Megalodon
Hoja yako ina mantiki sana lakini kuwalaumu Wasomi katika mazigira yaliyopo si sawa
Tunamkumbika Dr Lamwai (RIP) alikuwa diwani wa Manzese kabla ya kuwa Mbunge.
Ule ulikuwa mwanzo wa Wasomi kuchukua hatamu za madaraka, na tuliona mwamko
Vyama vingi vikianza ushindani uliletwa na Wasomi ndani ya Bunge ,CCM ikalazimika kuchagua Wasomi ili wakabilane na hoja nzito.
Tangu chaguzi zimevurugwa idadi ya Wasomi imepungua. CCM hawana upinzani wala sababu ya kuepeleka wasomi. Muhimu ni idadi ya watakaosema ndiyooo! siyo kujenga hoja.
Wasomi wachache ndani ya Bunge wanapigwa vita kama akina Mpina! Hawahitajiki.
Ili Wasomi wawe na msisimko na ili tuwe na Bunge la Wasomi maboresho ya mifumo ya uchaguzi hayana mjadala. Ndio maana hoja ya NRNE ina mantiki sana.
Kwamba tuwe na mfumo utakao favor '' big brain'', siyo huu kuengua na kupachika madubwana
Hoja ya pili, VITI MAALUM futilia mbali.
Bila kubadili mifumo ya uchaguzi, Wasomi hawana sababu, tusiwalaumu
JokaKuu