Wassira on ITV (kipindi maalum)

Wassira on ITV (kipindi maalum)

Waache wafanye wapendavyo. Hata kama ni kuwapakia watu kwenye malori. Tumewashika pabaya mwaka huu. Kitaeleweka tu!
 
Mtangazaji kachemka sana leo alikuwa kama yeye ndo mgeni mualikwa hala wasira muendesha kipindi na alikuwa anauliza maswali elekezi. Kafunikwa na gabriel zakaria wa tbc1 ambaye maswali yake yalikuwa ya akili.
 
Amemaliza na hana jipya
Ukweli ni kwamba chadema imeiweka pabaya ccm pale jimboni kwake bunda baada ya mkutano na maandamano ambapo mgombea wa CDM alishushwa jukwaani na wananchi kwa kumuuzia jimbo wasira a.k.a hasira,anajuä amekalia kuti kavu.sasa hv kila wiki hakosi hapa na sijui hata huko dar anafanya kazi saa ngapi kama ametoka bunda leo na amefikia ITV.
 
Naona tv nazo zimekosa watu wa kualika! Hapo leo wamepoteza audience kubwa tu!
 
kutumia matusi kujibu hoja za wassira hapa JF kumbe nayo ni maendeleo. hakika demokrasia inashamiri.
 
Hili ndilo neno kuwaacha chadema wakitema cheche nchi nzima bila CCM kuzunguka kujibu mapigo ni hatari.
 
Watazunguka kusema nini? Kwamba maisha hayajapanda au kwamba hakuna mikataba ya kifisadi? Akili hawana kweli hawa!
 
kutumia matusi kujibu hoja za wassira hapa JF kumbe nayo ni maendeleo. hakika demokrasia inashamiri.

kesho nakuja na thread kuhusu wasira inaonekana wana jf hammjui vizuri ngoja nikalale kesho kila kitu live alichowahi kufanya wasira.
 
Kama mtazunguka nchi nzima kujibu kwa kusema uongo kuwa mmetimiza ahadi mlizo ahidi wananchi wakati zinaonekana wazi hazija tekelezwa na hazitekelezeki hicho kita kuwa kitanzi CDM haina deni kumbuka haichukui kodi zetu.......Njooni mlete longolongo tuwa zomee....
 
eti mpaka leo hii anategemea kilimo cha mvua kiondoe njaa!
 
Wazunguke tu wakakumbane na aibu..na matatizo haya kweli watawaambia nin wananchi...hata waliowapa kura plus kuchakachua wanajuta kuzaliwa na kuisapot chichiemu.
 
Haitasaidia, wasipoteze muda maana wanamajukumu mengi ya kutenda ili kujibu hoja za CDM. Kama ni kweli wanampango huo, basi ni dhahiri tusitegemee Ufisadi kwisha, DOWANS na mikataba mingine feki kushughulikiwa kiadilifu nk. Yani pamoja na ushauri mwingi niliousoma hapa JF na kwingineko bado hawajifunzi. Kweli nimeamini ule usemi wa wenzetu usemao mbwa mzee huwezi kumfundisha mbinu mpya.
 
Haitasaidia, wasipoteze muda maana wanamajukumu mengi ya kutenda ili kujibu hoja za CDM. Kama ni kweli wanampango huo, basi ni dhahiri tusitegemee Ufisadi kwisha, DOWANS na mikataba mingine feki kushughulikiwa kiadilifu nk. Yani pamoja na ushauri mwingi niliousoma hapa JF na kwingineko bado hawajifunzi. Kweli nimeamini ule usemi wa wenzetu usemao mbwa mzee huwezi kumfundisha mbinu mpya.

kwa manara ya kwanza naanimini ccm kinakufa.


loo!!!!!!!!!!

maskini ccm.
 
Kwani yeye ni msemaji wa serikali au CCM!, au Makamba kafa! lakini Chiligati pia siyupo? kweli CCM haina kichwa wala miguu, Ikulu inatumika kisiasa zaidi mi nawalani kwa nguvu zangu zote UWT kwa uovo huu
 
Bado anasema Chadema wanataka kuiondoa serikali kwa mabavu.
Si wawashitaki viongozi hao wa CDM wanaotuhumiwa kwa uhaini, uchochezi, majungu na fitna mbaya kwa JK. Mbona kila siku kulalamika sasa tutashindwa kuelewa kama serikali inaiogopa CDM au?
 
Mie nilimchoka kabisa! Alionesha kutokuwa makini na maswali mazito mazito akawa amemuachia aseme anavyotaka!
 
.
Kuna jamaa juzi alinivunja mbavu. Eti dereva wa wasira aliwahikamatwa na askari wa mbuga ya serengeti. Siku hiyo walikuwa wametoka mara wakiwawanacross mbuga ghafla wakakuta geti la askari wa Tanapa, wakati huo mh. Alikuwa ameuchapa usingizi kwenye kiti cha nyuma baada ya hao askari kulikagua gari wakamwambia dereva uko chini ya ulinzi, alipohoji sababu akajibiwa kwamba amebeba nyara za serikali kwa nia ya kuzitorosha. Ndipo dereva alipojitetea kuwa "jamani hizi siyo nyara za serikali bali ni mh, waziri wa serikali"
.

Duuuuh hiyo kali, jamaa keshakuwa nyara ya serikali! Ndiyo maana JK hamtupi kwa sababu ni highly demanded.
 
Back
Top Bottom