Wasukuma na utamaduni wa kutakasa mapacha

Wasukuma na utamaduni wa kutakasa mapacha

Wanyantuzu sio Wasukuma, ni waamiaji tu na walicopy lugha ya Kisukuma ambayo wanaiongea kwa lafudhi tofauti na kisukuma asilia, pamoja na kukopi lugha pia walikopi baadhi ya mila na zingine waliziacha

Weka vyanzo...
 
We kweli kituko! Kama uko Dar nenda pale UDSM Library waambie wakupe dissertation ya Buluda Itandala. Inaelezea vizuri sana mchanganuo wa Wasukuma (wakiwemo Wanyantuzu), asili yao n.k. Tafuta pia maandiko ya Batibo kuhusu uhusiano wa lahaja ya Kinyantuzu na lugha jirani. Jisomee kwanza kabla ya kupanda jukwaani vinginevyo utaendelea kuonekana kituko.
 
Aisee, asante kwa kunifahamisha kuwa Wanyantuzu kuwa nao ni Wasukuma
 
Nimegundua wewe ni ki**laza,Bumera makao makuu ya kanadi ndio kwetu.KANADI SECONDARY ndio shule yangu ya O-level.Siwezi bishana na taahira anayebisha bila evidence.....Mkuu wangu wa shule wakati huo nilimwacha Mwl moja hivi anaitwa MUGUBE (wakati ule alikua ndi mpya)
Mi naishia hapa,endelea na utumwa wako wa USA BABY Msukuma fake wewe
Kwetu Ng'wabuki kata ya Bumera
 
We kweli kituko! Kama uko Dar nenda pale UDSM Library waambie wakupe dissertation ya Buluda Itandala. Inaelezea vizuri sana mchanganuo wa Wasukuma (wakiwemo Wanyantuzu), asili yao n.k. Tafuta pia maandiko ya Batibo kuhusu uhusiano wa lahaja ya Kinyantuzu na lugha jirani. Jisomee kwanza kabla ya kupanda jukwaani vinginevyo utaendelea kuonekana kituko.
Sijawahi kusikia Wanyambiti, wanyankanga, wanyageita, bali wote huwà wanaitwa Wasukuma tu, nashindwa kuelewa ikawaje hawa wa Ntuzu kuitwa Wanyantuzu?
 
Nenda makumbusho ya Bujora, utafahamu hata mengine ambayo huyajui! Siyo kuandika vitu vya kusadikika ambavyo huna ushahidi navyo.

Ntaenda kaka hapo Bujora, lakini hakuna Msukuma wa maeneo mengine anaekubali kuwa mnyantuzu kuwa ni Msukuma, bali huwa wanawaita Wanyantuzu tu kwa nini?
 
Wewe ndiyo Mnyantuzu feki na hizo simulizi zako za familia yako.

Na sitashangaa kama hayo matendo ni ya familia yenu tu. Si ya Wasukuma wote na kwa uhakika kabisa si ya Wasukuma kama mimi tuliotokea Kanadi na Ikungulyabashashi.

Eti unatokea Itilima....umehamia lini huko?
USA baby...
Huwezi kufiti kila sehemu kihivyo, utachekesha!
 
Ntuzu ni tabaka kama ilivyo kwa Nkamba na Nseya. Lakini Ntuzu ndiyo tabaka iliyokuwa imara katika kutunza tamaduni za kisukuma hadi leo. Nenda Bujora utajifunza mengi..
Daaaah mkuu umenikumbusha home kabsa,mimi ni mseya pale ikulu ya chief makwaya kidaha pale Ukenyenge negezi.sisi maeneo yetu ukizaa mapacha unachezwa ngoma inayoitwa bhukango,aiseee yaani nyama kwa wingi.
 
Naona BBC wanashida na watu wa huko maana walianza na mauji ya vikongwe, wakaja ndoa za utotoni na sasa hivi wamekuja na hii ya watoto mapacha!
haujuwi kuna reporter wao yuko huko anakusanya habari kwani wangejuaje yote hayo
 
Wanyantuzu sio Wasukuma, ni waamiaji tu na walicopy lugha ya Kisukuma ambayo wanaiongea kwa lafudhi tofauti na kisukuma asilia, pamoja na kukopi lugha pia walikopi baadhi ya mila na zingine waliziacha
waliami akutoka wapi mkuu maana naona unawafahamu sana
 
Babu yangu ni Pacha,Baba yangu amefuata mapacha na mimi tumezaliwa mapacha na mdogo wangu wa kike,mashangazi zangu na dada zangu wengi tu wana mapacha,hii sherehe nishafanyiwaga,tena ziko mbili...ile mkiwa vitoto vidogo mama yenu hawezi akaenda ugenini akalala nanyi huko,mpaka mfanyiwe tambiko kidogo,zinachinjwa kondoo kulingana na jinsia yenu (kama ni wa kiume,kondoo atakua wa dume,km sivyo basi kondoo watakua jike na dume) watu wanakula.Kuna ngozi kutoka kwa wale kondoo mnavalishwa kama pete (watoto na mama yenu).Tambiko hilo likiisha basi mnaruhusa ya kulala ugenini.
Pia mtu akijifungua mapacha, kiongozi wa jadi wa kanda (Lugoye) atapiga Kalulu ili kujulishwa wanazengo wote (hii kalulu inaashiriaga majanga au mkosi,mfano ikinyesha mvua ya mawe,mtu kuzaa mtoto mfu au mtu kufa akiwa anazaa huwa wanapiga kalulu pia) hii "kalulu" huwa inapigwa afu mpiga anatamka neno "Boyo" then anataja jina la familia.
Kuzaa mapacha ilikua kama mkosi flani hivi kama alivyosema mwandishi,watoto wa mapacha tulikua tunafichwa sana tulikua tunajulikana kama "Basebu" ikiwa na maana wa "moto" ikimaanisha mapacha wanaweza kufa muda wowote na huwa wanafanyiwa matambiko sana.Kama ulisoma kitabu cha Things Fall Apart,kwenye kabila la akina Okonkwo mapacha walikua wanaitwa "Osu" na walikua dalili ya mkosi katika jamii na walikua wanatupwa porini.
Zamani usukumani mwanamke anayezaa mapacha alikua anaachwa....Natokea Bariadi,wilaya mpya ya Itilima....kwenye ukoo wetu akina saka (mtoto pacha aliyebaki baada ya mwenzake kufa wakati wa kuzaliwa au kufa baada ya muda mchache ni wengi sana.
Majina haya kwetu ni common
1.Kulwa-Pacha wa kwanza kutoka (mkubwa)
2.Doto - pacha wa pili kutoka (mdogo)
3.Kija- mtoto wa kwanza(kiume) kufuata mapacha
4.Hoja-Mtoto wa pili(kiume) kufuata mapacha
*Saka ni mtoto mapacha ambaye mwenzake hayupo (ashakufa) Maana ya neno SAKA ni "BAKI" Kwa hiyo SAKA ni pacha aliyebaki baada ya mwenzake kufa.
Kwa hiyo Nyani Ngabu wewe ni msukuma fake umeongea uongo,mimi ni mshosha ng'ombe halisi,Msukuma grade A,Mnyantuzu pure kabisa na natoka familia ya mapacha kutoka babu yangu hadi mimi.

sio kija ni shija
 
Back
Top Bottom