Wassira: Warioba alinikimbiza CCM mwaka 1995

Wassira: Warioba alinikimbiza CCM mwaka 1995

Kesi yake ilisikilizwa na Jaji Mwaikasu(RIP) wa Dodoma ambaye alikuwa mmoja kati ya majaji bora kabisa kupata kutokea ktk nchi hii!

Naikumbuka kesi hii,Wasira alipatikana na hatia ya rushwa ya vyakula na mapombe kwa wapiga kura wake walio kuja Mahakamani kutoa ushahidi(Kipindi hicho takrima ilikuwa inachukuliwa kama rushwa mbaya sana)

Jaji Mwaikasu asinge mpendelea mtu yyt kwa wale tulio kuwa tunajua uweledi wake!Aache visingizio
Huyo atakuwa shujaa Mwalusanya.
 
mkuu kama ni Mwaikasu basi sina shaka haki ilipatikana na ilitendeka. Mwaikasu J, Mwalusany J na Lugakingira J walikuwa ni majaji mahiri na ambao ukisoma hukumu zao hupati shaka yoyote.
 
Huyo atakuwa shujaa Mwalusanya.

Mmoja kati ya wanasheria walio nisukuma kuingia ktk fani ya sheria!Jaji Mwaikasu,Jaji Mwalusanya,Jaji Lugakingira,Jaji Nasoro Mzavas,Jaji Francis Nyalali

Huwa hadi leo napenda kusoma muhtasari wa kesi zao hawa mabingwa!Acha kabisa hawa majaji walijua kuandika hukumu zao jamani!Kiingereza simple na kimenyoka

Sio siku hizi ukiwa rafiki wa JK unapata ujaji
 
Wewe Mwanasheria wa Mahakama gani?
Au umejiajiri.
 
Ukiacha mambo mengine mengine, Wasira ni mmoja wa watu wenye akili na weledi wa hali ya juu sana. Ana uwezo wa kujenga au kupangua hoja kwa kiwango cha juu. Nadhani ndio maana JK kamng'ang'ania kipindi chote cha miaka 10 licha ya umri wake. Akili yake inakata kama wembe. Wakati wa sekeseke la minofu ya samaki iliyomng'oa Profesa Mbilinyi, Wasira alikuwa moto wa kuotea mbali. Alilichangamsha Bunge kwa hoja murua. Sijui wakirejea CCM wanafanywa nini hadi kupoteza weledi wao.
Angalizo: Maelezo haya hayana uhusiano wowote na nia yake ya kutaka awe Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa letu.
jk kamng'ang'ania wasira kwasaba ni mtu wa ndiyo mzee. kwenye vikao vya chama alisema hawezi mpinga rais sababu ni rais wake. pia hana weledi wowote. kwenye escrow badala ya kutoa hoja akawa anasema eti kuna mtu anapesa na anataka urais ndiyo anawavuruga! kitendo cha kupiga waandishi ni kukosa weledi.
 
Naaaamm, Dada leo hujapost na kuandama dini fulani na kusapot vikundi vya kigaidi.
Nimekuja huku mbio nikijua kuna thread ya ugomvi wa kidini....naaam asante kwa maelezo marefu.
My advice! Focus kwenye dini achana na mambo ya kisiasa. Hao uliowataja waache ni makafiri pia.

Naona unahororoja na kubwabwaja bila mpango, umeshalewa?
 
ilikuawe wassira alionekana ametoa rushwa kiasi cha kuzuiwa kugombea kwa miaka mitano?

Jamani, Mahakama ndiyo iliyoona hilo jambo. Maswali mengine nadhani yaishie tu hapo. Tukichimbia makaburi si CCM wala Upinzani atakayebaki salama. Unaweza kuliliwa kwamba wewe unashiriki kuwakosesha watu kuingia Magogoni.
 
Wewe na FF mnautaka ukurugenzi ndo maana mnampigania huyu AJUZA.

Yamekuwa hayo tena!! Ukumbuke kuwa sisi wengine haya mambo tunayajua kwa sababu tunaipenda historia. Ninyi vijana wa leo mkiganda kwenye FB, Bongo Fleva, Bongo Movie na sinema za Nigeria weledi wenu unakomea hapo hapo. Wale wa enzi zetu tulifuatilia vema mambo na ndiyo maana utaona wachangiaji wanatiririka tu.
 
Mwaka 1996 niliripoti kesi ya Warioba Vs Wasira. Ilifanyika Mjini Musoma. Wakati huo Mutungi (huyu wa Usajili wa vyama) alikuwa Hakimu Mkoa wa Mara. Kesi ilisikilizwa na Jaji Kahwa Lugakingira. Mawakili wa Wasira walikuwa Malamsha, Mwambegele (sasa ni Jaji), na Mabere Marando. Warioba aliwakilishwa na Josephar Rweyemamu na Profesa Jwan Mwaikusa (marehemu). Kesi ilikuwa tamu sana sana. Ushahidi ulikuwa na mvuto wa aina yake.
Nakumbuka Mabere alimwuliza Warioba, "Hivi wewe Warioba umeoa?" Halafu akamwambia, "Wewe umeshakuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na tena Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, unajua ukiongea uongo hapa mahakamani utafungwa?"
Baadhi ya mashahidi wa Wasira ni kama Kicharwi Chacha Henche, Gamitwe, Museveni nk. Hizo notebook za kesi nzima ninazo hadi leo. Lakini tukio moja nalikumbuka, tukiwa karibu na Mkendo Guest House (nje kuliuzwa vinywaji na vyakula), jioni; Wasira akaniona. Akanifuata akiwa amewaka kweli kweli. Akataka akiidake anizabe kibao, bahati nzuri nami nilikuwa 'mzima'. Nikasimama kando. Marando akaingilia kati kuzuia. Wasira akawa amewaka kweli kweli akidai nilikuwa nikiripoti kwa kumpendelea Warioba. Marando akajaribu kumweleza kwamba kwenye ile kesi hatua za awali hapakuwa na namna ya kuripoti zaidi ya vile nilivyofanya.
Nikadhani yameisha, Kesho yake mawakili wa Wasira wakawasilisha hoja kwa Jaji Lugakingira nizuiwe kuripoti. Jaji akawaomba ushahidi wa distortion, wakawa hawana. Jaji akaamuri niendelee na kazi. Kesi hiyo ilikuwa na mvuto wa aina yake kwa kweli.

Mkuu nakumbuka swali aliloulizwa Warioba na wakili wa Wasira. Nilcheka sana. Aliulizwa hivi: Wakili: Hivi ilikuwaje Rais akakuteua wewe kuwa Waziri Mkuu kama siyo umjomba uliotumika?' Jaji Warioba: Kimya.......
 
Asante kwa Flashback ... ila mzee Wassira apumzike umri umeshasogea.
 
Nilichojifunza ni kwamba.
Kwanza, ndani ya ccm kuanzia mashinani mpaka ngazi ya taifa hakuna haki.

Pili,matumizi ya rushwa kwenye chaguzi ndani ya ccm hayajaanza Leo.ni ya muda mrefu sana na yawezekana sasa yamekithiri.

Tatu,viongozi ndani ya ccm wako katika chama hicho kwa maslahi ya kiuchumi.ni watu wasioweza kuendesha maisha yao wakiwa nje ya mfumo Wa chama hicho.
Duuu ndg we unasema issue za rushwa ndani Ya chama hiki ni donda sugu mid 90s nikiwa bording school nakumbuka hata sikuwa na idea na issue za siasa makada walikuwa waki organise vikundi vya wanafunzi wenzetu enzi hizo wakigawa sukari na pesa nakumbuka Land Rover zikishusha magunia Ya sukari shuleni mid night ndo maana kazi Ya kung'oa kizazi kisicho na rushwa ni ngumu sana kwani watawala wameifanya kama syllabus kwa muda mrefu sana
 
Warioba ni janga:

Hili ni hitimisho lako, kwa sababu umeamua kwa makusudi ukifahamu hiyo ni habari ya upande mmoja, na hilo ndilo unapenda kusikia. Eti Warioba ni janga! Hivi kuna kesi iliyowahi kuwa kivutio zaidi Musoma zaidi ya hii ya Warioba na Wasira? akitoa fact Warioba zenyeuthibitisho ambazo zinaishawishi mahakama ulitaka mahakama ifanyeje? , basi tutangaze leo kuwa majaji wasiwe wanashitakiwa sababu ni kesi ya nyani. Halafu mbona haongelei uchaguzi mdogo wa 1998 jimbo la Bunda kama kweli alikuwa anaipenda CCM mbona alikuwa anampigia debe Victor Kubini?, sababu mwaka huo mgombea wa Ccm alikuwepo Canal Laban T Makunenge(Rip) ambaye aliibuka mshindi mwingine akiwa Makongoro Nyerere kuipenda ccm kunatoka wapi?. guys don't be easily moved by a one side story.
 
Warioba ni janga...

Trueman, huyo faizaFozy msikie tu. Kilichomkimbiza kuanzisha hii mada ni kumkomoa Jaji Warioba kwa tuhuma kwamba alishinda hiyo kesi kwa kutumia rushwa. Bahati mbaya JF kwa sasa imejaa watoto waliozaliwa kwenye ufisadi, wakalelewa katika ufisadi, wakakua ndani ya ufisadi na sasa ufisadi kwao ni neno la kawaida tu na mtu anaweza kuthubutu hata kujivunia.

FaizaFoxy anaelewa sana weledi wa Jaji Warioba na kwamba kwenye kipimo cha weledi huwezi kumweka kwenye mizani sawa na Steven Wassira, Tyson. Kinachomharibia Warioba ni msimamo wake usioyumba katika mchakato wa kupata Katiba mpya. Mwishoni mwa mwaka jana, Jaji Warioba alitamka bila kusita kuwa kura ya maoni haingewezekana katika muda uliopangwa.

Katika watu waliotoa matamko wakimpinga mojawapo alikuwa ni Steven Wassira lakini kama asemavyo FaizaFoxy, Mungu si athumani, kura ya maoni sasa ni ndoto. Kwa CCM kuna njia mbili za kumshughulikia mtu kama Warioba...ama kumshushia hadhi kwa kumchafua au kumuinua mbaya wake ili aonekane na yeye yumo. FaizaFoxy amechagua njia zote mbili.

Jaji Lugakingira (Luga) aliyesikiliza kesi hii na kutoa hukumu hii alikuwa moja katika mashujaa wa taifa hili waliokataa kununulika hata pale serikali ilipolazimisha. Kulinganisha mtu aliyeutafuta ubunge kwa udi na uvumba hadi kukisaliti chama chake na kumwaga rushwa hadharani na Waziri Mkuu mstaafu ni kukosa adabu. Lengo? Kumchafua aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Katiba.

Si mara ya kwanza watu kuchafuliwa ndani ya CCM, si mara ya kwanza rushwa kutumika ndani ya CCM na si mara ya kwanza watu wasiokubali kununulika kunyamazishwa ndani ya CCM. Msururu ni mrefu wa walioshughulikiwa ndani ya CCM kwa sababu tu ya misimamo yao isoyumba. Kwa FaizaFoxy nasema, kilimia kikizama kwa jua huzuka kwa mvua, kikizama kwa mvua huzuka kwa jua...tafakari.
 
Warioba hana uweledi wa kumfikia hata nusu ya Wassira, hilo kumbuka. Vyeo vyake vilikuwa vya undugunaizeshen tu, hakuna zaidi.
 
Warioba hana ueledi wa kumfikia hata nusu ya Wassira, hilo kumbuka. Vyeo vyake vilikuwa vya undugunaizeshen tu, hakuna zaidi.
Hii mpya, sikujua Warioba na Kikwete wanao undugu wa karibu hivyo...kisebusebu na roho kipapo!

Hii mpya, sikujua Warioba na Kikwete wanao undugu wa karibu hivyo...kisebusebu na roho kipapo!

Soma post namba moja. Au nikukumbushe?

"Nataka mwelewe kwamba mimi sikwenda upinzani kwa sababu nilikuwa napingana na sera za CCM. Kwanza 1985 nilikuwa mbunge na ndiyo maana Rais Ali Hassan Mwinyi aliniteua kuwa waziri wa kilimo," "Mwaka 1990 niliacha kugombea kwa kumwachia Jaji Warioba. Kwa sababu kama utakumbuka mwaka 1985 Warioba alikuwa ameteuliwa kuwa mbunge na waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais."
 
Back
Top Bottom