Watalaamu wa masuala ya uwekazaji wa amana na mifuko ya serikali naomba mnijibu swali langu hili

From Meru

JF-Expert Member
May 19, 2023
2,381
5,231
Nikiwa kama miongoni mwa raia tunaopambana nje ya mfumo rasmi nimefikiria kuwekeza kwenye mfuko wa amana za serikali wa UTT AMIS kwenye scheme ya BOND TRUST FUND ambayo itanipa gawio la kila mwezi. Mfuko huu ili kupata gawio la kila mwezi kiwango cha chini cha uwekezaji ni milioni 10.

Lengo la kuwekeza ni kujitengenezea malipo yangu ya pension ya uzeeni. Nina mpango mpaka ninapofikisha 5th floor niwe nimewekeza kiasi cha milioni 90 ambayo itanipa gawio si chini ya laki 8 kwa mwezi kama pension yangu ya kunisaidia uzeeni. Kazi yangu sio pensionable.

Swali langu: Wasiwasi wangu ni hiki chama chakavu Ccm kutokana na mwenendo wake wa kuchota pesa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, hawawezi kuja kuchota pesa kwenye huu mfuko wa UTT na kuufilisi kiasi ukashindwa kutulipa sisi wawekezaji wake?

Wabobezi, wataalamu nimeweka kambi kusikia kutoka kwenu.
 
Iyo ni risk kama Risk nyingine tu achana na Chama cha Majambazi kuna kushuka kwa thamani hasa ukizingatia Tsh inazidi kushuka thamani kina uchwao...Hapo zamani kabla wengi hawajaijua UTT iyo 90M unaweza pata gawio mpaka la 1M kwa mwezi ILA sasa ili upate 1M inabidi uweke 120M So utaona thamani inavyoshuka kwahiyo unaweza jikuta unapata hypertension na Stroke ukifika hiyo 5th floo ukakuta thamani imeshuka mara dufu..Hiyo ndio stock ilivyo mzee
 
Chek8 na uwekezaji mwingine pia maana hata mambo ya stock na kama forex tu au cryptocurrency,muda wowote soko linashuka kulingana na idadi ya wawekezaji na demand

Cheki pension trust zinazoaminika na zenye consistent nzuri juu ya masuala ya retirement funds(policy)

Maana yake Nini,ni kuwa hizi trust nyingine zinakuja kwa staili ya vyama vya walimu and the so like

Goodluck
 
Iyo ni risk kama Risk nyingine tu achana na Chama cha Majambazi kuna kushuka kwa thamani hasa ukizingatia Tsh inazidi kushuka thamani kina uchwao...Hapo zamani kabla wengi hawajaijua UTT iyo 90M unaweza pata gawio mpaka la 1M kwa mwezi ILA sasa ili upate 1M inabidi uweke 120M So utaona thamani inavyoshuka kwahiyo unaweza jikuta unapata hypertension na Stroke ukifika hiyo 5th floo ukakuta thamani imeshuka mara dufu..Hiyo ndio stock ilivyo mzee
daah asante sana mkuu kenge.
 
Nikiwa kama miongoni mwa raia tunaopambana nje ya mfumo rasmi nimefikiria kuwekeza kwenye mfuko wa amana za serikali wa UTT AMIS kwenye scheme ya BOND TRUST FUND ambayo itanipa gawio la kila mwezi. Mfuko huu ili kupata gawio la kila mwezi kiwango cha chini cha uwekezaji ni milioni 10.

Lengo la kuwekeza ni kujitengenezea malipo yangu ya pension ya uzeeni. Nina mpango mpaka ninapofikisha 5th floor niwe nimewekeza kiasi cha milioni 90 ambayo itanipa gawio si chini ya laki 8 kwa mwezi kama pension yangu ya kunisaidia uzeeni. Kazi yangu sio pensionable.

Swali langu: Wasiwasi wangu ni hiki chama chakavu Ccm kutokana na mwenendo wake wa kuchota pesa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, hawawezi kuja kuchota pesa kwenye huu mfuko wa UTT na kuufilisi kiasi ukashindwa kutulipa sisi wawekezaji wake?

Wabobezi, wataalamu nimeweka kambi kusikia kutoka kwenu.
From experience thamani za vipande zinakua Kadri muda unavoenda ....pia kuhusu kuchotwa pesa Sio rahisi sababu ukitaka kuchukua pesa zako muda wowote unachukua Ni within 3 days or 10 days kulingana Na Aina YA mfuko..UTT inakusanya fedha kwenye pool Na kwenda kuinvest sehemu mbalimbali gawio watakalopata wanakuja kuligawa Kwa holders uzuri wanainvest sehemu ambazo known Na reliable kama gvt securities,bond pia Kuna viongozi wa serikali mawaziri wamewekeza UTT....so kua Na Amani
 
Mfano kipande cha Umoja 2005 kilikua Na thamani ya Tshs 70 saiv 2024 kina Thamani YA 1000Tshs
 
Mbona kama unachanganya mkuu, hao wenyewe UTT ndio wanawekeza pesa kwenye dhamana za serikali.

Pili sijui una umri gani lakini kama unataka ukuze mtaji wako kwa mda mrefu ni bora uweke kwenye umoja fund, alafu ikifika 90M ndio uweke bond fund
chama chakavu wanashindwa jambo mkuu????? hukohuko wanazikula
 
Back
Top Bottom