Kituko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2009
- 9,555
- 9,368
Humu utapigwa mawe, watu wanashindwa kujua asili zaowaliami akutoka wapi mkuu maana naona unawafahamu sana
Humu utapigwa mawe, watu wanashindwa kujua asili zaowaliami akutoka wapi mkuu maana naona unawafahamu sana
Zile habari za mauaji ya vikongwe na watu wenye albinism Nazo ni za uongo ?Uongo ndiyo!
Wasukuma wanamatabaka mengi mno. Tukiorodhesha hapa yanafika mia.Kuna wengine watashangaa humu kama kuna hilo tabaka la Waseya kama ilivyo kwa Wanyantuzu na Wakamba.
Huwezi kuwa unaabudu miti au mizimu ukasema umestaarabika. Huo ndoo ukweli hata kama ni mchunguKugeukia Ukristo na Uislamu ndiyo KUSTAARABIKA? Waafrika yaani dah! Ikiwezekana kwa kweli wazungu warudi tu watutawale tena kwa sababu hakuna namna.
Usidanganye watu wewe, vitu Vingi umetumia nadhariaBabu yangu ni Pacha,Baba yangu amefuata mapacha na mimi tumezaliwa mapacha na mdogo wangu wa kike,mashangazi zangu na dada zangu wengi tu wana mapacha,hii sherehe nishafanyiwaga,tena ziko mbili...ile mkiwa vitoto vidogo mama yenu hawezi akaenda ugenini akalala nanyi huko,mpaka mfanyiwe tambiko kidogo,zinachinjwa kondoo kulingana na jinsia yenu (kama ni wa kiume,kondoo atakua wa dume,km sivyo basi kondoo watakua jike na dume) watu wanakula.Kuna ngozi kutoka kwa wale kondoo mnavalishwa kama pete (watoto na mama yenu).Tambiko hilo likiisha basi mnaruhusa ya kulala ugenini.
Pia mtu akijifungua mapacha, kiongozi wa jadi wa kanda (Lugoye) atapiga Kalulu ili kujulishwa wanazengo wote (hii kalulu inaashiriaga majanga au mkosi,mfano ikinyesha mvua ya mawe,mtu kuzaa mtoto mfu au mtu kufa akiwa anazaa huwa wanapiga kalulu pia) hii "kalulu" huwa inapigwa afu mpiga anatamka neno "Boyo" then anataja jina la familia.
Kuzaa mapacha ilikua kama mkosi flani hivi kama alivyosema mwandishi,watoto wa mapacha tulikua tunafichwa sana tulikua tunajulikana kama "Basebu" ikiwa na maana wa "moto" ikimaanisha mapacha wanaweza kufa muda wowote na huwa wanafanyiwa matambiko sana.Kama ulisoma kitabu cha Things Fall Apart,kwenye kabila la akina Okonkwo mapacha walikua wanaitwa "Osu" na walikua dalili ya mkosi katika jamii na walikua wanatupwa porini.
Zamani usukumani mwanamke anayezaa mapacha alikua anaachwa....Natokea Bariadi,wilaya mpya ya Itilima....kwenye ukoo wetu akina saka (mtoto pacha aliyebaki baada ya mwenzake kufa wakati wa kuzaliwa au kufa baada ya muda mchache ni wengi sana.
Majina haya kwetu ni common
1.Kulwa-Pacha wa kwanza kutoka (mkubwa)
2.Doto - pacha wa pili kutoka (mdogo)
3.Kija- mtoto wa kwanza(kiume) kufuata mapacha
4.Hoja-Mtoto wa pili(kiume) kufuata mapacha
*Saka ni mtoto mapacha ambaye mwenzake hayupo (ashakufa) Maana ya neno SAKA ni "BAKI" Kwa hiyo SAKA ni pacha aliyebaki baada ya mwenzake kufa.
Kwa hiyo Nyani Ngabu wewe ni msukuma fake umeongea uongo,mimi ni mshosha ng'ombe halisi,Msukuma grade A,Mnyantuzu pure kabisa na natoka familia ya mapacha kutoka babu yangu hadi mimi.
Ujuaji wa JF kivipi?, wewe ndio unajiona ndio msukuma samahani Mnyantuzu wa mwisho kabisa hakuna zaidi yako?Nimekuuliza ulishasikia wasukuma wanasalimiana "enkamba" au "iseya"? Unakuta hata siyo msukuma, kumbe ni ujuaji wa JF tu.
Hiyo kusalimiana naamini unajua inaitwa Lwèmbo na ukifuatilia hizi lwèmbo zinatumia majina ya wanawake, Majina haya ni wake wa watemi wa utemi fulani, mfano kama mke wa mtemi wa Ntuzu alikuwa anaitwa Minza basi watu wote waliotoka utemi wa Ntuzu watakuwa babinza na watakuwa wanasalimia éminza.Hivi una miaka mingapi wewe? Kuna Wakamba huwa wanasalimiana "enkamba" na kuna Waiseya huwa wanasalimiana "iseya" kama kutambulisha tabaka walipotoka. Hukuwahi kusikia hizi salamu?
Sahihisho :mtoto aliyezaliwa katanguliza miguu hatuiti mabasa ila huitwa "Kashinje "Kwa Wasukuma wa jamii ya Wanyantuzu hizi mila hazipo, ila kwa Wasukuma ambao wanyantuzu huwaitwa Banang'weli huo utamaduni wanao, tena kwao neno mabasa haimanishi tu mapacha kwa maana ya kujifungua watoto wawili kwa mimba moja, wao humanisha kama mkosi. Hii ni kwa sababu wao wana mabasa ya aina mbili, Mama akijifungua watoto wawili huita mabasa na hufanya tambiko, mtoto akitanguliza miguu pia huita mabasa tena wanasema ni mabasa matale na wanafanya tambiko.
Na hayo yametokana na kuwa kuna Makabila ambayo hayakuwa Wasukuma ila wameingia ndani ya Usukuma kwa kuitumia lugha ya kisukuma na kuchukua baadhi ya mila za KisukumaWasukuma wanamatabaka mengi mno. Tukiorodhesha hapa yanafika mia.
Wanyantuzu cyo wasukuma halisi ni mchanganyiko wa wasukuma na wanyiramba.Na hayo yametokana na kuwa kuna Makabila ambayo hayakuwa Wasukuma ila wameingia ndani ya Usukuma kwa kuitumia lugha ya kisukuma na kuchukua baadhi ya mila za Kisukuma
Ndugu upo sahihi kabisa. Kuna watu wanajifanya wanajua sana issue za kisukuma kwa kutumia nadharia bila kufanya uchunguziUsidanganye watu wewe, vitu Vingi umetumia nadharia
Kwa mfano
1.ngoma wanayochezewa Mapacha inaitwa "MABASANA"
2.Katika utamaduni Wa kisukuma Hakuna jina SAKA ila aliyefiwa na pacha wake tunamwita "MASAGA"au"SAGA" kwa kifupi.
3."KALULU"ni vigelegele hasa vya Furaha wapigavyo kina mama kwenye matukio Mhimu Kama vile arusi, posa
4.BHOYO ni mjumuiko Wa ubalozi au mtaa ambapo msiba umetokea.
NAKARIBISHA. MASWALI!!!!!!
Unajua kuwa mpaka leo kuna Wajapan na watu wengi tu waliostaarabika (per your standard) wanaabudu miti na mizimu?. Na wakitoka hapo wanakwenda kukutengenezea Sony Music System na Toyota Land Cruiser. Kwako wewe ustaarabu ni nini?Huwezi kuwa unaabudu miti au mizimu ukasema umestaarabika. Huo ndoo ukweli hata kama ni mchungu
Sio jina lake, ile hali ya kutanguliza miguu ndo mabasa yenyewe. Narudia tena sikumaanisha kwamba jina lake ni mabasa ila mabasa ni kile kitendo cha kutanguliza miguu.Sahihisho :mtoto aliyezaliwa katanguliza miguu hatuiti mabasa ila huitwa "Kashinje "
Karibu Kwa maswali
Yaan mtu anaibuka na nadharia zake ili aonekane bingwa kumbe hamna kituNdugu upo sahihi kabisa. Kuna watu wanajifanya wanajua sana issue za kisukuma kwa kutumia nadharia bila kufanya uchunguzi
Tuwekee hiyo orodha kwa uwezo wako kama unaijua, plsWasukuma wanamatabaka mengi mno. Tukiorodhesha hapa yanafika mia.