Wassira on ITV (kipindi maalum)

Wassira on ITV (kipindi maalum)

Ahaa, anasema ccm itajibu mashambulizi kwa maandamano
Mikwara ya namna hiyo tumeshaisikia mpaka, naomba warudishe ile salamu yao ya kidumu Chama cha Mapinduzi, Kigumuuuuu badala yake imekuja CCM Oyeeeee, Oyeeeeeeee chini ya rais wetu JK. CCM bana!
 
Anaruhusu maswali ya kupigiwa simu?
Hakukuwa na maswali ya kupigiwa simu, na mwandishi mwenyewe maswali yake ni ya kinyela mpaka Wassira ana shine. Wassira kasema kuondoa serikali "kwa nguvu ya umma" maana yake uchaguzi, lakini uchaguzi ushapita na ujao muda wake bado. Kwa maana hiyo matamko hayo ni ya kichochezi.

Halafu kasema Dr. Slaa kamsingizia Mkuu wa Mkoa (Shinyanga nadhani) kwamba kafa! Akasema Slaa mwongo!

Halafu kasema point ya Slaa kwamba Bunda kuna njaa ilhali Wassira alikuwa Waziri wa kilimo ni nonsense kwa sababu yeye sio waziri wa Bunda, na huyo Dr. Slaa angekuwa Rais angepeleka rasilimali za nchi zote Karatu?

Na akasema ya Tunisia na Libya vurugu etc. hayana haja kutokea hapa kwa sababu hapa Rais ana term limit ya miaka 10 hata "angenogewa vipi." Huko kwingine wametawala miaka 40.

Kuhusu lalamiko la bei ya mafuta, kasema chanzo chake ni huko huko ambako CHADEMA wanasema tuige mfano wa "nguvu ya umma". Na hawawezi kushusha kodi ya mafuta kwa sababu wanazihitaji kujenga barabara, na hii ni "trade off" ya kiuchumi.

Kasema kosoeni serikali, ndio kazi yenu, lakini mkichochea kuiondoa madarakani kimabavu yeye ana nguvu ya dola.

Kale ka mwandishi kalivyokuwa katupu eti kakamuuliza, kwa nini usitumie ukali. Wassira akasema watoto wadogo ndio wanakaripiwa yeye anaelimisha!
 
Wakuu, mh! Wasira mbunge wa bunda na mjumbe wa nec ya ccm, amesema wanajipanga CCM kuzunguka nchi, kujibu mapigo ya CHADEMA kwa kutumia mikutano ya hadhara.
My take, CCM wasije wakawa wanawapakiza watu kwenye malory na kuwalipa. HATUDANGANYIKI

Binafsi sidhani kama hii ni strategy muafaka kwa CCM at this time. Wananchi wana hasira, na wamekata tamaa. Ushahidi tosha ni umati wa watu kwenye mikutano ya CDM na kufurika kwa watu kule Loliondo. Tatizo la CCM ni la kisera zaidi kuliko kuzunguka kujibu mapigo ya CDM ambayo sidhani kama wana majibu ya kuridhisha kwa sasa badala ya propaganda. Watanzania wanataka majibu ya vitendo na si majibu ya nadharia kwenye mikutano ya hadhara. Wakifanya hivyo watakosea na watazidisha hasira ya wananchi. I think damages itakuwa kubwa kuliko kujikalia tu kimywa huku wakitimiza ahadi zao pole pole.

Kuna haja pia ya CCM kuwaelemisha makada wake kuhusu dhana nzima ya siasa za ushindani. Chama chochote makini cha siasa lengo lake ni kushika dola, na CDM wanachofanya ni kutafuta njia za kushika dola.Kwa mtu mwenye hadhi ya uraisi au waziri kusema wanataka kuiondoa serekali madarakani ni kutokuwa responsible. Jeshi bado ni tiifu kwa serekali, sasa CDM watawezaje kuiondoa serekali madarakani. Na hata hivyo kuna ubaya gani kwa walioiweka serekali madarakani kuindoa ambao ni wananchi? CDM inahamasisha wananchi tu kujua haki zao na thamani ya kura zao, kama Republican walivyohamasisha wapiga kura wa marekani kuipunguza nguvu Democrats kwenye mid term election. Kuna haja sana ya kujifunza!!

Lakini cha msingi ni kizazi cha kina Wassira na watu wenye mawazo mgando kama Mrema, Cheyo Chiligati Gadaffi etc kufutika ili kuona mabadiliko ya kweli. Tutajidanyanya kama viongozi wetu ni hao wa hicho kizazi, wanajiwazia wao tu bila kuwawazia wengine. Na hata CDM wakiingia madarakani, kama wasipokuwa na viongozi wa kutoka vizazi tofauti wakabakia kina Dr Slaa, etc, bado hali haitabadilika.
 
Kwani yeye ni msemaji wa serikali au CCM!, au Makamba kafa! lakini Chiligati pia siyupo? kweli CCM haina kichwa wala miguu, Ikulu inatumika kisiasa zaidi mi nawalani kwa nguvu zangu zote UWT kwa uovo huu

Kama siyo wewe! Unajitahidi sana kwenda na upepo!
 
hivi hawa watu hawana kitu kingine cha kuongelea kila siku cdm umeme unavyotutesa hawaoni wanaiona cdm tu hebu watuondolee upumbavu wao kwenye tv najisikia kutapika nikiona picha zao kwenye tv
 
I

Mkuu, kama kweli basi itakuwa balaa.
Siaa ni mashine ingine kabisa.
Mkuu ni kweli we endelea kuangalia tu ITV utaona oneday wanatoa tangazo kama lilivyokuwa kwa wasira kwenye kipindi cha 45 mnts....ila inakuwa recorded. This time itakuwa someone from Chadema kuja kujibu utumbo wa wasira na ccm yake
 
Jamani mimi leo ni kuku mgeni kamba mguuni naomba msinitupie mawe.

CCM walisema uchaguzi umekwisha sasa ni kufanya kazi wanapotaka kuandamana si watakuwa wanalamba matapishi yao au nisaidieni hapa.
 
Hawajajua kinacho wasibu nini hawa CCM! Wana-fumble tu. La kuvunda kweli halina ubani!
 
Mh,wasira..a.k.a(hasira) on,itv .vijembe na kejeli ya wazi aliyoonyesha.nimegundua wazi..
HOFU kubwa aliyonayo juu ya CDM baada ya mkutano wa Dk slaa Bunda, na aliyekuwa mgombea wa CDM,kushushwa jukwaani na umati akituhumiwa kuuza jimbo kwake."TYSON AMEKALIA KUTI KAVU" JIMBONI MAPEEMA.hivyo hasira ni ya KUPOTEZA JIMBO si AMANI ya NCHI.Nawakilisha..
 
Wakuu, mh! Wasira mbunge wa bunda na mjumbe wa nec ya ccm, amesema wanajipanga CCM kuzunguka nchi, kujibu mapigo ya CHADEMA kwa kutumia mikutano ya hadhara.
My take, CCM wasije wakawa wanawapakiza watu kwenye malory na kuwalipa. HATUDANGANYIKI

Jamani kwani Wassira ndiye amechukua nafasi ya Makamba sasa? Yeye sasa ndiye msemaji wa CCM? Mbona anafanya kazi ya Tambwe Hiza na Chiligati? Kama kiongozi wa serikali tulitarajia azungumze kwa mamlaka kama serikali na si kama hivyo anavyofanya propaganda!!! No wonder hajui hata wajibu wake nini au JK hakumpa terms of reference ya hiyo wizara fake anayoiongoza?

Shame on him!!!

Tiba
 
hasira zangu juu ya hichi chama cha nyundo na jembe ni kubwa sana kama huyu mzee hata pale kwao awamtaki nilibahatika kuwa pale mwezi mmoja uliopita bunda stand pale wazee wamekaa kucheza bao huku wakizungumzia siasa karibia watu wote ni chadema na wanamponda sana wasira alafu anakuja kujitapa hapa leo itv na maneno yake ya kijinga aende zake iko siku hii nchi tutaikamata na cha moto watakiona.
 
Anahojiwa katika ule muendelezo wa vipindi maalum vya ushirikina dhidi ya Chadema.

CCM wataanza kuzunguka kuzijibu hoja za CHADEMA

Chadema nendeni kwenye tv programs na nyie pelekeni majibu na ccm wapate joto lao. Nani anataka kumsikiliza Wassira kama alikuwa na majibu mbona asije miaka mitano iliyopita alikuwa wapi? Miaka karibu ishirini anabadilisha wizara kama yeye ndie alizaliwa kushika nafasi mbalimbali serikalini. Porojo tupu na pumba.
 
sikuwa najua kama wassira ni pumba kiasi kile, duuh CCM wana kazi kubwa ya kujisafisha
 
Anahojiwa katika ule muendelezo wa vipindi maalum vya ushirikina dhidi ya Chadema.

CCM wataanza kuzunguka kuzijibu hoja za CHADEMA

Inabidi slaa(chadema) wanyoshe maelezo kuhusu suala la uzushi wa kifo cha RC wa Shinyanga ndugu Balele na pia kuhusu kuiondoa serikali kwa mtindo wa misri,tunisia n.k utaona kwamba haya ndo mambo ambayo wassira(ccm) ameshikia bango! cdm iweke sawa masuala haya otherwise ccm itayatumia kushusha reputation ya cdm na slaa mwenyewe! cdm should be aware of this and should do required efforts to rectify the situation!
 
hivi hawa watu hawana kitu kingine cha kuongelea kila siku cdm umeme unavyotutesa hawaoni wanaiona cdm tu hebu watuondolee upumbavu wao kwenye tv najisikia kutapika nikiona picha zao kwenye tv
Ccm hawana haja na kuleta maendeleo,haja yao ni KUSHINDA CHAGUZI,NA cdm inahatarisha malengo yao, kwa hiyo kwao huyo ndiyo adui no 1.chini ya Ccm tusitegemee lolote,
 
Jamani kwanza wanajamii kama ni great thinker hatupaswi kutoa mitusi, hakuna mshindi kwenye Mitusi na haisaidii, maana sisi ndo wakuwaongoza kina wasira, sasa mnamuita sura mbaya nani mwanaume mzuri? Kama mzuri ujue unauza na wewe, pia hatuwezi hata kuumba kidole chake kwanini tunadharau umbile la mtu. Na kama uzuri ungekua uongozi basi Richard wa big brohter angekua raisi, Tuongeleeni hoja zake zaidi.

Nimemsikiliza Wasira, Pia nilimsikiliza na Tendwa TBC taifa siku mbili za nyuma wote wanaongea vitu vinafanana, Kama wanaCDM lisemwalo lipo tuwe waungwana zaidi tusifanye mambo ya ujanja ujanja, Arusha mabomu yamepigwa juzi kesi ilipoahirishwa watu wanataka waandamane wawapeleke viongozi ofisin kwa ruhusa ya nani? Matendo ya Chadema yanonyesha wazi hawajakubaliana na Matokeo ya uchaguzi ambao ndio chaguo la wengi.

Hatukubali kuwa RAIS amepata kura 5M, wakati CDM 2M, wabunge 178 majimbo, CMD 25 sasa CDM inataka nchi hawa waliowachagua hawa wabunge 178 mtawapeleka wapi? Mtawashawishi wawaunge mkono? Au mtawaua? Nchi sio Arusha, Mwanza na MBEYA. ni pamoja na lindi, singida na TABORA, nani atasema kua MKONO ameiba kura Musoma vijijini? Nani atasema NYARANDU ameiba kura Singida? nani atasema RAGE ameiba kura TABORA? Hawa wamepewa kura na wananchi ambao na hakika ni wengi kuliko wa Mikoa ya chadema tusidharau hili

Muhimu chadema tukubali kuwa ni suprise kuangakuka lakini ndo imetokea tayari, tuwe wapole tusubiri 2015

Chadema wanasema Kikwete kashindwa kuendesha nchi wakati BAJETI YA KWANZA ndo inapelekwa mwezi Juni ameshindwa vipi kabla ya mipango. hata chadema ingekua madarakani ingetumia bajeti na mipango iliyopo mpaka hapo juni ndo wangeweza kurekebisha. Siku mia mnataka rais amalize matatizo ya watanzania tuwe kama libya maji bure, umeme bure, ukioa nyumba unapewa.

Mbona majomboni mimi sijaona walkichofanya wabunge zaidi ya kuita wapiga picha kupiga picha matrekta, trekta la milion saba litatatua matatizo ya wannchi wa jimbo kwani hiyo ni SACCOS?

Awangalie wabunge wenzake wa MUSOMA ameweka Grader na engineer, angalia Mo singida anafanya nini

TUACHE MANENO TUCHAPE KAZI

KUCHAMBA KWINGI MWISHO...., CDM tuache kuchamba maana.........
 
jamani hii nyara ya serikali mbona inatumika vibaya bila vibali kutoka maliasili.....
 
Back
Top Bottom