Watambue madalali wa shetani

Hivi umeshawahi kuimagine ulimwengu usingelikuwa na dini kabisa....nini maoni yako?
 

USIJALI NAKUPA FACT:

Safina Radio ya Arusha ni wanyonyaji wa pesa za watu wanaohudhuria pale, binafsi yangu nimewaongelea tu Wanawake masikini wakiwa ndio wanyonywaji wakuu na hawa watumishi TUMBO.

Hao walioondoka waliondoka kwakuwa walikuwa wakihudumia kiroho haswaa na walipendwa sana na waumin wa pale ila hilo likamuumiza Mkurugenzi wao Daniel Lema.

Kwa mfano, Luca alishakuwa akifanya ibada hasa maombi ya kufungua watu pale pale na watu wakawa wanatamka wazi wazi kuwa wanatoa sadaka special kwa Luca, kuna mama aliahidi kumnunulia kiwanja na wengine watamjengea...HIYO HABARI IKAWA MWIBA MKALI KWA MKURUGENZI.

Luca akafanyiwa figisu figisu mpaka akaondoka...ILA maajabu ni kwamba waumin haohao ndio walikwenda kumjengea luca nyumba ya ibada kwake na kumzungushia uzio na sasa ana waumin wengi sana. Na hii ni habari isiyompendeza LEMA na kuna namna huwa watangazaji wa radio yake wanatupa madongo kwa Luca..

MWABUKUSI CASE:

Mwabukusi yeye huwa anadeal na samaritan organisation ya kuwasomesha watoto yatima (Compassion ya Arusha) yeye alitoa ushauri kuwa kiasi flan cha sadaka za safina ziende kuwasomesha hao watoto wenye hali mbaya (kumbuka Mwabukusi alikuwa mtumishi pale)...Hiyo ikawa habari mbaya kwa Mkurugenzi DANIEL LEMA, later Mwabukusi alisema wazi katika baadhi ya Makanisa kuwa ni ngumu kufanya kazi na Mkurugenzi wa Safina. Mungu kamwinua Mwabukusi na amepata wafadhili wengi tu.

Tunaifahamu Safina Radio tangu inaanzishwa, sio tunakurupuka.

Umewahi kuanalyse ile hela ya minara iliyopatikana na kazi iliyofanya?
 
Ndio maana kila mtu ana kanisa siku hizi,naona huruma wale waumini wa makanisa ya hawa matapeli ,wengine wameuza mpaka nyumba na kupeleka hela kanisani ,,,,,,,,,,,Akili za binadamu zimehamia kwenye kisigino
 
Soma biblia utaelewa... OMABA SANA NA ROHO MTAKATIFU ATAKUFUNULIA NA KUKUONYESHA NA KUKUFUNDISHA NAMNA GANI YA KUWATAMBUA.... Na swali la kujiuliza jee wanafanya wakiongozwa na roho gani? Kutenda miujiza na kufanya uponyaji hata kalumanzila yanafanyika ila kwa roho isiyo ya Mungu...
 
Hela ya minara sijui hata wanakusanya kiasi gani ndio maana hata siwezi kuifanyia analysis
Sawa, na hayo mengine ulikuwa unayajua?

Unajua kuwa kuna wakati Safina Radio waligoma tu kurusha matangazo ya Radio ya mafundisho ya Mwl. Mwakasege bila sababu za msingi?

Yalivyoanza kurushwa na Radio Sauti ya Injili ya KKKT moshi, ndio nao wakaanza kurusha ili wasipoteze wasikilizaji?
 
Mtume Kibwetele nae yumo?
 
Inaonyesha ni kwa kiwango gani humjui mtumishi wa Mungu Kakobe. Ndiyo maana namuunga mkono mtoa post kwamba SIYO WOTE. Wewe unakurupuka. Onyesha utajiri wa Kakobe. Acha chuki binafsi. No research, no right to speak.
Amka hakuna eoho ya Mungu kwa huyu mtuu... Tena kwa taarifa yako huyu ndio aliyeanza akapiga pesa kuliko hawa wa sasa... Maana hata watu wengi walikuwa hawastuka bado..
 
Kuhusu lucas niliwahi kulisikia wakati niko arusha, tangu niondoke hayo mengine sijui

Sawa Mkuu, Ila yapaswa tujue kuwa MUNGU HADHIHAKIWI.

Pili Mungu anapaswa kuabudiwa kwa Roho na Kweli (Kwa kuongozwa na Roho wake) si kiushabiki na kuiga huduma za wengine (kama Otieno anayemwiga Mwakasege hadi kuongea).

Tatu, kufundisha NENO na UHUSIANO NA MUNGU ni muhimu kuliko MIUJIZA.
 
Laaaa hii huwa ni kali, tena hao wachungaji feki wameligawa kanisa kwa grade ya utoaji wa sadaka kuna waumini wa kuanza kutoa sh elf 5 labda mpk laki,wengine kuanzia laki mpk 1 mil,kuna wa kuanzia hiyo 1 mil kuendelea hapa ndipo utajua usemi wa Mungu kule ktk Hosea 4:4. WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA. S kwamba wataangamia suku zijazo bali wanaangamia wakt huohuo ww unapochukua hela yako na kuisend ktk namba za hao wachungaji wa viwango vya sadaka kisha unaenda kulala njaa na watoto hauon kuwa unaangamia kwa mda huohuo?

Una kila aina ya mahitaji ya lazima km nguo za watoto mahitaji ya kila uchao lakin we ni kukimbiza hela kwa huyo mchungaji anakutapeli lakin kakufumba macho kuwa ukitoa nyingi utapata nyingi we unadhani nikutoa pesa upate pesa? Kacheze biko utapata pesa hayo ma-laki unayotoa kwa mwaka ungekuwa unaxcheza BIKO ungeshapata pesa yako taam.

Kutoa kuko hivi km kweli unaaja ya kumtolea Mungu sadaka nenda kwa wahitaji masikin,wagonnjwa,wasiojiweza na jamii yenye uhitaji wako wengi sana,na pale unapojitolea kwa ajili yao unajiwekea HAZINA MBINGUNI si hizi hazina ya kubahatisha kwa hawa wachungaji feki.

Ili somo la zaka na zadaka hawa wachungaji feki wanawaangamiza nao sn waumini wao kwa faida zao binafsi
 
Njia ya kuwatambua ni so simple. 1. Wanafundisha na kuhimiza watu wawe matajiri hapa duniani tu kwa mafanikio ya muda tu.wanaacha kuwahimiza watu kuutafuta uzima wa milele ulio katika Kristo Yesu. 2. Hawamhubiri Yesu kama ni njia ya wokovu na uponyaji, badala yake wanajiinua wenyewe wakiichukua nafasi ya Bw .Yesu. 3. Mungu wanayemuinua, ni Mungu wao na sio MUNGU Baba wa Bw.Yesu Kristo.. Kwa mfano ,:- mungu wa machomanne, mungu wa kanisa Machomanne NK, NK. 4.Angalia matunda yao sio matendo yao-- Wazinzi, Wanazaa nje ya ndoa zao, Wafiraji, Wabakaji, Watu wenyewe visasi.. 5. Wananena kwa Lugha zisizofahamika wakiunga na kiswahili kama za watoto wanaojifunza kuongea (baba, mama, Dada, kaka, tata, Toto, dodo, moto,raba, sata,maka, NK,NK.), ukiwabana wanakwambia wanaongea lugha ya kimalaika.. 6.Zingatia haya:--- a.Lugha ya malaika hata ibilisi anafahamu kwa vile naye ni malaika. b. Watu wanapaswa kufundishwa kuhusu safari ya kwenda mbingini aliko Yesu, na sio Ulaya wala America. c. Utajiri wa duniani sio kipaumbele cha mkristo bali ni Ufalme wa Mbinguni. Utajiri ni kitu cha nyongeza..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…