Wasomi na kiingereza

Unafikiri kwa nini nchi kama Kenya, uganda, Zambia wapo fluent? Kwamba wao wana akili za kujua sana kiingereza kuliko sisi? No, ni kwamba wao tangu shule za awali (elementary school) wanasoma kwa kiingereza. Hivyo wanaizoea lugha at an early age.
Kwahiyo sie tatizo ni kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia?
Nimekuelewa
 
Kwa bongo ni kawaida,mfumo wetu wa elimu haufundishi kiingereza vzr,ukimtoa Mkapa,nitajie kiongozi gani anaweza kuongea kizungu kilichonyooka,Hata Mkapa Elimu ya juu,kasoma Makerere university Uganda,
Ukienda Zanzibar,Kuna beach boys,wanaongea kizungu,kiitaliano,kirusi,kilichonyooka,na Hawa vijana unakuta hata Darasa la Saba hawakusoma,
Ila tusiwaponde sana wahandisi wetu,maana hata wachina wanaotujengea flyover hawajuhi kizungu,
Muhandisi akishindwa,kufanya kazi yake ya ujenzi aliyosomea,asemwe,ila siyo kushindwa kuongea kizungu.
Mkuu huko Uganda na Kenya wanakiongea kiingereza na ndio maana wanakijua na si kwamba wanafundishwa vizuri english drasani,na wakati wewe unasema mfumo wetu wa ufundishaji ndio sio mzuri kuna wengine wanasema mfumo wa ufundishaji kiingereza mashuleni duniani kote sio mzuri.

Na kweli haya matatizo yapo sehemu nyingi tu ambako raia zake hawatumii kiingereza kama lugha ya mawasiliano.
 
Ili tujue uwezo wako katika kiingereza tafsiri hili bandiko lako katika kiingereza, chukua paragraphs ya kwanza na ya 2.
Translation is also a professional like other professionals. There is hearsay that in Tz there are only three people who qualify for the job!!! Mara nyingi nikisoma Magazetini watu hutafsiri kwa kusema " kwa tafsiri yangu" huwa siwaelewi wana maana gani.
Kingereza kipo cha aina nyingi sana, kila wigo una kingereza chake.
Huwa naingia mtandao wa Quora, kuna baadhi ya maoni kuyaelewa inabidi upretend.
 
Kuna Technical English and General Fluency English. Watu wanao soma sayansi wanatumia Technical English sana. Hivyo ukiwaingiza kwenye General fluency hawatakuelewa. na wewe wakiungiza kwenye technical hutowaelewa. Watu wanaosoma arts ndio wanatumia General fluency English, sana ila nao technical English holaaaa
Siku hizi haki ya nani hata wanaosoma arts bila bila aisee. Asikwambie mtu
 
😆😆 Hao ndio ma boss wenu ?
Kiingereza cha darasani hata mwingereza mwenyewe anajifunza,kiswahili cha darasani pia ni tofauti na cha mtaani,anaweza akawafaulu vizuri mtihani wa kiswahili mtu ambaye sio mswahili lakini akikutanishwa na mswahili kwenue presentation akapigwa bao. So lugha isitumike kumgrade mtu. Tuangalie matumizi ya hiyo lugha pia.
 
Inakuwaje msomi ama graduate wa chuo kikuu aliespend miaka kama minne chuo kikuu na ana degree, masomo yake yote ni kiingereza tupu anafanikiwa kugraduate, lakini ukimwongelesha kiingereza haelewi

Akiamua yeye sasa Hata kuandika ujumbe kwa kiingereza anashusha broken ya hatari hadI unashangaa? Wengine wamefanikiwa kupata kazi kabisa unakuta bonge la engineer from ardhi university English mbovu mkichat yuko kwenye bonge la kampuni

Mbaya zaidi graduate kamaliza chuo few days anaambiwa andika barua ya kuomba internship anaweweseka..Mara nipe google..maelezo yake binafsi yanamshinda kujieleza kwa kiingereza anatafuta CV za wengine akopi.sasa najiuliza huyu mtu kafanikiwa kumaliza successful report zake aliandikaje?kama kiingereza cha kuandika anababaika presentation alihudhuriaje akapata marks
Research zake?

Au ndo wale wa kukariri? Sawa basi hata kama kukariri unashindwa kujifunzia hapo mpangilio wa grammar.

Boss mzima ananitext "is you coming or no"
Kiingereza nacho ni kipaji?
Aliekwambia kupata degree kunauhusiano na kuongea kiingereza nani.

Yani wewe unaonekana fala Kweli kisa umeombwa umsaidie mtu kuandika cv unakuja kumtangaza humu. Kwendaa kafie mbele
 
Kuna Technical English and General Fluency English. Watu wanao soma sayansi wanatumia Technical English sana. Hivyo ukiwaingiza kwenye General fluency hawatakuelewa. na wewe wakiungiza kwenye technical hutowaelewa. Watu wanaosoma arts ndio wanatumia General fluency English, sana ila nao technical English holaaaa

Unapotosha. Hakuna vitu vya namna hiyo.
 
Unapotosha. Hakuna vitu vya namna hiyo.
napotosha kivipi sasa mkuu sema wewe ndio uelewa wako mdogo. Huwezi kunielewa mfano wewe umesoma combination ya HKL na mwingine kasoma PCM. Ni yupi atatoka na skills za kuzungumza na kuandika kiingereza kizuri hapo. Tumia akili acha ushabiki, huyo wa PCM anasoma number tu na kiingereza kwa mbali, na hizo hesabu hazi improve chochote kwenye english yake na wala hazitumiki mtaani. Huyo wa HKL masomo yake yote ni maneno ya kiingereza yaliyojaa na kwenye mitihani yake yote anaandika ma essay tu. Hivyo ni wazi lazima ata improve writing, speaking na listening skills.
 
Kuna Technical English and General Fluency English. Watu wanao soma sayansi wanatumia Technical English sana. Hivyo ukiwaingiza kwenye General fluency hawatakuelewa. na wewe wakiungiza kwenye technical hutowaelewa. Watu wanaosoma arts ndio wanatumia General fluency English, sana ila nao technical English holaaaa
Hoja yako ina mashiko kwa Tanzania tu! Mbona wenzetu Wakenya na Waganda wote wanajua hiyo sjui Tech na Fluent English? Tukubali elimu yetu ina shida.
 
Back
Top Bottom