Wassira: Warioba alinikimbiza CCM mwaka 1995

Wassira: Warioba alinikimbiza CCM mwaka 1995

Ukiacha mambo mengine mengine, Wasira ni mmoja wa watu wenye akili na weledi wa hali ya juu sana. Ana uwezo wa kujenga au kupangua hoja kwa kiwango cha juu. Nadhani ndio maana JK kamng'ang'ania kipindi chote cha miaka 10 licha ya umri wake. Akili yake inakata kama wembe. Wakati wa sekeseke la minofu ya samaki iliyomng'oa Profesa Mbilinyi, Wasira alikuwa moto wa kuotea mbali. Alilichangamsha Bunge kwa hoja murua. Sijui wakirejea CCM wanafanywa nini hadi kupoteza weledi wao.
Angalizo: Maelezo haya hayana uhusiano wowote na nia yake ya kutaka awe Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa letu.

Kaka Manyerere Jackton, huu ndo wakati wenu. Imba mapambio yote.
 
Last edited by a moderator:
Manyerere Jackton anasema:

Tumuamini nani?
Kwa uelewo wangu Mara HAKUKUWA na kanda ya Mahakama Kuu kipindi hicho na Jaji Lugakingira RIP alikuwa kanda Mahakama ya Dodoma na kesi maarufu iliyo mpa credit ni ile ya Mtikila na wagombea binafsi

Anyway miaka mingi imepita Manyerere anaweza akawa yupo correct
 
Last edited by a moderator:
Ukiacha mambo mengine mengine, Wasira ni mmoja wa watu wenye akili na weledi wa hali ya juu sana. Ana uwezo wa kujenga au kupangua hoja kwa kiwango cha juu. Nadhani ndio maana JK kamng'ang'ania kipindi chote cha miaka 10 licha ya umri wake. Akili yake inakata kama wembe. Wakati wa sekeseke la minofu ya samaki iliyomng'oa Profesa Mbilinyi, Wasira alikuwa moto wa kuotea mbali. Alilichangamsha Bunge kwa hoja murua. Sijui wakirejea CCM wanafanywa nini hadi kupoteza weledi wao.
Angalizo: Maelezo haya hayana uhusiano wowote na nia yake ya kutaka awe Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa letu.



amiri jeshi mkuu ?manyerere kuwa makini wakati mwingine
 
Ina maana kwa sasa CCM imejipanga kuondoa mizengwe kwenye uteuzi na kutokufanya makosa?
Kama ni ndio tunasubiria kuona kuanzia ngazi ya Uraisi maana kama hawajajipanga kulingana na Wassira, nchi itaenda Upinzani.
 
Ina maana kwa sasa CCM imejipanga kuondoa mizengwe kwenye uteuzi na kutokufanya makosa?
Kama ni ndio tunasubiria kuona kuanzia ngazi ya Uraisi maana kama hawajajipanga kulingana na Wassira, nchi itaenda Upinzani.

upinzani kwa hawa kinambowe waroppkaji upinzani tz bado sana
 
Kwa uelewo wangu Mara HAKUKUWA na kanda ya Mahakama Kuu kipindi hicho na Jaji Lugakingira RIP alikuwa kanda Mahakama ya Dodoma na kesi maarufu iliyo mpa credit ni ile ya Mtikila na wagombea binafsi

Anyway miaka mingi imepita Manyerere anaweza akawa yupo correct

Mkuu, Mahakama Kuu ilikuwa katika Kanda. Majaji walisafiri mikoani. Nakumbuka kesi ilichelewa kuanza kwa siku mbili. Nilimfuata Hakimu Mutungi wa Mahakama Mkoa wa Mara (sasa Jaji) ofisini kwake kumuuliza kulikoni kesi ichelewe kuanza kama ilivyopangwa. Jibu alilonipa ni kwamba Jaji alikuwa amekwama njiani kutoka Mwanza kwenda Musoma baada ya gari lake kuharibika. Ilimlazimu apelekwe hotelini (nadhani Magu) ili utafutwe usafiri mwingine. Kumbuka wakati huo usafiri ilikuwa shida na barabara hazikuwa njema. Kwa maelezo haya ni kwamba Jaji Kahwa Lugakingira hakuwa Jaji wa Musoma au Mara. Alikuwa anatoka Kanda ya Kati.
 
Gwanco unamwonea Mzee Warioba. Jaji Kahwa Lugakingira alikuwa ni jaji wa kipekee. Sina kumbukumbu ya kesi aliyoamua kisha ikatenguliwa na Mahakama ya juu. Kumbuka hata kesi ya Mtikila la mgombea binafsi alikuwa ni Jaji Lugakingira. Hadi leo msumari wa hukumu yake uko pale pale. Alikuwa Jaji makini sana.

Jaji Lugakingira alikuwa kiboko, Kama kesi yako hiko kwa Lugakingira basi wewe tegemea haki tu.. KUna kesi mmoja ya vyama vya ushirika (nafikiri) walikuwa na kesi na masikini mmoja.. Hiyo kesi alipangiwa Lugakingira, basi bwana watu wakaleta mlungula kwa Jaji, Jaji Lugakingira aliwambia kuwa "Mimi ni masikini, na pesa ninazipenda sana,niletee pesa yako baada ya kufanya maamuzi ya kesi yako na mimi nitapokea" (hapo unaongea naye hakuangalii machoni)...

Yaani mahakama kuu ya Mwanza kulikuwa hakuna jaji mpenda haki kama Lugakingira kesi zake nyingi kama si zote zilikuwa hazikatiwi rufaa maana alikuwa ana bana kote kote..

RIP Lugakingira uliyetumia elimu yako kutoa hak!!
 
Brother, kwani Wasira hautaki urais? Anautaka. Je, hujui anayepata urais ndiye anayekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?

mkuu pale juu ulisema "licha ya uzee wake kikwete kamng'ang'ania" hii inamaana waasira ni mzee sana hivyo apumzike au .....
 
Ukiacha mambo mengine mengine, Wasira ni mmoja wa watu wenye akili na weledi wa hali ya juu sana. Ana uwezo wa kujenga au kupangua hoja kwa kiwango cha juu. Nadhani ndio maana JK kamng'ang'ania kipindi chote cha miaka 10 licha ya umri wake. Akili yake inakata kama wembe. Wakati wa sekeseke la minofu ya samaki iliyomng'oa Profesa Mbilinyi, Wasira alikuwa moto wa kuotea mbali. Alilichangamsha Bunge kwa hoja murua. Sijui wakirejea CCM wanafanywa nini hadi kupoteza weledi wao.
Angalizo: Maelezo haya hayana uhusiano wowote na nia yake ya kutaka awe Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa letu.

Hilo nnakubaliana na wewe na nimemsikiliza mara nyingi na nnaamini hilo ni sawa kabisa.
 
Ukiacha mambo mengine mengine, Wasira ni mmoja wa watu wenye akili na weledi wa hali ya juu sana. Ana uwezo wa kujenga au kupangua hoja kwa kiwango cha juu. Nadhani ndio maana JK kamng'ang'ania kipindi chote cha miaka 10 licha ya umri wake. Akili yake inakata kama wembe. Wakati wa sekeseke la minofu ya samaki iliyomng'oa Profesa Mbilinyi, Wasira alikuwa moto wa kuotea mbali. Alilichangamsha Bunge kwa hoja murua. Sijui wakirejea CCM wanafanywa nini hadi kupoteza weledi wao.
Angalizo: Maelezo haya hayana uhusiano wowote na nia yake ya kutaka awe Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa letu.
Kuna kitu Wasira hakukisema, labda kasahau. Alivyotoka NCCR alianzisha chama yeye na Weid Mwasakafyuka na chama chao kikapata usajili wa muda, nimelisahau jina la chama hicho kwani ni siku nyingi. Ni baada ya chama chao kukosa usajili wa kudumu na biashara yake ya samaki hapo Msasani kwenda kombo ndipo alipowapigia magoti ccm. Alikuwa taabani kiuchumi na mke akawa amezamia huko majuu. Msongo wa mawazo alikuwa anaongea peke yake kama chizi.
 
Kuna kitu Wasira hakukisema, labda kasahau. Alivyotoka NCCR alianzisha chama yeye na Weid Mwasakafyuka na chama chao kikapata usajili wa muda, nimelisahau jina la chama hicho kwani ni siku nyingi. Ni baada ya chama chao kukosa usajili wa kudumu na biashara yake ya samaki hapo Msasani kwenda kombo ndipo alipowapigia magoti ccm. Alikuwa taabani kiuchumi na mke akawa amezamia huko majuu. Msongo wa mawazo alikuwa anaongea peke yake kama chizi.


TRA walimwandama sana. Biashara yake ya samaki ikakosa nguvu. kwa kweli kwa wapinzani wa wakati huo ambao wamevumilia hadi leo wanastahili kupongezwa. Mtu kama Ndesamburo, Mbowe na wengine wana roho ngumu kwa kweli.
 
TRA walimwandama sana. Biashara yake ya samaki ikakosa nguvu. kwa kweli kwa wapinzani wa wakati huo ambao wamevumilia hadi leo wanastahili kupongezwa. Mtu kama Ndesamburo, Mbowe na wengine wana roho ngumu kwa kweli.

Naskia ugomvi wa Wassira na Warioba ,uliamia kwenye mchakato wa katiba mpya
 
Kamanda, Comred Manyerere Jackton ndio yuko right, Jaji alikuwa Kahwa Lugakingira.
Malafyale, atakuwa amelichanganya jina la Prof. Jwan Mwaikusa na Mwaikasu

Mwaikusa alikuwa wakili wa Warioba!.

Siku zile ilikuwa very interesting kusoma kesi magazetini. Mimi nilianza kusoma kesi magazetini nikiwa darasa la tano, primary enzi ya Kesi ya Mauaji Mwanza, Mzee ndiye alikuwa RSO wa Mwanza wakati wa seke seke ile!. Nyumba ya RPC, RSO NA DSO wa mwanza zilikuwa zinafuatana, sisi watoto tulikuwa marafiki, hivyo ikatokea kesi wababa wa nyumba tatu zinafuatana wanahusika!.

Pasco.
Baba yako alisalimika baada ya ile kesi?! Nakumbuka RSO wa Shinyanga alifungwa miaka 7.
 
Du, ile radi ya jana Dar ilikuwa ikiashiria ujio wa pongezi hizi kutoka kwako. Kwa mara ya kwanza walau tumekubaliana.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

"Nitasema kweli daima, uongo kwangu ni mwiko" (ingawa mwenyewe aliyetuaminisha maneno hayo alikuwa muongo).
 
Mwaka 1996 niliripoti kesi ya Warioba Vs Wasira. Ilifanyika Mjini Musoma. Wakati huo Mutungi (huyu wa Usajili wa vyama) alikuwa Hakimu Mkoa wa Mara. Kesi ilisikilizwa na Jaji Kahwa Lugakingira. Mawakili wa Wasira walikuwa Malamsha, Mwambegele (sasa ni Jaji), na Mabere Marando. Warioba aliwakilishwa na Josephar Rweyemamu na Profesa Jwan Mwaikusa (marehemu). Kesi ilikuwa tamu sana sana. Ushahidi ulikuwa na mvuto wa aina yake.
Nakumbuka Mabere alimwuliza Warioba, "Hivi wewe Warioba umeoa?" Halafu akamwambia, "Wewe umeshakuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na tena Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, unajua ukiongea uongo hapa mahakamani utafungwa?"
Baadhi ya mashahidi wa Wasira ni kama Kicharwi Chacha Henche, Gamitwe, Museveni nk. Hizo notebook za kesi nzima ninazo hadi leo. Lakini tukio moja nalikumbuka, tukiwa karibu na Mkendo Guest House (nje kuliuzwa vinywaji na vyakula), jioni; Wasira akaniona. Akanifuata akiwa amewaka kweli kweli. Akataka akiidake anizabe kibao, bahati nzuri nami nilikuwa 'mzima'. Nikasimama kando. Marando akaingilia kati kuzuia. Wasira akawa amewaka kweli kweli akidai nilikuwa nikiripoti kwa kumpendelea Warioba. Marando akajaribu kumweleza kwamba kwenye ile kesi hatua za awali hapakuwa na namna ya kuripoti zaidi ya vile nilivyofanya.
Nikadhani yameisha, Kesho yake mawakili wa Wasira wakawasilisha hoja kwa Jaji Lugakingira nizuiwe kuripoti. Jaji akawaomba ushahidi wa distortion, wakawa hawana. Jaji akaamuri niendelee na kazi. Kesi hiyo ilikuwa na mvuto wa aina yake kwa kweli.

ilikuawe wassira alionekana ametoa rushwa kiasi cha kuzuiwa kugombea kwa miaka mitano?
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira amesema mgogoro wake na Jaji Joseph Warioba uliotokana na kura za maoni ndani ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, ndiyo uliomsukuma kujitoa chama tawala na kujiunga na NCCR-Mageuzi.

Hata hivyo, katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Wasira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda (CCM) amesema hajutii uamuzi wake huo kwa kuwa anaamini historia imeandikwa.

Wasira aliingia kwenye mgogoro na Jaji Warioba wakati mwanasheria huyo akiwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais katika Serikali ya awamu ya pili na Wasira akiwa Waziri wa Kilimo.

Wasira alisema hakwenda NCCR-Mageuzi kwa lengo la kufanya ushushushu na baadaye kurudi CCM kama alivyofanya mwaka 2000, bali alikwenda huko baada ya haki yake kuminywa na viongozi wa CCM wa wakati huo.

Alieleza kuwa baada ya uchakachuaji huo katika kura za maoni, aliamua kwenda Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam kukata rufaa, lakini hata huko hakutendewa haki, kwani rufaa yake iliwekwa kiporo na ingesikilizwa baada ya uchaguzi mkuu.

Mgogoro ulivyoanza
“Nataka mwelewe kwamba mimi sikwenda upinzani kwa sababu nilikuwa napingana na sera za CCM. Kwanza 1985 nilikuwa mbunge na ndiyo maana Rais Ali Hassan Mwinyi aliniteua kuwa waziri wa kilimo,” “Mwaka 1990 niliacha kugombea kwa kumwachia Jaji Warioba. Kwa sababu kama utakumbuka mwaka 1985 Warioba alikuwa ameteuliwa kuwa mbunge na waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais.”​
Wasira alisema aliamua kumwachia Jaji Warioba kwa kumheshimu kwani aliamini ingekuwa
kampeni ngumu kwamba waziri mkuu anachuana na waziri wa kilimo, ingawa hata hivyo, alisema iwapo angeamua kuchuana naye angemshinda.
“Lakini lile jimbo lilikuwa la kwangu kwa sababu mimi ni kiongozi kutokea chini kwenda juu na mwenzangu Warioba ni mwanasiasa wa kutokea juu kwenda chini,”​
alisema.

Wasira ambaye alionekana kuukumbuka vizuri mgogoro huo alisema,
“Hiyo ndiyo tofauti iliyopo. Kwa hiyo kama mimi ningeamua kuchuana naye, angeshindwa mwaka huo wa 1990. Sasa faida yenyewe iko wapi?”​
alihoji Wasira.
“Mimi nikaamua kujitoa si kwa kumwogopa Warioba, hapana. Hii ilinipa sifa nzuri kwa sababu Mwalimu (Julius Nyerere) aliniambia umefanya jambo la heshima sana,”​
alisema.

Hata hivyo, Wasira alisema ilishangaza kuona Mwalimu Nyerere alimsifia kwa uamuzi wake huo, lakini Warioba mwenyewe aliyeachiwa jimbo hilo hajamsifia wala kumpongeza.

Alisema katika kipindi chote cha miaka mitano aliyomwachia Warioba jimbo hilo, wananchi hawakupata huduma nzuri hivyo wakamtaka yeye arudi mwaka 1995.
“Wapigakura wetu hawakupata huduma nzuri sana katika miaka hiyo mitano. Labda kwa kuwa alikuwa mtu mwenye shughuli nyingi sana kwa hiyo hakugusa msingi wa watu wa kawaida, kukawa na manung’uniko mengi,”
“Walinung’unika sana kwamba mimi nimewaacha nimekabidhi jimbo lao kwa mtu ambaye hayuko karibu na wao, basi kukawa na demand (hitaji) la mimi kurudi. Sasa mwaka 1995 mimi nikarudi kupitia CCM. Hiyo ndiyo nataka mjue.”​
alisema Wasira.

Alifafanua kuwa wakati huo kura ya maoni ilikuwa ikifanyika kata kwa kata ikiwahusisha mabalozi wa nyumba kumi na walipofanya kura hiyo katika kata kumi kati ya 12 yeye (Wasira) akawa ameshinda kata nane za jimbo hilo.
“Nikawa nimeshinda nane yeye ameshinda mbili, lakini zimebaki nyingine mbili. Kati ya mbili zilizobaki, moja ni ya nyumbani kwake kwa hiyo ili ashinde ilikuwa sasa lazima aweze kufanya mbinu,”​
alidai Wasira katika mahojiano hayo.

Wasira alisema mbinu iliyotumiwa na Jaji Warioba wakati huo ilikuwa ni kuwafanya wananchi karibu wote wa kata hiyo wapige kura upande wake badala ya mabalozi wa nyumba kumi kama Katiba ya CCM ilivyokuwa inaelekeza.
“Unaweza uka-imagine (kufikiria) kijiji chote sasa kinapiga kura, kila mtu akageuka kuwa balozi wa nyumba kumi. Kwa ajili ya ku-offset (kuondoa) tofauti kati ya ushindi wangu wa kata nane ili uweze kujibiwa na kata moja”​
Alisema hali hiyo ilimfanya ajitoe katika kinyang’anyiro hicho baada ya kutoridhishwa na namna uongozi wa CCM Wilaya ya Bunda ulivyoshindwa kuingilia kati suala hilo la wazi.

Ashtaki kwa makao makuu

Waziri Wasira alisema baada ya kuona suala hilo limeshindwa kupata mwafaka, yeye na wazee kadhaa wa jimbo hilo walifunga safari hadi makao makuu ya CCM jijini Dare es Salaam ili kumshtaki Jaji Warioba.
“Sasa manung’uniko tukayaleta makao makuu ya chama wakati ule Lawrence Gama (Marehemu) ndio alikuwa katibu mkuu. Tukaja kukata rufaa na wazee wa CCM kutoka Bunda wanasema uchaguzi si sawa,”
“Wale wazee sasa tulipokuja kwa mheshimiwa Gama akatuambia hilo tatizo lenu tutalishughulikia baada ya uchaguzi. Tukasema hii hakuna haki sasa, maana baada ya uchaguzi wakati uchaguzi ndiyo hoja, haukuendeshwa vizuri?”
“Tulitarajia katibu mkuu atasema anaingilia kati ili uchaguzi urudiwe, sasa badala ya kusema unarudiwa anasema kesi itasikilizwa baada ya uchaguzi, tukawa njiapanda mimi pamoja na wale wazee tuliokuja nao Dar es Salaam.”​
Kuhamia NCCR-Mageuzi

Wasira alisema kutokana na kukasirishwa na namna marehemu Gama alivyoshughulikia suala hilo, wale wazee walimweleza kuwa jimbo hilo lingeangukia mikononi mwa upinzani kwa kuwa Jaji Warioba alikuwa hakubaliki kwa wananchi.
“Wakaniambia hata usiposimama wewe sasa, kwa sababu hutasimama kupitia CCM akisimama mtu mwingine wa vyama vya upinzani atachukua na ambaye anaweza kuwa dhaifu zaidi,”
“Kwa hiyo wale wazee wakaniambia utoke CCM uende chama kingine ili uchukue lile jimbo uendelee kuongoza. Lakini wao wakasema hawatoki CCM watanipigia kura wakiwa huko huko.”
“Sikwenda NCCR-Mageuzi kwa sababu nilikuwa napinga sera za CCM, hapana. Nilienda kunusuru jimbo kwa sababu nimeshindwa kupata jibu CCM,” alisema Wasira na kueleza kuwa huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuhamia NCCR-Mageuzi.
“Kwa hiyo nikaenda NCCR-Mageuzi, (hicho chama) bado kipo niliingia bila kujua madhumuni na mpaka leo bado sijasoma madhumuni hayo, lakini nikaenda. Unaingia chama siku hiyo hiyo unapewa na kadi na uteuzi hapo hapo,”​
alisema Wasira.

Warioba kortini

Waziri Wasira alisema baada ya kupata kadi na uteuzi wa kuwa mgombea ubunge Jimbo la Bunda kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, walirudi Bunda na aligombea na kumshinda Jaji Warioba.
“Tukaenda tukagombea ubunge tukamshinda Warioba. Nikawa mbunge na bwana Warioba akakimbilia mahakamani. Warioba ni jaji, sasa kesi ya tumbili unampelekea nyani sina hakika sana kama nitashinda. Siwezi kusema zaidi ya hapo.”​
Wasira alisema Mahakama Kuu ilisikiliza shauri hilo la kupinga matokeo ya uchaguzi na kuamua kutengua ubunge wake na kumzuia kugombea ubunge kwa kipindi cha miaka mitano kwa kuridhika na madai ya ushindi wake kugubikwa na rushwa.
“Tumefanya kesi nimezuiwa kugombea tena, tumekaa, nikaenda kuuza samaki zangu pale Msasani (Dar es Salaam) kwenye kituo changu cha Cold Storage maana huwezi kusema kwa vile umetoka basi kazi yako ni kusubiri ufe, lazima utafute suluhisho,”
“Nilifanyafanya pale vibiashara na vyenyewe havilipi lakini haikupita muda mrefu sana nikaamua kurudi CCM,” alisema na kuongeza; kwa sababu mimi kwa kweli historia yangu ni ya ndani ya CCM tangu nina miaka 13, sasa utaenda wapi, lakini siyo kwamba historia haikuandikwa, historia imeandikwa na uzoefu nimepata.”​
Kuhusu upinzani

Wasira alisema hivi karibuni alikutana na mtu mmoja ambaye hata hivyo hakutaka kumtaja, akimtaka ampe uzoefu wake kuhusu vyama vya upinzani nchini kwa kuwa yeye aliwahi kuwa huko.
“Nikamwambia mimi naviona kama ni vya watu binafsi. Kwa mwenye chama chake huwezi kusema lolote. Aliyekianzisha ndiye huyo huyo anaendelea nacho,”
“Ukijaribu kupambana naye unapata matatizo. Mrema (Augustino wa TLP) alipata matatizo sana NCCR-Mageuzi kwa sababu kile chama kilikuwa cha Marando (Mabere) na Mbatia (James).”​
Wasira alisema chama hicho kilimkodisha Mrema mwaka 1994 kwa kuwa alionekana kama ana nguvu kidogo, lakini baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wakamtosa.
“Wakagombana na Marando. Marando tukamwambia si mtoke wote akasema hakuna, bora kifo. Hilo ndilo tatizo la vyama hivyo vipya, anayevianzisha ndiye anaendelea tu na demokrasia ni ndogo sana,” alisisitiza Wasira.
“Wala msijidanganye sana ukaona televisheni watu wanapiga makofi siyo rahisi. Hao waanzilishi wa hivyo vyama siyo rahisi kutoka na mifano ipo wala sitaki kutaja majina ya watu kwa sababu mnawajua na vyama mnavijua.”
“Siwezi kujuta kutoka CCM kwenda NCCR- Mageuzi kwa sababu nilikuwa natafuta haki na haki zina gharama. Unachojutia ni nini, si uamuzi niliufanya mimi na haki nilinyimwa mimi nikaitafuta kwa njia nyingine sasa kujuta unajutia nini?​
alihoji.

Makosa ya uteuzi CCM

Mbunge huyo wa Bunda ambaye pia anatajwatajwa kuwania urais, alibainisha kuwa kushindwa kwa CCM katika baadhi ya majimbo baada ya vyama vingi nchini, kulichangiwa na uteuzi mbovu wa wagombea na mizengwe kwa wale walioongoza kura za maoni.
“CCM ni taasisi inayoongozwa na wanadamu wala siyo kwamba yenyewe huwa haifanyi makosa. Ni taasisi ya kibinadamu tu. Mahali pote CCM tulishindwa kwenye majimbo, tulishindwa kutokana na makosa yetu katika uteuzi,” alisema Wasira.
“Shibuda (John) ni mfano mmojawapo, lakini majimbo ya Iringa Mjini, Mbeya, Musoma Mjini, Arusha na Lindi, mahali popote unaposikia CCM imeshindwa lazima kuna makosa fulani imefanya halafu hao wapinzani wakapita.”​
Imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la Mwananchi: Wasira - Warioba alinikimbiza CCM 1995


Chanzo: Mgogoro wa Wasira na Warioba... "mwanasiasa wa kutokea juu kwenda chini." - wavuti

Naaaamm, Dada leo hujapost na kuandama dini fulani na kusapot vikundi vya kigaidi.
Nimekuja huku mbio nikijua kuna thread ya ugomvi wa kidini....naaam asante kwa maelezo marefu.
My advice! Focus kwenye dini achana na mambo ya kisiasa. Hao uliowataja waache ni makafiri pia.
 
Wasira alipewa jina la Tyson kwa kumshinda Warioba sio kwa kumpiga Mwandishi

tatizo nini, warudie round hapo Octoba tuone. Wariba agombee kwa tiketi ya mgombea binafsi (kikatiba kama itakuwa ok) na wassira ccm mana najua Warioba ccm wanamgwaya hawatampitisha kwa msimamo aliokuwa nao
 
Back
Top Bottom