Wassira: Warioba alinikimbiza CCM mwaka 1995

Wassira: Warioba alinikimbiza CCM mwaka 1995

Soma post namba moja. Au nikukumbushe?

“Nataka mwelewe kwamba mimi sikwenda upinzani kwa sababu nilikuwa napingana na sera za CCM. Kwanza 1985 nilikuwa mbunge na ndiyo maana Rais Ali Hassan Mwinyi aliniteua kuwa waziri wa kilimo,” “Mwaka 1990 niliacha kugombea kwa kumwachia Jaji Warioba. Kwa sababu kama utakumbuka mwaka 1985 Warioba alikuwa ameteuliwa kuwa mbunge na waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais.”
Mbona unafoka wewe ajuza mbele ya wanaume? Au ni kawaida kwa wanawake wa Pwani? Kwetu si kawaida kabisa kwani mpemba akipata gogo hanyii chini. Kwa ufahamisho ngoja na mimi nikurudishe nyuma mwezi wa Aprili mwaka 2012 Raisi Kikwete alipomteua Jaji Joseph Sinde Warioba kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba. Ndio hapo nikauliza toka lini wamekuwa ndugu kihivyo?
 
Siku Wasira anamchapa Sadik pale Maelezo, nilikuwapo. Tulichoshuhudia ni Wasira akiwa ameshamlamba vibao. Mara moja akaenda nje na kuendelea na safari yake. Wakati wa kesi Wasira alimuomba Sadik wayamalize nje ya Mahakama, lakini kuna taarifa kuwa Sadik aligoma akitaka Mahakama imalize kazi. Siku ya hukumu, Wasira akashinda!! Sidhani kama Sadik alikuwa na hamu ya kukata rufaa.
Mkuu Kamanda Comredi Manyerere Jackton, asante kwa hii. Masikini Sadik, mtu upigwe magumi bila kosa lolote, tena kwenye kadamnasi ya watu, kisha aliyetenda kosa hilo la wazi akutwe hana hatia!. Ama kweli ndio maana mbobezi wa sheria wa Uingereza, Lord Denning aliwahi kusema hivi "Justice must not only be done, but must be seen to have been done!", yaani haki sio tuu ni lazima itendeke, bali lazima pia ionekane kuwa haki imetendeka!. Hapa kwenye hili kiukweli kabisa haki haikutendeka, na haikuonekana kutendeka, ila ila ile hukumu ya haki kabisa duniani hukumu ya 'karma' ndio itakatoa haki kwa Sadik na Wasira!.

Pasco
 
Baba yako alisalimika baada ya ile kesi?! Nakumbuka RSO wa Shinyanga alifungwa miaka 7.
Mkuu Gagnija, kiukweli kesi hiyo ilinitesa sana na kuni affect mno kwa sababu ilichukuwa muda mrefu sana, mimi nikiwa primary, baba ana muder case huku hukumu ni kunyongwa mpaka kufa!. He was innocent and thank God, he was the one and only aliyesalimika. Alikuwa akitetewa na Wakili Murtaza Lakha.From then niliipenda sheria, nikaja kuishia kuwa journalist, lakini bado nikaosoma tuu sheria just for the love of it, lakini nendelea ku practice journalism and not law!.

Enzi hizo Mwanasheria Mkuu alikuwa Joseph Sinde Warioba, DPP aliwa William Sekule, mwendesha mashitaka alikuwa Kulwa Satto Massaba, kesi ilisikilizwa na Jaji Kiongozi Nassor Mzavas!.

Kamanda mimi niliamua kuwa journalist kwa sababu tu sikupenda polisi walivyokuwa wakinyanyasa watu. Nikiwa darasa la nne polisi walininyang'anya boots zangu za scout na wakaniweka ndani. Tangu siku hiyo nikaapa nitakuwa mwandishi ili niwe natetea wanaoonewa kwa kuwaandika.
 
Mkuu Nicholas, no nilikuwa namaanisha contents, hili bandiko la FaizaFoxy, lilihitaji watu wenye level fulani ya upeo wa uelewa kulichangia, ndio maana nimeshangaa wewe unachangia humu kwa upeo upi wakati level yako humu inaeleweka?!. Pasco
kwa upeo huo huo unaoleweka
 
Ukiacha mambo mengine mengine, Wasira ni mmoja wa watu wenye akili na weledi wa hali ya juu sana. Ana uwezo wa kujenga au kupangua hoja kwa kiwango cha juu. Nadhani ndio maana JK kamng'ang'ania kipindi chote cha miaka 10 licha ya umri wake. Akili yake inakata kama wembe. Wakati wa sekeseke la minofu ya samaki iliyomng'oa Profesa Mbilinyi, Wasira alikuwa moto wa kuotea mbali. Alilichangamsha Bunge kwa hoja murua. Sijui wakirejea CCM wanafanywa nini hadi kupoteza weledi wao. Angalizo: Maelezo haya hayana uhusiano wowote na nia yake ya kutaka awe Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa letu.
Pengine usichojua ni kwamba usipokuwa makini sana,ni ngumu sana kupima lunatics au sadists...wassira,zitto na wengine wanaweza tumia neno au jibu lolote kujibu chochote ila si kweli hayo majibu yanahusiana na sababu ya wao kufanya hicho kitu...ndio maan wehu wa hii nchi upo juu sana..Watau wanatenda ndio wanafikiria sababu za kufanya,hawaanzi na sababu...
 
upinzani kwa hawa kinambowe waroppkaji upinzani tz bado sana
hizo kauli ziliwadanganya sana watz ila sasa hivi imekula kwenu..watz wanajua hii mibunge yenu ilivyopwaya..sasa leo mtadai vipi kuwa inaweza urais kuliko ubunge?
 
sasa hawa journalist mbona hawajui kilichowapelekea kuwa journalists...kwaniw ao kunewa na polisi,au mahakama au kesi za kisiasa..kuna tofauti gani na Injustices hizo hizo kufanyiwa vyama vya upinzani..sasa mlisoma ili mkajilinde pekee yenu?mbona haitokuwa worth it yaani uosme miaka yote ili kufnaya kazi ambyo ukishajikombea ndio huna tena kazi unayoipenda na kuona umuhimu wake?So now Pasco na Manyerere Jackton hawana tena kazi wanayoipenda wala kuichukulia serious...Naweza pata picture kwanini mnafanya kazi wa waovu wanaofanya uovu ambao ndio uliochangia mkachagua njia iliyowafikisha ktk kazi mnazofanya.
 
So now Pasco na Manyerere Jackton hawana tena kazi wanayoipenda wala kuichukulia serious...Naweza pata picture kwanini mnafanya kazi wa waovu wanaofanya uovu ambao ndio uliochangia mkachagua njia iliyowafikisha ktk kazi mnazofanya.
nahisi uwezo wangu kuelewa umeshuka!.
Pasco
 
Warioba ni janga:

Waziri Wasira alisema baada ya kupata kadi na uteuzi wa kuwa mgombea ubunge Jimbo la Bunda kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, walirudi Bunda na aligombea na kumshinda Jaji Warioba.
“Tukaenda tukagombea ubunge tukamshinda Warioba. Nikawa mbunge na bwana Warioba akakimbilia mahakamani. Warioba ni jaji, sasa kesi ya tumbili unampelekea nyani sina hakika sana kama nitashinda. Siwezi kusema zaidi ya hapo.”
​

EBU NIELEWESHENI, hiyo 1995 Warioba alishakuwa jaji?
 
Mama ungeweka na majibu ya warioba baada hizo tuhuma za uongo.. mwananchi toleo lilofuatia Warioba alijibu kila kitu na kumuumbua mzee wa fiksi...
 
Mama ungeweka na majibu ya warioba baada hizo tuhuma za uongo.. mwananchi toleo lilofuatia Warioba alijibu kila kitu na kumuumbua mzee wa fiksi...

Kwanini usiweke wewe? ndiyo raha ya mjadala, mimi nimeweka ya Wassira wewe weka ya Warioba.
 
Warioba hana uweledi wa kumfikia hata nusu ya Wassira, hilo kumbuka. Vyeo vyake vilikuwa vya undugunaizeshen tu, hakuna zaidi.

Bibi katika ubora wako hivi hawa wazee wa nchi hii walikukosea nini
Weka wazi tujue maana naweza nkawa na pingana na mawazo yako kumbe upo sahihi
 
Bibi katika ubora wako hivi hawa wazee wa nchi hii walikukosea nini
Weka wazi tujue maana naweza nkawa na pingana na mawazo yako kumbe upo sahihi

Hawakujuwa kuweka misingi bora ya kuiendesha nchi walipopewa dhamana ya kuijenga hii nchi, fikiri miaka yote ya Nyerere madarakani life expectancy ya Mtanzania haijafika miaka 45.

Nyerere anaondoka sisi ni masikini wa mwisho duniani.

Na hawa kina Warioba ndiyo waliokuwa watendaji, wakati wa Mwinyi huyu alikuwa Waziri Mkuu hakuweza kufanya au kubadili lolote. Hajaishia hapo, Mkapa anaondoka maradakani Tanzania bado tupo kwenye tano hoi za umasikini duniani.

Leo eti anataka kuaminisha watu kuwa ule ujinga wake mwenyewe alioujaza kwenye mapendekezo ya katiba ndiyo bora.

tena nililaumu sana Kikwete alipompa huyu mzee ile kazi, nilisema hivi huyu alifanya nini alipokuwa na wadhifa Tanzania hii hata leo aweze kukusanya maoni vyema? sikupata jibu lenye maana, watu wakaishia kuhororoja na kubwabwaja bila mpango.

Kama si kunikosea huko ni nini? wewe hayakuumizi hayo?
 
Brother, kwani Wasira hautaki urais? Anautaka. Je, hujui anayepata urais ndiye anayekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?
Kwasasa jina la Wasira liko juu sana, anakubalika sana Ndani ya Chama chake.
Kama hesabu zikipigwa vizuri mwezi Oktoba huyu Mzee anaweza kuwa Rais.
Kasi yake sio ya kubezwa hata kidogo.
Nimependa Mtiririko wa simulizi yako kwenye Uzi huu.
 
Yasin alimshitaki na kesi iliunguruma kwa muda mrefu ila sijui iliishaje!. Zile bahasha ni bahasha za uwezeshaji, waandishi wote duniani lazima wawezeshwe ili waweze!. Hata waandishi wanaosafiri na Obama kwenye Airforce One, nao pia huwezeshwa!.

Wewe unaonekana ni type ya wale ambao kwa vile mke ameolewa kwa kulipiwa mahari, hata akitandikwa makofi kwa kuzidisha tuu chumvi kwenye mboga!.

Pasco.
Pasco umekuwa mtu unaeheshimika sana hapa jukwaani na watu wote. Hii ni kwasababu una nondo za mambo mengi tena magumu.
Binafsi niko positive kumtakia Kheri Bwana Tyson Ushindani mwema huko CC
 
Yasin alimshitaki na kesi iliunguruma kwa muda mrefu ila sijui iliishaje!. Zile bahasha ni bahasha za uwezeshaji, waandishi wote duniani lazima wawezeshwe ili waweze!. Hata waandishi wanaosafiri na Obama kwenye Airforce One, nao pia huwezeshwa!.

Wewe unaonekana ni type ya wale ambao kwa vile mke ameolewa kwa kulipiwa mahari, hata akitandikwa makofi kwa kuzidisha tuu chumvi kwenye mboga!.

Pasco.
Pasco umekuwa mtu unaeheshimika sana hapa jukwaani na watu wote. Hii ni kwasababu una nondo za mambo mengi tena magumu.
Binafsi niko positive kumtakia Kheri Bwana Tyson Ushindani mwema huko CCM.
Akiibuka kidedea unapaswa uwe miongoni mwa Washauri wake.
 
Back
Top Bottom