakuta. Nyerere kwa ujahili na ukatili wake mkubwa na mipango yake ya udikteta aliamua kuwauwa wasomi wote wa Kizanzibari hasa wale aliodhani wanapingana na utawala wake wa mabavu hapa nnaona niwataje wachache miongoni mwa wengi nao ni; (1) Kassim Hanga (2) Othmani Shariff, (3) Wilium Chacha. (4) Mdungi Ussi (Mwana wa Kitumbatu kindaki ndaki) n.k.

  Aidha alithubutu kuwaweka LUPANGO (Mahabusu) Viongozi kadhaa wa kizanzibari na hata Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar WOLFGANG DOURADO. Dourado aliwahi kuwekwa ndani kwa ajili tu ya kupingana na Udhalimu wa Nyerere. Nyerere pia lithubutu kuanzisha Jela Maalumu ya Mateso kwa wazanzibari, jela ambayo ikijulikana kama KWAMANDELA. Hapo kilimani ndani ya Jela iliopo sasa kuna sehemu inaitwa kofia Jekundu, na sehemu ya kunyongea, vyote hivyo vilikua kwaajili ya kuwatesea wazanzibari wenye mtizamo tofauti na ule wa nyerere. Alianzisha ofisi maalum ya Mateso hii ikijuilikana kwajina la kwa Bamkwe ofisi hii ilikua hapo kwa Muumiani, ambapo leo panajuilikana ama kwa Marwa au kwa DPP karibu na Ofisi ya Uhamiaji Mahala hapo palifanywa unyama mkubwa kwa wazanzibari wenyemuelekeo tu wakupingana na Nyerere na Vibaraka wake alio wapandikiza hapa Zanziba kwa maslahi ya utawala wake Ilifikia pahala Wa Zanzibari kubanwa mbegu za uume kwa pakari na mateso mengine ambayo nnaona kashfa kuyataja katika makala haya Katika misemo ya Nyerere aliwahi kusema Mtu akizowea kula nyama ya Mtu hawezi kuiwacha na ndio vivyohivyo Mtu akizoea kuuwa hawezi kuacha na ndiyo alivyokua nyerere,Kwakua alizoea kuuwa hatimae iligeuka usemi wa Kiswahili Tumbiri akiisha miti huingia mwilini,Tarehe 7/4/1972 Tumbiri kweli aliisha miti akaja mwilini na ndipo Nyerere alipomuuwa karume. Haikua nia yangu kusema chochote katika kipindi cha mchakato wa Katiba mpya, lakini nilitaka kufanya hivyo kwa kuamini kwamba viongozi wetu hasa ndani ya CCM wanajua kila kitu na nikaamini kwamba huu ndio muda wao muafaka wawao ama kufuta dhambi zao au za wazee wao kwa kuikombowa nchi yetu ya Zanzibar ilio mikononi mwa wakoloni weusi (Mtanganyika). Wao ndio waliokua sababu ya kutawaliwa kwetu au kupata madhila haya ya leo na ya jana.waliopata wazee wetu na tusipoangalia watapata vizazi vyetu na vijukuu vyetu. Baada ya kumuona na kumsikia Naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Tarehe 24/4/2012 hapo ukumbi wa Baraza la wawakilishi wa zamani niligundua au kupata hisia kwamba Ndugu Vuai hajui kitu au bado na yeye anaitumikia Tanganyika katika kuimaliza Zanzibar na wazanzibari wenyewe.
  Huo unaoitwa Muungano hauna faida yoyote bali umejaa hasara kwa wazanzibar na Zanzibar yenyewe, hata utamaduni, silka, na mila zetu zinapotea na nijambo lenye hasara kubwa katika uso wa dunia hata kiuchumi Zanziba yaleo sio ile ya karume ya kuwakopesha watanganyika kisha wasitulipe, hatunacho cha kuwakopesha Tena licha cha kuwakopesha hata chakutumia sisi wenyewe seuze wao washatufilisi vya kutosha, nabado wanaendeleza mikakati ya kutumaliza hata hichi kidole kimoja kilicho baki Mioongoni mwa hasara kubwa za muungano huu ni kule kupoteza Roho za watu wetu akiwemo Ndugu yetu Rais wetu kipenzi chetu ABEDI AMANI KARUME Muungu amlaze mahali pema Peponi.Nyerere Alimuuwa Karume mwaka 1972 hapo kisiwandui Kwa kupigwa Risasi na watu alio
  waanda yeye kwakuwapandikiza chuki. Ushahidi wa kutosha wa Nyerere kuhusika katika mauaji ya kipenzi chetu upo na kwaanae taka marejeo ya hayo ni ushahidi ulio tolewa na walioitwa mahaini, kesi ilioendeshwa Mahkama kuu vuga Jaji akiwa ALI HAJI PANDU jaji mkuu kwa wakati ule na Muendesha Mashtaka PP alikua W. DOURADO mwanasheri mkuu wa Serikali kwa wakati ule. Nyerere Katika kesi hii alitajwa kwa jina na cheo chake na vipi aliandaa njama hizo na jinsi alivyo fanikisha mauaji hayo ingawa katika kesi hio Bwana Daourado alisema Nyerere katika kesi hiyo atajuilikana kwa jina la bwana X na ndivyo alivyoitwa hadi kesi kumalizika. Vuai kwa nafasi yake anapaswa kujua hivyo. Tena afatilie aone Mambo yalivyo hadharani. Kuna sababu tatu(3) kuu zilizo mfanya nyerere amuuwe karume nazo ni hizi zifuatazo.
  Sababu ya kwanza, wakati Nyerere anamkabidhi uongozi wa Zanzibar Karume baada ya hayo yanayoitwa Mapinduzi alimwambia Atakaa kwa Miaka kumi (10) ili kuwaziba macho wazanzibari na yeye kuji tengenezea hatima ya maisha yake, baada ya hapo aiyuwe Afro Shirazi na Serikali ya Mapinduzi na wataunda Serikali moja na Chama kimoja, Kwabahati mbaya karume kwaujasiri mkubwa na kwakujua njama za Nyerere alianza kumbadilikia na kukataa maandalizi ya kuvunja serikali yake ambayo yalikua yaanze Mwaka 1970. Nyerere akashtushwa na hilo na lika muudhi sana kwani haukua mkataba wao huo.Akaamua amuuwe na alifanya hivyo. Baadae ingawa kwa muda akaiyuwa ASP,
  Uwongozi na serikali yake Akaunda CCM kama alivyo pangia hapo awali katika mbinu zake za kuitawala Zanzibar. Karume alijifunza sana baada ya mapinduzi maana mtawala wetu Nyerere mara baada ya mapinduzi alimlazimisha karume atamke kwamba Zanzibar imejiunga na Tanganyika jambo ambalo Karume hakulitaka na ndipo alipo mtishia na kumwambia walio wapindua kawahifadhi Tanganyika na kama hataki Ataondowa majeshi yake nawao Atawapa kila aina ya msaada ili wampinduie na wamuuwe. Karume akaogopa hivyo akakubali. Kuungana na Tanganyika na kutamka kwamba Nyerere atakua Raisi wa Maisha nayeye atakua makamo wa kwanza.
  Kwa maudhi mengi ya Nyerere yakiwamo yale ya kutaka kuhodhi uchumi wa Zanzibar Karume alijitoa Muhanga na kusema Muungano kama koti likikubana unalivua na sisi tuko tayari kulivua, haya aliyasema 1971 pale alipotumwa Amiri Jamali waziri wa Fedha wa Tanganyika amuulize karume anakiasi gain cha fedha za kigeni karume alingaka kwakusema Ebo wana ume hawasachiani mifukoni; jambohili lilimuudhi sana Nyerere hivyo nyerere alimfokea karume na karume akatoa kauli hii ya muungano kamakoti aliitowa katika mkutano wa hadhara pale maisara na wazanzibari walifurahishwa mno na kauli hile.
  Sababu ya pili ni vita baina ya Nyerere na Iddi Amini mwishoni mwa 1971 na mwanzoni mwa 1972. Nyerere alipanga njama za kumuangusha Iddi Amini kule Uganda na kumrudisha Obote hivyo aliagiza majeshi kutoka Zanzibar na kweli walipelekwa hadi bandarini lakini karume aliposikia yeye mwenyewe alikwenda bandarini na kuwarudisha majeshi kambini Chukwani na Ubago na kusema yeye hawezi kutoa damu za wa Zanzibari kama Nyerere. Karume alisisitiza kwamba kama Nyerere anataka Pesa na silaha kwa ajili ya wanajeshi wake atawapa na kweli aliwakopesha pesa na aliwapa silaha zikiwemo Light machinegun na Medium machinegun ambazo zote zilikamatwa na majeshi ya Amini pale Minziro Forest. Kwa wakati ule ukiacha Mizinga basi silaha hizi zilikua ndio silaha kubwa na ndio maana zikachukuliwa kama silaha za msaada (Support weapons). Silaha hizi zilikua mali ya Zanzibar na zilinunuliwa nchini china wakati Mheshimiwa Ramadhani Haji bado yuko hai aulizwe kuhusu ukweli wa suala hili. Aliekufa ni Musa Maisara Kheri, Luteni Kanali Mkuu wa Wafanyakazi Aidha pesa zetu zilizokopwa kwa vita hivyo labda akatulipe Mungu huko alikotangulia Nyerere. Baada ya tendo lile la kurudisha majeshi Karume aliandika kitabu kidogo kilichoitwa MWANAJESHI SAWA NA MWANAGU NILIE MZAA vitabu hivi vinapatikana makumbusho ya Jeshi na hata hapo migombani kuna maktaba ya kijeshi vipo kama wa Tanganyika hawaja vichoma moto.
  Suala hili nalo lilimkera Nyerere sana kwa sababu hizo na nyenginezo. Nyerere aliamua kumuua Karume na Tabaan alifanikiwa kuiondosha ASP na Serikali yake. AZIMIO LA ARUSHA nalo likafika hadi aliko kutaka Nyerere. Hivi karibuni Ndugu Vuai alisema moja ya faida kubwa ya muungano ni kule kuzama kwa Meli ya Mv Spice na michango ya Watanganyika. Ama mimi hili ninaona nikumdhihaki Mungu na sina shaka atamlipa. Kwanza lazima tufahamu kwamba Meli yenyewe imezamishwa na watanganyika na sababu zangu ni hizi;-
  (1) Nahoza wa Meli hio ni mtanganyika Mkaazi wa Temeke kabila lake ni Mzaramo Kazaliwa wa Mkoa wa Pwani na Watanganyika wanajua yuko wapi hivi sasa na wanajua kua anatafutwa Zanzibar kwa kosa la mauwaji lakini hawamleti kwanini, kwasababu ni njama zao wenyewe
  (2) Meli iliondoka Tanganyika ikiwa tayari imesha anza kuzama nyuma ama kwa visingizio kwamba Mzigo umezidi nyuma au inaigia maji kwa nyuma. Tanganyika ndipo penye SUMATRA na Chombo hakiondoki mpaka kikaguliwe na wao, jee hichi ilikuaje wakakiacha si kwasababu walitaka kukizamisha ili baadae iundwe tume ambayo wao wana uhakika watakuemo katika Tume hiyo nawatajifaidie pesa za wa Zanzi bari wanyonge walio tawaliwa na wao.
  (3) Hapo bandarini unguja wapo maafisa wa Usalama kutoka bara ambao mbali ya kazi zao za kulinda bandari ya Zanziba kama Mpaka wanchi lakini pia wana jukumu la kulinda usalama wa Raia na Mali zao Jee meli hii hawakuiyona au waliona bora wapate tu shilingi elfu kumi kila mmoja kwa kuchochomeka Raiya katika meli hiyojapo wameshajaa
  (4) Meli hio ilizama Nungwi Karibu sana na ufukwe na ilianza kuzama saa 6 usiku wakati inazama vyombo vingi vya habari vilikua vina piga kelele na vyombo vya dola vilikua vina sikia. Na hata kama vilikua havisikii basi hebu tuweke wazi; Jeshi la Wanachi Commande ya Nevy ina rada 2 zilizopo Kidoti unguja na Wazo hill Dare es salam zote zinaangalia eneo la tukio hivyo kwa vyovyote tukio waliliona mapema aidha Commande hiyo ya Navy inazo meli za vita na uwokozi moja ya meli hio ni Pono ambayo ni kamisheni boti na imepewa nambari ilio anza na P… kwavile ni cammision bot. Boti hii sawa na Rada inatumia GPS hivyo kama walitaka wangewezakuwaokowa Wahanga usiku huohuo.
  Inawezekana Rada Opereta wa rada zote 2 kwa sikuhiyo walipitikiwa na usingizi lakini pia itakumbukwa kwamba hapo migombani kuna ofisi inaitwa chumba mahususi wao ndani ya chumba hicho kuna vifaa kadha vya kupokelea habari ikiwemo TV, Radio Domestrec, Radio Commonication, nk tukiacha redio Nuru na nyengine zilizo zikitangaza mfululizo pia watu binafsi walikua wakipigiana simu jee mawasiliano kwasiku hiyo yalikua mabaya hawakuyanasa? kadhalika Nahoza wa meli iliopata ajali Mv Spaice Alikua ana wasiliana na Control tower kwakutumia Channerl 9 au 10 au12 au ya Dharura Channerl 5 jee Majeshi hawakunasa hata moja wakati sikuzote wana moneter mawasiliano ya Bahari,
  Ukweli walinasa mawasiliano yote na ndio maana wale majeshi wa Afrika kusini waliokuja Tanzania kwa zoezi la Natural fire wakasema kuna meli inazama Nungwi GPS au MILLS 100 umbali wa Nutecal male 5 kutoka ufukweni nungwi na kwa Boti ya Pono kutoka kigamboni hadi eneo la tukio watatembea kwa saa 2 na Dakika 35. lakini kwakua ni wa Zanzibar wanao zama hata hawakujali,
  Nnajua hawakujali kwasababu boti zote za kigamboni ziko Bahari kuu zina walinda wachimba Mafuta ati kwa sababu wakiingia Eneo la Zanzibar wenyewe hawakubali hivyo wanawapa ulinzi wafanye watakavyo
  Eti sababu nyengine uwokozi ungekua mgumu kwavile ni usiku. Vuai unalishushiauwezo
  Jeshi. Labda hujui kua jeshi lina uwezo mkubwa wakufanya kazi usiku zaidi kuliko Mchana Tukiacha Mafunzo maalum waliopewa na Muizrail Kanali Nioma basi pia wana vifaa vya Muangaza. Kama wangetaka wangepiga Barlight na kwa uwokozi hule wangetumia mawili au matau tu yaani eneo la ajali lingeonekana kama mchana Saa 6. Tuseme hawakutaka tu.

  Hata wa Afrika kusini walikasirika na ndio maana hawakusaidia chochote maana walisema Tokea mapema na walikataliwa kwenda kuokowa ati wanaficha siri. Na badala yake wali wapeleka wakati meli na vifaa vimesha zama hivyo na wao kwa kuiyogopa Aibu hile waliwacha goma kama lilivyo na wakaahidi baada ya miaka mitatu watakuja na Nyambizi kuja kuitoa meli hile jamani huu si utoto.
  (5) Hata kulipo kucha Jeshi ilikataa kushiriki katika maokozi ingawa hili mimi siwalaumu sana maana jeshi sio la wa Zanzibari nila Tanganyika na ushahidi Hebu tuangalie wanapo fanya sherehe za UHURU wa Tanganyika wanatumia hata Ndege za Kijeshi wakati sisi tukifanya sherehe ya mapinduzi tunawalipa kila askari anae cheza paredi shilingi 160,000 Mbali ya chakula asali Mayai njugu zabibu na chai iliotimilia hadi paredi imalizike na ikisha wanala zimisha Raisi wetu akalenao chakula cha pamoja cha kuagana.
  Inaeleweka kukataa kwao ni kwa mujibu wa sheria ya Ulinzi wa taifa National deffance Act No 24 ya 1966 ambayo pia imeipa uwezo Jeshi kujiundia kanuni zake na Kanuni ya majeshi ya ulinzi juzuu ya kwanza Utawala kifungu 15.02 na kifungu 15.13 Kanuni hizi zimeundwa chini ya kibali cha rais wa Tanganyika kifungu 15.01 vinajieleza na hata NDA namba 24 kifungu cha 21 kinaeleza kwa urefu maelekezo ya utendaji ikiwa nipamoja na kumdhalilisha Rais wa Zanzibar
  Hata katiba ya kikandamizaji ilio wekwa mwaka 1977 mika 5 baada ya kifo cha Karume toleo la 2005 kifungu(Ibara) ya 148 (1) cha katiba hiyo kiliwazuia majeshi yasiwaokowe wazanzibari hii nikwasababu majeshi hawapaswi kutenda kazi yoyote ya dharura kama hiyo pasi na amri ya Rais wa Tanganyika ambaye kwa sasa ni Kikwete nae hakutoa agizo hilo la kuwaokowa wa Zanzibar na ndio maana wakaonekana majeshi walikua ama wakishika kiuno pale nungwi kama watalii na au wakipokea maiti tu jambo ambalo madaktari wetu walikua na uwezo nalo.
  Tukio la nungwi ni la dharura sana Ingekua Rais wetu anauwezo wa kuyaamrisha majeshi kwa ninavyomfahamuMheshimiwa Sheni kwa Huruma zake na jinsi tatizo hili lilivyo mgusa angefanya hivyo lakini bahati mbaya kwamujibu wa sheria hizo zilizo wekwa na Nyerere tokea kipindi kile Karume aliporejesha majeshi wasiende Mtukula kinamyima uwezo wa kuamrisha majeshi hata waliopo Zanzibar ni afadhali mkuu wa mkowa wa Tanganyika anao uwezo huo kwa mujibu wa sheria. Anapaswa aulizwe Vuai JEE HII NDIO FAIDA YA MUUNGANO? Jeshi lina uwezo mkubwa wakuokoa watu na Malizao ukitaka kujua ukweli huu angalia mafuriko ya DSM, ndani ya masaa 3 watu wote wamesha okolewa
  Hizo na sababu nyengine nyingi ambazo zinanisukuma kusema meli ilio zama nungwi imezamishwa kwa makusudi na watanganyika na akina Vuai kama Mtaji wa kisiasa. Ndugu Vuai Miongoni mwa faida alizo zitaja kua za muungano ni VITA ya kagera na kwamba alidai ALH HAJI USTADH SHEIKH IDDI AMINI DADAYE kama sio vita vile kushindwa ange fika hata Zanzibar; labda niulize jee ukiacha Tanganyika Nchi ni Zanzibar pekee? Kwanini asivamie Kenya? Bora na hapa niweke wazi pengine Vuai hajui chanzo cha vita nacho ni wa Tanganyika kua WACHOKOZI na UDINI
  Chanzo cha vita ni nyerere kutaka kumrejesha OBOTE katika utawala jambo ambalo Nyerere alidhani litapunguza nguvu za waislam Uganda na alifanya hivyo Baada ya Alhaji Sheikh Marehemu Iddi Amini Dadaye Muungu amlaze Mahalapema Peponi (amina) kutaka kujenga Msikiti mkubwa Bukoba Msikiti ambao alitaka uwe wa Afrika Mashari na kati yote ili waislam wafanyie Ijitmai na mambo mengine ya aina hiyo ya kiislam.
  Msaada wa Ujenzi wa Msikiti huo ulitolea na kipenzi chetu Habibi AMARY GADDAF ambaye katika kipindi hicho hicho alitusaidia na sisi wa Zanzibari Tujenge msikiti mkubwa wa Tanzania yote Pale Muembeshauri. Kwa bahati mbaya Pesa za kujengea Msikiti huo pamoja na za kulipwa watakao athirika na ujenzi huo zilitumika kununulia mabomu ya kwenda kumtwanga muislamu mwenzetu hadi leo msikiti hule haukujengwa badala yake palijengwa kituturi kiliopo sasa tena baada ya miaka kadhaa na Serikali kuona aibu.
  walio athirika na ujenzi ule hadi leo hawajalipwa na kule Bukoba Nyerere alitumia majeshi yote wakiwemo wa Zanzibar kuhakikisha Amini amepinduliwa ili asiweze kujenga huo msikiti na kumrudisha Ubote akakuze ukristo. Ndugu zangu akiwemo Vuai Amini hakua na silaha wala askari wakutosha wakuichokoza Tanganyika bali ni Nyerere baada ya matayarisho ya vita ya muda mrefu ali Mvamia Amini. Ambaye Silaha Kubwa Aliokua Nayo ni ile tulio zowea kuita BM 40B nayo ilikua mizinga minne.
  Mizinga hii iliwekwa Itigi, Jinja, Masaka na Intebe Mizinga yote hiyo ilipigwa na ndege zetu isipokua mmoja tu uliokua Intebe ulitekwa mzima na ndio uliokua unaoneshwa kama silaha kubwa ya Amini Na Askari wake wote ni Brigadi moja ambayo ilikua inaongozwa na Brigedia General Aizak Maliyamuungu Briged hii ilikua na Batalioni Nne ambazo zilikua zimewekwa Mbarara ilikuepo Simba Makanizim Batalion, Jinja Gadaff Barack Bombo ilikua Bombo Baracks na moja ilikua Batalian mchanganyiko ilikua Kampala hii ilibeba Komando.Reconaises na Field Eginiar.Troops. Vyote kwa pamoja pamoja na vikundi vya utawala vinaunda Briged moja ilio ongezwa. Aidha Iddi Amini silaha nyengine aliotegemea ni 60mm Moter
  Kadhalika alikua ana silaha inaitwa 106mm ambayo ilikua imefungwa katika gari na zote zilikua Waganda pia walikua na 12.5mm Ant Air Craft 12B na zenyewe zilikua zimefungwa katika gari silaha hizi zilikua 4tu na zilikua zinatembea kwa vikosi vilivyo mstari wa mbele.
  Wakati Amini ana vijisilaha hivyo Sisi tumeingia vitani na Silaha za kileo naAskari walioingizwa vitani tu niDivision 2 za Kivita.ukiacha waliokua kwenye Mipaka mengine na waliokua vikosini (Makambini) Kwa muundo wa Tanzania Division moja yakivita ina Brigedi 4 wakati Amini alikua na Brigedi moja tu hivyo sisi tulikua na division 2 sawa na Brigedi 8 kati ya hizo Brigadi 2 zilikua za silaha za Msaada ambazo nipamoja na BM 40B Mizinga ya kirusi yote ilikua 12 yaani kila briged ya Msaada ilikua na mizinga sita Pia tuliingia vitani tukiwa na mizinga ya 120mm moter Silaha hizi zilikua 10 na zote zilichukuliwa hapa Zanzibar na hadi leo hazija rejeshwa na sio hizi tu bali hata silaha ndogo

  ndogo Salf Wipon hazijarejeshwa hadi leo na hata Pistol zilichukuliwa hapa unguja na hatimae waliuziana Watanganyika Silaha nyengine zilizo ingizwa Vitani na Watanganyika ni pamoja na 122mm Moter Silaha hizi zilikua 18 nazo zilichukuliwa hapa Unguja kule Dunga Camp na hadi leo hazijare jeshwa ziko Tanganyika.na zimewekwa Arusha zilitaka zitumike kwa kuivamia Kenya kipindi kile Nyerere alipo mwita Jomo Kenyata Nyangau.hadi leo ziko huko. Kulikua na silaha nyengine ambazo nazo zilichukuliwa hapa unguja na hazija Rejeshwa Hadileo labda zitarudi baada ya Jumbe alie zipeleka azidai nazo ni 130mm
  Kulikua na silaha nyengine ambazo ziliwekwa kwa hali ya Tahadhari nazo ni 155mm zilikua 10 na ziliwekwa Mwanza pale Nyegezi na Pasiasi juu. Hizi hazikutumika mpaka vita vimekisha isipokua mabomu 3 tu ya majaribio Mabomu yake yamehifadhiwa gongo la mboto na ndio hayo yanayo ripuka leo. Silaha nyengine ambayo nayo iliwekwa kwa tahadhari na haikutumika ni 166mm hizi zilikua Dodoma zote zilikua 14 Tulikua na vijisilaha vidogo vidogo kama alivyo kua navyo amini lakini sisi tulivigawa kwa kila Batalian Hapa Zanzibar ziliondoshwa silaha nyingi hata Stellar za kutungulia ndege ambazo kule Uganda tulizigawa kwa askari wa miguu nazo hazikurudi labda muhudi ashuke na hata mizail za mwanzo tulizo pewa na warusi ziko doodoomaaaaaa!!!!
  Silaha nyengine hatutazitaja kwa usalama wa Nchi.
  Ndugu yetu katika imani Ustadhi IDDI AMINI alipoingia vitani alikua na Ndege za kivita 10 tu na zilikua Makao Makuu yake yalikua Nakasongola Air Port na wakati wa vita ziliwekwa Intebe Air Port. Wakati sisi tuna ingia katika vita tulikua na ndege za vita Aina 2 ambazo Basse zao zilikua Ngerengere Air Force zilikuepo ndege 20 za kichina Mig 19 Na Basse nyengine ilikuepo mwanza hapa palikua na ndege 15 za kirusi Mig 21 na zote hizi zilitumika kumshambulia Iddi Amini.
  Si Hivyo tu lakini tumeingia vitani tukiwa na Vifaru Lage Tank 20 Wasomaji wa Makala haya ukipenda kujua idadi ya askari wa kitanzania walio ingia vitani unaweza kufanya hesabu ifatayo Division 1 ya kivita kwa Tanzani inakua na Brigedi 4 moja kati ya Brigedi hizo inakua ya msaada zilizobaki zinakua za Infantry kila Brigadi ya Infantry inaku na Batalion 4 Kati ya battalion hizo moja inakua ya msaada na utawala maranyingi inakua Acheron. Na 3 zinakua za Infantry Kila battalion 1 ya Infantry inakua na kombania 4 za Infantry na kila kombania 1 ina Platon 4 na kila Platon ina Section 3. na Sectin 1 ya kimapigano kwa Uganda ilikua na watu kati ya 15 na 20 hii ilitegemea na idadi ya mgambo walio pelekwa katika kikosi hicho.
  Katika muundo huu hata silaha za kutungulia ndege zilibebwa na Askari wa Miguu Infantry. Ukiangalia hesabu hio utaona kua Amini hakua na uwezo hata wa kuthubutu kuchokoza seuze kuvamia. Kwa kweli Tanzania ilijiandaa ilikua na matayarisho yakutosha wakati Amini hakua na habari kabisa ya vita. Vita hii sisi wazanzibari ilitupa hasara kubwa na miongoni mwa hasara tulizopata nikupoteza roho za ndugu zetu wengi na wengiwao waliuliwa na watanganyika.
  Wakati tunaingia vitani pale Kagera watanganyika walitega mabomu na hawakuweka alama yoyote Kama ilivyo sheria za uwekaji mabomu na baadadae wakawambia wazanzibari wasonge mbele. Hapa ndipo mwanzo tulipopoteza vijana kadhaa wakiwemo Pte Mikidadi wa Bambi Unguja, Pte Shehe wa Kaskazini Unguja. Pte Mwalimu wa Makunduchi Uguja, Cpl Ali Musa Msuwaki wa Mitakawani Unguja na Pte Daudi Muhunzi wa Donge Unguja. Wengine walioathirika Ni Pte Mohd Omari ambae alikatika Mguu na yupo hapo Darajabovu baada ya kutelekezwa na Jeshi. Hivi sasa amekuwa mganga wa kienyeji ili apate riziki yake. Cpl Nassor wa ndijani alikatwa Hasua. Yeye bado angali hai. Wengine ni Pte Juma Ali ambae yupo Saateni. Yeye hana mguu hata mmoja. Wengine ni Kitiba wa Chaani, Major Ali Nassor wa Donge na Mila wa Bandamaji ambae kafa kwao akiwa na vipande vya bomu katika uti wake wa Mgongo wala hakuna aliemjali. Wote hawa wameacha vizuka na mayatima.
  Majeruhi wote Nyerere aliagiza kwa maneno kwamba wajengewe nyumba. Wazanzxibari hata kibada hawakujengewa. Kinyume chake wako waliowekwa ndani kwa kudai haki zao. Wakati wenzetu wa Tanganyika wamejengewa nyumba na wagonjwa wanaendelea kutibiwa Lugalo mpaka wafe, wazanzibari wana kejeliwa na kudharauliwa. Hasara haikua hii tu kwa vita hivi, Zanzibar iliathirika kwa kiasi kikubwa kiuchumi. Nyerere baada ya vita alilitangazia Taifa miezi 18 ya halingumu kiuchumi lakini sisi wazannzibari ilikua miaka 18. Wakati Nyerere anafufua uchumi wake alikua pia anadidimiza uchumi wa Zanzibar sisi tulifikia hata mshahara wa wafanyakazi wetu ukatushinda.
  Watanganyika walifikia pahala hata zao letu la karafuu wakalitoa katika biashara za kimataifa badala yake wakaingiza korosho. Mzee wetu Jumbe alipokwenda kwa Nyerere Kumtaka zao hilo lieleweke kama mazao ya kimataifa kutoka Tanzania alijibiwa basi Maghala ya karafuu yakajengwe Dodoma. Jamani huu si unyama wa hali ya juu na kashfa dhidi ya wazanzibari? Kuna faida ya muungano hapo? Vuai kwa hoja hii atufafanulie. Tunamshukuru Mzee Jumbe, kwa hili alisema bora tufe sote kwa njaa lakini karafuu haitakwenda kuhifadhiwa na kuuzwa Dodoma. Hali ya Zanzibar ilikua mbaya hata ikafikia pale kwa Suma ya leo ndio pekee palipokua na biashara tena biashara yenyewe ni ya vyungu vya Udongo.
  Mungu hamtupi mja wake. Bahati nzuri Jumbe akajiuzulu na Awamu ya Ali Hassan mwinyi na Seif Sharif Hamadi ikafika. Tunapaswa kuushukuru sana utawala huu kwani hali ya kiuchumi Zanzibar iligeuka ghafla na ikawa kuliko Tanganyika. Jambo hili ndio lililojenga misingi na ikawa hadi leo pamoja na vita vyote vya kiuchumi ambavyo Tanganyika inaipiga Zanzibar kamavile kutupandishia ushuru, kuweka ushuru mara mbili (2) na kutuletea TRA bado wazanzibari wanapata riziki zao. Hivi tunavyo zungumza pia watanganyika wamekataa kuliondowa suala la mafuta katika orodha ya mambo ya muungano na hivi sasa wako bahari kuu pamoja na kampuni ya kichina wanachimba Gesi na mafuta ya Zanzibar chini ya ulinzi wa Jeshi la wananchi Commande ya Nevy. Meli zilipaswa kutumika kuokowa waliopatwa na maafa kama yale ya Nungwi badala yake zinazotumika kuwalinda wachina. Ni juzi tu wasomali walipita karibu na meli hizo na walishikwa.
  Nyerere aliamuwa kumchukua Ali Hasan Mwinyi na kumfanya Rais wa kwao Tanganyika. Alifanya hivyo kwa kudhani kwake kua mipango ile ni mbinu za uongozi wa Ali Hassan ndio inayofanikisha kumbe sivyo. Alipogundua kua Ali Hassan hana uwezo wowote alimtukana matusi ya nguoni. Badala yake alipofahamu kuwa kazi yote ile iliyofanyika katika kipindi cha Ali Hassan cha kuisuka Zanzibar kiuchumi ilikua ni kazi ya Seif Sharif aliamua kumfukuza ili Zanzibar jitihada hizo zikwame na Zanzibar ididimie kama zamani au zaidi.
  Hapo mwanzo dhamira kubwa ya muungano ilikuwa ni ulinzi. Sikweli kwamba ulinzi uliopo ni wetu bali ni ulinzi wa wawala wetu. Kwa hapa Unguja walinzi hawa (polisi na jeshi) wameletwa au kuwekwa kulinda maslahi ya Tanganyika. Kama kweli ulinzi huu ni wa muungano ni Afisa yupi mnadhimu katika maafisa wakuu wa Jeshi alie Mzanzibari? Muundo wa Jeshi la Tanganyika liitwalo la Tanzania ni Mkuu wa Jeshi, na Anawasaidizi wake. Wa kwanza ni Afisa mnadhimu mkuu Luteni Ganaral (Chief of Staff) (C of S), wengine ni Mkuu wa Mafunzo na Utendaji wa Kivita (Cheiff of Oparation and Training)(COT), mwengine ni Mkuu wa wafanyakazi (Chieff of Parsonnel) (CP) na mwengine ni Mkuu wa Usalama (Chieff of Military Intellagence) (CMI) nk. Kati ya wote hao hakuna mzanzibari hata mmoja.
  Si hivyo tu hata katika Commande zake zote yaani Land Force, Air Force na Marine zote hakuna mzanzibari ambaye ni kiongozi. Katika Comande ya Nevy yupo Mzanzibara Mndegereko Major General Saidi Omari Mzaliwa wa Bagamoyo ambae amekulia kwao Rufiji na kuajiriwa katika Jeshi hapa Zanzibar. Huyo ndie anaeitwa mzanzibari. Baadhi ya jamaa zake wapo Kwahani. Comandi zote hizo zinaongozwa na mamajor generali lakini hakuna mzanzibari mwenye cheo hicho hata kama ana elimu ilio wapita wote hao. Tena wapo wengi lakini akifikia muda apandishwe cheo anastaafishwa.
  Mimi kwa maoni yangu Muungano huu hautufai hata chembe. Na kama lazima tuwe na Muungano basi tunashauri tuwe na Muungano wa Mkataba wa nchi mbili na serikali Mbili (ya Tanganyika na ya Zanzibar). Serikali hizo kila moja iwe na mamlaka yake mwenyewe na inafanya mambo yake yenyewe. Kila serikali kwa hivyo iwe ina mamlaka yote ya kusimamia vyanzo vya kiuchumi, Mahusiano ya kimataifa, Ulinzi na Mambo ya ndani. Aidha Mambo ya Muungano yatasimamiwa na Bunge la Muungano litakalopatikana kutoka katika mabunge ya Tanganyika Zanzibar.
  WITO KWA WAZANZIBARI WOTE TUJIPANGE KUIKOMBOWA NCHI YETU KWA KUTUMIA NGUVU ZETU ZOTE.
   
 2. Grand Master Dulla

  Grand Master Dulla JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 378
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Daaa!! kweli nimekukubali we ni mjuvi sana tena nimekubali kwamba mnaonewa sana,ila msife moyo uonevu una mwisho wake,angalia south afrca,zimbabwe na kote kwenye uonevu una mwisho jitahidini msikate tamaa.nilikuwa nataka nikuulize hivi hicho kijitabu cha BABU mbona sijawahi hata kukiona nitakipatia wapi ndugu yangu.MAPINDUZI AU UVAMIZI,nakiri sijawahi kukiona na ndo kwanza nakusikia wewe ukikitaja,mi najua babu mpaka kufa kaandika kitabu kimoja tu cha AFRICAN SOCIALISM OR .......

   
 3. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,183
  Likes Received: 700
  Trophy Points: 280
  Vitabu vipo ukikitaka utakipata tu.
   
Loading...