Watalii kutoka China wahimiza maendeleo ya sekta ya utalii Tanzania

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1000.jpg


Muda mfupi baada ya serikali ya China kuondoa kizuizi cha mwisho cha hatua za kupambana na janga la COVID-19, wachina walianza kusafiri kwenda katika nchi mbalimbali duniani. Mwishoni mwa mwezi Aprili kundi la watalii 28 kutoka China, lilikuwa ni moja kati ya makundi ya mwanzo kusafiri kwenye nje ya China na kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kwa ajili ya kutalii nchini Tanzania.

Tanzania inaichukulia China kama moja ya masoko muhimu ya utalii, sio tu kutokana na ukubwa wa China na uwezekano wa kuwa chanzo kikubwa cha mapato yanayotokana na ujio wa wachina, lakini pia utofauti wa mwenendo wa watalii wa China ikilinganishwa na masoko ya jadi ya utalii.

Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Utalii ya Tanzania Bw. Damasi Mfugale alisema baada ya ujio wa watalii hao, kuwa si kama tu wamekwenda kutalii, bali pia wamekwenda kuhimiza mahusiano ya kiutamaduni kati ya China na Tanzania, na hata kurudisha uhai uliokupweo kwenye mawasiliano kati ya watu wa China na Tanzania yaliyokuwepo kabla ya janga la COVID-19.

Wadau wa sekta ya utalii wa Tanzania wamekuwa ni waungaji mkono wakubwa wa ujio wa watalii kutoka China. Sababu moja inayotajwa ni kuwa mbali na kulipia gharama za usafiri, malazi na chakula, watalii wa China pia wanapenda kununua zawadi na vitu vya ukumbusho wanavyorudi navyo nyumbani. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Utalii duniani mwaka 2021, kwa wastani mtalii wa China anatumia dola za kimarekani 1,250 kwa safari moja, kiasi ambacho ni zaidi kwa asilimia 35 ikilinganishwa na watalii kutoka Ulaya. Sababu ni kuwa watalii wa nchi za magharibi hawana desturi ya matumizi makubwa, matumizi yao yanajikita zaidi kwenye tiketi za ndege, malazi, chakula na hela ya kiingilio kwenye sehemu za vivutio.

Hata hivyo kumekuwa na changamoto moja kubwa ya namna ya kuendana na watalii wa China. Wachina ni watu wenye desturi tofauti, siku zote wanapokuwa mahali popote, wanapenda kujua ni nini kinaendelea nyumbani kwao wanapenda kutazama televisheni zinazoonesha mambo ya nyumbani kwao wakiwa kwenye nyumba za watalii, wanapenda kutumia pesa kwa mifumo yao kama vile Alipay na Wechat, na pia hawapendi kusahau ladha za chakula chao. Ni hoteli chache sana za nchi za Afrika Mashariki na hata katika nchi nyingine za Afrika, zilizoweza kuweka mazingira yanayoendana vizuri na watalii kutoka China.

China inatambua kuwa sekta ya utalii ni moja ya maeneo yanayoweza kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa nchi za Afrika, na hata kuimarisha mafungamano ya watu wa pande hizo mbili. Mwaka 2004 ilizitangaza nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda, kuwa maeneo yaliyochaguliwa kutalii (Approved Destination Status).

Kabla ya janga la COVID-19, wachina zaidi ya milioni 155 walisafiri nje ya China kwa ajili ya utalii, idadi ambayo ilikuwa ni asilimia 10 ya watalii wote duniani. Idadi hiyo kwa nchi za Afrika mashariki ilikuwa ni wastani wa watalii elfu 30 kwa mwaka. Kutokana na wingi wa watalii kutoka China, na wingi wa vivutio vya utalii katika nchi za Afrika, kama mazingira yataendelea kuboreshwa bila shaka idadi ya watalii wa China katika eneo la Afrika Mashariki itaendelea kuongezeka.
 
Back
Top Bottom