Wasukuma acheni kuongea kilugha mkiwa mjini

Wasukuma acheni kuongea kilugha mkiwa mjini

Lugha ni njia kuu ya mawasiliano na kupata elimu na ujuzi mpya wa maisha. Unapojichanganya na jamii zingine na wewe ukaendelea kung'ang'ana ya lugha yako ya asili unakosa kupata au kujifunza mambo mapya kutoka kwa jamii mpya unayokutana nayo. Jambo hili limefanya hawa wenzangu wasukuma kurudi nyuma kimaendeleo au kuendeleza makosa ambayo wameyafanya huko kwao walikotoka. Mfano mikoa ya Kigoma na Katavi wameingia wasukuma wengi na wanapenda sana kuongea lugha yao hata huko ugenini, hivyo hawajifunzi. Matokeo yake wameendeleza makosa yale yale ya kufyeka misitu na kuharibu vyanzo vya maji kama walivyofanya huko kwao walikokimbia.. Si hiyo tuu hata kuendekeza ufugaji wa kizamani wa kuwa na mifugo mingi.
Kwani walikwambia hawajui lugha nyingine yoyote zaidi ya kisukuma? Kujua lugha nyingi kuna raha yake na ongea lugha uliyoizoea, sio ujifanye kuongea kiswahili huku hukijui, sio ujifanye kuongea kiingereza huku hukijui sio ujifanye kuongea kisukuma huku hukijui vizuri utaboa sana.
 
Jana nilijieziwa kibao ddm pale kwa kuitwa mm Ni mkabila
 
Leo nilienda kupungwa upepo coco, ila nilichokutana nacho kwa hawa ndugu zetu wasukuma kimenishangaza!

Vijana wanaongea kilugha tu mwanzo mwisho(kisukuma) kama vile wapo usukumani!

Acheni ushamba bana, tumieni kiswahili mnapokuwa mjini. Hawana hata aibu wanaongea kwa sauti kubwa kila mtu anawashangaa wao! Mnakera kiukweli.
Wao ndo wanakushangaa wewe kutokujua kisukuma, chezea ngosha nini.......
 
Labda kama we ni mtani wao so huu uzi umeuleta kuwatania ntakuelewa ila kama uke serious kwamba umeshangazwa na hii issue basi we ndo mshamba na limbukeni.
 
Sensa ya Mwaka huu inaonesha kabila lenye watu wengi ni Wasukuma na wapili kwa idadi ni waha nadhani sababu makabila hayo hawana uzazi wa mpango
Bhebhe!!

Kwani Sensa ya mwaka huu, walikuwa wanauliza na Kabila?
 
Sasa mtu alieamua kuongea lugha yake ww inakuuma nini?
 
Bora hata hao walikuwa eneo la wazi...

Hujakutana na wamaasai kwenye daladala, mmoja mbele na mwingine nyuma kabisa wakibonga kilugha chao kwa sauti kubwa...

Anyway, kuongea kilugha sio ushamba maana ile ni lugha kama zilivgo lugha nyingine zozote kama Kiswahili, Kiingereza n.k
Kiswahili ni lugha ya taifa, Kiingereza ni lugha ya kimataifa, kisukuma ni lugha ya kabila ambayo huwa inatumika sana kule usukumani, hakuna mtanzania yoyote anae katazwa kuongea lugha yakabila lake akiwa shehemu yoyote au mkoa wowote, ni busara tuu huwa inatumika

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Leo nilienda kupungwa upepo coco, ila nilichokutana nacho kwa hawa ndugu zetu wasukuma kimenishangaza!

Vijana wanaongea kilugha tu mwanzo mwisho(kisukuma) kama vile wapo usukumani!

Acheni ushamba bana, tumieni kiswahili mnapokuwa mjini. Hawana hata aibu wanaongea kwa sauti kubwa kila mtu anawashangaa wao! Mnakera kiukweli.
Hii ni lugha adhimu ya taifa.
 
Leo nilienda kupunga upepo coco, ila nilichokutana nacho kwa hawa ndugu zetu wasukuma kimenishangaza!

Vijana wanaongea kilugha tu mwanzo mwisho(kisukuma) kama vile wapo usukumani!

Acheni ushamba bana, tumieni kiswahili mnapokuwa mjini. Hawana hata aibu wanaongea kwa sauti kubwa kila mtu anawashangaa wao! Mnakera kiukweli.
Tulekaghee shii!.. Twekenekeee!..kwani Wa hadikejagwa kotodegeleka!.. Kwan nse ya ng'wamamayo ?
 
Duh,kwani wasukuma pekee ndiyo wanaongea kilugha mjini

Ova
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom