Wataalam wa sheria, hakuna uwezekano wa kwenda mahakamani kuishinikiza Serikali iruhusu uwepo wa mshindani wa TANESCO?

Rurakha

Senior Member
Oct 20, 2019
121
209
Habari za leo,

Natumaini mnaendelea vizuri na utekelezaji wa majukum ya kila siku.

Binafsi nimekuwa nikifuatilia utekelezaji wa shughuli za mahakama Nchini Kenya nimeona mamna ambavyo Mahakama ya Kenya imekuwa ikitoa mashinikizo mbali mbali kwa serikali kwa manufaa ya wananchi

Tukirudi hapa kwetu Tanzania kumekuwepo na tatizo la mgao wa UMEME ambao hauna sababu za kueleweka mara utasikia matengenezo kinga, mara miundombinu imeharibika, au ukame. Matatizo haya yamekuwepo kwa mda mrefu sana.

Binafsi nafikiri wanasheria wetu waende mahakamani kuishinikiza serikali na TANESCO waruhusu uwekezaji wa sekta Binafsi katika huduma hii muhimu kwa maslahi mapana ya Uchumi wetu ufanyike kwa haraka.

Uamuzi huo uzingatie kwamba serikali imefeli pakubwa katika Biashara na imekuwa ikitumia pesa nyingi sana bila matokeo ya kueleweka mfano angalia TBC na AZAM hizi taasisi mbili ukiangalia gharama za uendeshaji kuna uwezekano TBC anatumia pesa nyingi kuliko AZAM ila azam TV inafanya biashara ya utangazaji kwa ufanisi.

Mashirika mengine ambayo yapo yapo tu TRC, DART, TTCL, ni makampuni ambayo ukipitia Taarifa za fedha ni hasara tupu.
 
Kinadharia, njia rahisi kabisa ni bunge kufanya mabadiliko ya sheria kuondoa ukiritImba wa TANESCO.

Mahakama haitungi sheria. Mahakama inatoa hukumu kwa mujibu wa sheria zilizopo pamoja na kutafsiri sheria. Kama sheria inasema TANESCO ina monopoly, mahakama kubadili hilo ni vigumu, unless uingize masuala ya kwamba sheria hii ipo kinyume na vifungu vya katiba na hivyo ni batili.

Kiuhalisia, bunge hili kufanya tofauti na serikali inavyotaka ni ndoto.
 
Back
Top Bottom