Waziri Bashe: Upatikanaji wa Sukari hauhusiani na masuala ya Kidini

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Bashe ametoa ufafanuzi kuhusu kauli ya uhaba wa Sukari kumalizika kabla ya Mfungo wa Ramadhan

=====

Salaam Ndugu Zangu,

Ningependa kutoa ufafanuzi wa kauli yangu iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari wakati wa maswali na majibu kwenye mkutano na wahariri uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 22.02.2024.

Kama Waziri wa Kilimo, nilitoa maelezo juu ya hali ya upungufu wa Sukari nchini, na muda wa usambazaji tunaotarajia wa shehena inayofuata ya sukari.

Nilisisitiza kuwa kutokana na usambazaji huu na hatua tulizochukua, tutarajie hadi kufikia mwezi mtukufu wa Ramadhan hali itakua nzuri.

Rejeo hili lilikusudiwa kuwa kiashiria cha MUDA kwa madhumuni ya kimipango na sio kuashiria kipaumbele chochote cha KIDINI.

Mara kadhaa nimesisitiza kwa kutaja vipindi vyote viwili Kwaresma na Ramadhani vina tukabili hapo mbeleni na kuwa tunajitahidi kama Serikali na azma yetu ya kutaka kutatua hii changamoto kabla ya hivi vipindi kufika na ndio maana tulianza kutoa vibali tangu mwezi wa 12, 2023.

Tuendelee kushirikiana kuboresha sekta ya kilimo na usalama wa chakula nchini.
 
MIMI NIMEKUELEWA VEMA.
 
Hii nchi inatakiwa kua makini sana kabla hujasema lolote hasa kwa viongozi maana ukibugi kidogo tuu kwa kumaanisha au kwa kutoeleweka vizuri watu wanaslide na kauli yako hadi utajuta.
 
Karekebisha kauli yake kutamka neno la kidini ramadhan as if nchi hii inaongozwa kwa misingi ya kiislam na ni islamic state, watu wali fume mpaka akashaa ikabidi arekebishe kauli yake
 
Solution ni kupiga marufuku dini za Ibrahim nchini, zimetuletea ujinga mwingi kuliko faida.

Sijawahi kuwasikia Buddha wala Hindu wakileta ulalamishi wa kuona wametengwa, wanaendesha mambo Yao Kwa ustaarabu wa Hali ya juu, kuna sikukuu Yao wengine inaitwa Ashura huwa wanaomba kibali kabisa cha kupiga mafataki.
 
Naomba mnisaidie wanajamii forum kwa panoja nimemwona wazri Bashe akitoa ahadi ya sukari kuwa nafuu mpaka Ramadhani ikianza najiuliza maswali je wale Wasio Waislam ambao wameanza mfungo zaidi ya siku 15 walipaswa kuteseka na hali hii kununua kilo moja ya sukari 6000 kwanini kila anaeongelea sakata la sukari anasema ikifika Ramadhani kwahiyo Wakristo waliofunga je viongozi wetu kuweni makini kuipasua hii nchi sio Udini kukumbusha Bwana bashe kuwa unakosea pamoja na viongozi wenzako hii nchi sio ya watu wa upande mmoja
 
Solution ni kupiga marufuku dini za Ibrahim nchini, zimetuletea ujinga mwingi kuliko faida.

Sijawahi kuwasikia Buddha wala Hindu wakileta ulalamishi wa kuona wametengwa, wanaendesha mambo Yao Kwa ustaarabu wa Hali ya juu, kuna sikukuu Yao wengine inaitwa Ashura huwa wanaomba kibali kabisa cha kupiga mafataki.
Hapa mkuu umeteleza kidogo...

Kwenye Buddha na Hinduism hakuna Ashura Mkuu.

Hao unaowapinga wa "dini za Ibrahim" ndio wenye Ashura. Inakua ni siku ya 10 tangu kuanza mwaka mpya wa Kiislamu.

Ashura means 10th day.
 
Bashe ametoa ufafanuzi kuhusu kauli ya uhaba wa Sukari kumalizika kabla ya Mfungo wa Ramadhan

=====

Salaam Ndugu Zangu,

Ningependa kutoa ufafanuzi wa kauli yangu iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari wakati wa maswali na majibu kwenye mkutano na wahariri uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 22.02.2024.

Kama Waziri wa Kilimo, nilitoa maelezo juu ya hali ya upungufu wa Sukari nchini, na muda wa usambazaji tunaotarajia wa shehena inayofuata ya sukari.

Nilisisitiza kuwa kutokana na usambazaji huu na hatua tulizochukua, tutarajie hadi kufikia mwezi mtukufu wa Ramadhan hali itakua nzuri.

Rejeo hili lilikusudiwa kuwa kiashiria cha MUDA kwa madhumuni ya kimipango na sio kuashiria kipaumbele chochote cha KIDINI.

Mara kadhaa nimesisitiza kwa kutaja vipindi vyote viwili Kwaresma na Ramadhani vina tukabili hapo mbeleni na kuwa tunajitahidi kama Serikali na azma yetu ya kutaka kutatua hii changamoto kabla ya hivi vipindi kufika na ndio maana tulianza kutoa vibali tangu mwezi wa 12, 2023.

Tuendelee kushirikiana kuboresha sekta ya kilimo na usalama wa chakula nchini.
Ila utahusiana na Ramadhani.
 
Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha bidhaa muhimu zinapatikana wakati wote bila kutoa umuhimu wa mhula wo wote ule. Sera ya kuwaachia walimaji sukari kuwa na usemi kwenye uagizaji wa sukari pungufu ulitoa ushindani ukawahakishia walima sukari kupata faida kupitia bei wakati wote bila kujali tija katika usalishaji na usambazaji. Hili somo la ushindani hapa nchini lilianza mwanzoni mwa 2000s.Halijakolea kwa viongozi wengi. Huko nje mnakokwenda hamjifunzi uchumi wa soko unavyoendeshwa mnataka tuwe waathirika wa fikra za watu wachache?
 
yuko sahihi mkuu , waislamu wanafunga ili wafuturu , tofaut na wakristo kwanza hawaruhusiwi hata kujitangaza kama wamefunga
Nasikia hawa ndugu zetu huwa ratiba ya mchana imehamishiwa usiku.
 
Nawaomba serikali mjitokeze kutupa mrejesho kama sukari ni kwa ramadhani tu au kwaajili ya watu wote maana tunateseka kisa Ramadhani haijafika je Wakristo waliofunga inakuwaje
 
Bei ya sukari itastabilize kuanzia July baada ya bunge kuifanya sukari kuuzwa kwenye soko huria.
Vuta subra...
 
Back
Top Bottom