PreGE2025 Wasomi wanaliangusha taifa kwa asilimia kubwa

PreGE2025 Wasomi wanaliangusha taifa kwa asilimia kubwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mtoa mada una hoja, tatizo la wa tz na waafrika ni ujinga, na uendekezaji wa uchawi na wizi wa kura ni vitu vinawakatisha tamaa wasomi wengi.

Binafsi nna bachelor ya Political science & Public Administration ila siasa za kibongo staki kuziskia asee
Mleta mada kakukusudia wewe haswaaa!
 
Megalodon
Hoja yako ina mantiki sana lakini kuwalaumu Wasomi katika mazigira yaliyopo si sawa
Tunamkumbika Dr Lamwai (RIP) alikuwa diwani wa Manzese kabla ya kuwa Mbunge.
Ule ulikuwa mwanzo wa Wasomi kuchukua hatamu za madaraka, na tuliona mwamko

Vyama vingi vikianza ushindani uliletwa na Wasomi ndani ya Bunge ,CCM ikalazimika kuchagua Wasomi ili wakabilane na hoja nzito.

Tangu chaguzi zimevurugwa idadi ya Wasomi imepungua. CCM hawana upinzani wala sababu ya kuepeleka wasomi. Muhimu ni idadi ya watakaosema ndiyooo! siyo kujenga hoja.

Wasomi wachache ndani ya Bunge wanapigwa vita kama akina Mpina! Hawahitajiki.

Ili Wasomi wawe na msisimko na ili tuwe na Bunge la Wasomi maboresho ya mifumo ya uchaguzi hayana mjadala. Ndio maana hoja ya NRNE ina mantiki sana.
Kwamba tuwe na mfumo utakao favor '' big brain'', siyo huu kuengua na kupachika madubwana

Hoja ya pili, VITI MAALUM futilia mbali.

Bila kubadili mifumo ya uchaguzi, Wasomi hawana sababu, tusiwalaumu


JokaKuu
 
Siasa ni zaidi ya usomi wa cheti, wanaoitwa wasomi wengi wanafeli kwenye siasa sababu sio risk takers, hawana hela na pia ambalo kubwa kuliko yote hawaji connect vizuri na jamii kwa maana sio wanasiasa wazuri.
 
Tatizo wasomi mnafikiria sana halaf really life haitak hiyo

Ngoja muongozwe na wahuni ndio mtastuka
 

Attachments

  • IMG_5571.jpeg
    IMG_5571.jpeg
    261.3 KB · Views: 11
Wasomi ni chanzo cha taifa la Tanzania kuwa jinsi lilivo kwa sasa kama lilivo.

Kipindi Kama hiki ndio kipindi wasomi wanapaswa kuwa mbele kwenye kuchukua fomu za ubunge na uongozi, badala yake utaona fomu zinachukuliwa na mbululazi na hopeless generation.

Utamsikia msomi anasema mimi sitaki siasa, my friend…. Siasa ndio inaamua mustakabali wa nchi, future ya maisha yako na kizazi chako, kwa kuwa wewe hupendi siasa…. Ngoja future yako , salary yako na future ya watoto zako ikaamuliwe na kina babu tale na kina mwijaku , kina salma kikwete bungeni.

Msichukulie poa hizi nafasi, hata Samia mzaha mzaha alitokea chini, leo ndio president wa URT…. na mnaona tofauti ni kubwa….. hi yote ni kwasababu wasomi watanzania mmekataa kukaa maeneo yenu, mnabaki kuwa inspiration writters kwenye social media na kingereza kingiiiii…….. but you are another hopeless generation kwenye taifa.

Imagine Babu tale, Msukuma , Salma and the likes… ndio wanawatungia nyie mustakabal wa taifa lenu…. What a hopeless life

Wasomi KACHUKUENI FOMU MKAE MAENEO YENU.
PERIOD

Dr Megalodon Mushi
Canada
Zibadilishwe kanuni wasomi wawe free kugombea,we kama ni msomi usiombe ucompete darasa la Saba,kunakurogwa hata kupotezwa kwasababu wewe ni threat !na tumekubali kuifanya Siasa kama ajira,survivor of the fittest
 
Hata uwe umesoma vipi kama huna hela huwezi kupata hata udiwani achilia mbali ubunge. Unahitaji angalau milioni 500+ ili uweze kugombea na hao unaowaita hopeless akina Musukuma na Babu Tale kinachowabeba ni pesa na umaarufu. Na wamewekeza wekeza huko majimboni. Kadogosa, kwa mfano, ndiye amekuwa akifadhili mbina ya Bagika na Bagalū kule Simiyu kila tarehe 30 Mei ya kila mwaka. Milioni 20+. Anajulikana. Sasa wewe kurupuka na uprofesa wako eti unakwenda kugombea. Ukipona kuchukuliwa mazima kwenda kufichwa Gamboshi shukuru Mungu 😂

Rudi kutoka huko Canada na usomi wako kama huna hela na exposure kwa wapiga kura wako hata kura moja ya wajumbe hupati!

By the way, wasomi ndiyo wanalaumiwa kwa kuliangamiza taifa hili. Na mara nyingi imeonekana kuwa darasa la 7 wanaweza kuwa bora kuliko maprofesa na Ph.D holders (mf. Kishimba). Hapa usomi hautakiwi bali uwezo wako wa kuwa mnafiki, kufisadika na kusifia!

View attachment 3386560
View attachment 3386564
Umeshaacha kuzusha vifo vya viongozi?

Dr msomi wewe mzee wa kamba nyingi??
 
Wasomi wanaojielewa ni wale wanaoamgalia mifumo na kuona kwamba kujiunga na siasa kwa sasa ni kupoteza mda!

Ni msomi Mpumbavu asiye na maono anayeweza kupoteza mda kuchukua form wakati Lisu yupo ndani Kwa sababu za hovyo.

Kama Lisu na usomi, moyo wake na uungwana wake anatendewa hivyo, ni msomi gani ataacha pigani no reform no election akachukue form?
 
Umeshaacha kuzusha vifo vya viongozi?

Dr msomi wewe mzee wa kamba nyingi??
Mkongwe wa JF tangu 2008. Heshima yako mkuu.

Nilizusha kiongozi gani kafa mkuu? Mimi huyu? Au umechanganya madesa? Unaweza kuleta ushahidi wa dai lako hapa? Kama huna ushahidi, nitake radhi aisee! 😡😡😡🚮🚮
 
Wasiosoma wanatumia mapanga kukamata nafasi; Ni muhimu kuzingatia Nrne kutatua tatizo hili mfano halisi mwangalie Bi kiziwi alivyobinuka sarakazi kuendelea kukalia kiti; Unategemea nini? nini kwenye uchaguzi 2025? nini ulikiona uchaguzi wa 2024?
 
Imagine tungekuwa na wasomi aina ya lisu walioingia bungeni, prety sure katiba ya warioba ingekuwa live now

NENDA KACHUKUE FOMU
ACHA EXCUSES
Siasa laana.
Wasomi Kama Prof.Sarungi, Kapuya,Tibaijuka, Mbilinyi,Muongo, ..
Dr.Mpango, Magufuli, na wengine wengi waligombea na kuingia bungeni.
Je, walileta hiyo katiba ya Warioba?
Wakifungua kule wanafanya mambo collectively na mambo yenyewe ya ajabu ya kulindana au kutetea mambo yanayo chelewesha maendeleo.
 
Back
Top Bottom