Hivi huyu mzee kwa umri wake kwa nini hatulii na kutumia busara kama wazee wengine?
Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Bora angekuwa na Busara za Marehemu Phares Kabuye....
Wabunge kumbukeni, fuateni nyayo za marehemu Kabuye
BY MASHAKA MGETA
29th June 2011
.
Akasema mkoani Kagera kuna hadithi inayomzungumzia nyani aliyeketi juu ya mwamba mkubwa. Akiwa kwenye mwamba huo, nyani huyo alitoa ushuzi.
Baada ya kitendo hicho, mwamba ule, kutokana na ukubwa wake, ulimwambia nyani ushuzi wako hauwezi kunitikisa na kweli mwamba haukutikisika.
Lakini nyani akitambua ukweli huo akajibu; japokuwa siwezi kukutikisa, lakini harufu yake umeipata.
Wabunge walicheka sana. Hata waandishi wa habari na watu wengine waliohudhuria kikao kile walishindwa kujizuia, wakacheka sana.
Wengine hawakujua kusudio la Kabuye. Ingawa watafsiri wa misemo ya asili waliweka bayana kwamba ukubwa na nguvu za mtoa hoja haviwezi kuukwepa ukweli. Kwa maana ukweli unabaki kuwa ukweli daima, hata kama utatofautiana na matakwa ya baadhi ya watu.
...
Itakumbukumbwa kwamba hata lilipoibuka suala la kufutwa posho zisizokuwa na tija kwa watumishi wa umma wakiwemo wabunge, watawala na wenye nguvu mithili ya mwamba waliwabeza, waliwadharau na kuwakejeli watoa hoja.
.
Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ni miongoni mwa waliokaririwa wakisema posho ni sehemu ya vyanzo vinavyowapa wanasiasa fedha nyingi kuliko hata wanataaluma na wataalamu wa fani tofauti nchini!
...
Kwa ambao hawakuwa bungeni wakati wa Kabuye, wanaweza kupitia kitengo cha taarifa za Bunge, wazisome na kuzisikiliza hoja zake, ili wajiepushe na kujiweka kando kabisa mwa kasumba ya ninaunga mkono hoja kwa asilimia 100 pasipo tija.
[h=2]Asiyekuwa na dhambi na awe wa kwanza
31/07/2007[/h][TABLE="width: 499"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
MBUNGE wa Biharamulo Magharibi, Phares Kabuye (TLP), jana aliwashtua wabunge na kuamsha hisia zao pale alipoinuka na kudai kuwa wabunge wote walipata ushindi baada ya kutumia rushwa. Akichangia katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria, Kabuye alisema kuwa hakuna mbunge safi ndani ya Bunge hilo isipokuwa yeye na Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
akini baada ya kauli hiyo, Kabuye alianza kuzungumzia rushwa na kusema: Rushwa katika siasa. Zamani kuku walikuwa hawajisaidii sehemu wanayolala, lakini akatokea jogoo akajisaidia mahali wanapolala, na kuku wengine wakiwamo vifaranga wakaona kumbe tulikuwa tunahangaika
tunaweza kujisaidia hapa hapa. Wakaanza kujisaidia.
Sasa wewe jogoo mwanasiasa unapotoa rushwa unakuwa umejisaidia sehemu tunayolala
humu ndani kama tunachunguza na kuwaondoa wabunge
sidhani kama angebaki mbunge
wabunge walioingia humu wameingia kwa rushwa
hatabaki mtu kasoro mimi
pengine na waziri mkuu na rais, alisema, hali iliyodhihirika kuwaudhi wabunge wenzake.
Mnasema mnamuenzi (Mwalimu Julius) Nyerere, halafu mnatumia rushwa
nasema akifufuka humu ndani mtamkimbia wote, alisisitiza.
Mara baada ya kauli hiyo, Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM) alisimama na kutaka mwongozo wa Spika, kuhusu alichotamka Kabuye.
Baada ya hapo, Kabuye alisema: Hilo nililitegemea. Ninao ushahidi wa watu wa Biharamulo, ninaweza kuwaleta wakathibitisha kuwa sijatoa hata pipi. Hata hivyo, wakati mbunge huyo akizungumza, wabunge wenzake walisikika wakitamka bila kutumia vipaza sauti wakimtaka afute usemi na aombe radhi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu), Dk. Batilda Burian naye alilazimika kusimama, kumdhibiti mbunge huyo kwa kutumia kanuni.
Dk. Burian alisema alikuwa amemvumilia kwa muda mrefu Kabuye wakati akizungumza kwa sababu amekuwa akitumia lugha ya kuudhi. Baada ya hapo, Kabuye alisimama na kusema: Kwa kulazimishwa, naomba kufuta usemi. Hali hiyo haikuishia hapo, Job Ndugai, Mwenyekiti wa kikao cha jana, alisimama na kumtaka mbunge huyo kuzungumza lugha inayowiana na mazingira ya Bunge, akisisitiza kwa kusema huenda Kabuye aliamka vibaya.
Mheshimiwa mwenyekiti, si kwamba leo nimeamka vibaya, bali nina uchungu
hata mtu anapofiwa hajui machozi yanatoka wapi
kuna wakati tutafukuzana humu bungeni kwa kusema kwa uchungu, alisema.