Wasira asumbuliwa na maandamano ya Chadema

Wasira asumbuliwa na maandamano ya Chadema

Kama Wassira haktaki kumjibu, je mwanakijiji wa kawaida mtamjibu?

Kumbukeni kuwa Wassira ni mtanzania (mwananchi) na akihoji jambo anapaswa kusikilizwa na kupewa majibu kama yao.

Kutokumjibu maana yake ni aidha kudharau mawazo ya wananchi au kutokuwa na majibu.
 
Nashindwa kuelewa, hutamjibu?
Mbona tayari umeshamjibu, ila tofauti ni kwamba hujjibu hoja yake..

Exactly!!!!!!! Jamaa kashafungua mdomo halafu anasema ati sitafungua,,, duh huyu vipi??
Nilikuwa napita fasta tu wakuu
 
Waziri aitisha Chadema Send to a friend Thursday, 03 March 2011 20:54 0diggsdigg

13wasiraleo.jpg
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira

Na Waandishi WetuWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kisije kikailaumu serikali itakapokosa uvumilivu na kutumia nguvu ya dola dhidi yake.

Wassira alisema chama hicho kinapandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali na kuandaa mpango wa kuiondoa kwa nguvu serikali iliyoko madarakani.

Wakati Wassira akisema hayo, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango naye amekishukia chama hicho akisema maandamano yake hayana nia ya kushinikiza Dowans isilipwe, bali kuhamasisha vurugu nchini.

Kauli hizo za viongozi hao wa CCM, zimekuja siku tatu tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaonya viongozi wa Chadema kwa kuandaa maandamano na kupandikiza mbegu mbaya za chuki dhidi ya serikali.

Rais Kikwete alisema hayo alipokuwa akilihutubia taifa katika hotuba ya mwisho wa mwezi Februari kupitia vyombo vya habari. Chadema kimekuwa kikifanya maandamano na mikutano ya hadhara katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kupinga serikali kuilipa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans pamoja na kuzungumzia ugumu wa maisha.

Waziri Wassira, akizungumza katika kipindi maalumu kilichorushwa juzi usiku na Televisheni ya Taifa (TBC), alisema Chadema hakina haki ya kufikiria kuiondoa serikali madarakani.

"Hawawezi na hawana haki ya kufikiria kuiondoa serikali, hawana hiyo haki. Kikatiba hawawezi na kama itatokea itakuwa ni ukiukwaji wa katiba," alisema Wassira na kuongeza:

"Suala la kuiondoa serikali madarakani halipo na wakitaka mazungumzo, hilo halizungumziki... hatuna chuki na Chadema, lakini tunapingana nao wanapowashawishi watu wawaunge mkono katika yao. Hilo haliwezekani."

Akizungumzia kile Chadema inachosema inachokiita hali ngumu ya maisha, Wassira alisema: "Hali ngumu ya maisha inatokana na mtandao mrefu. Hivi sasa mafuta yako juu, pipa moja linafikia dola 150, sasa wanataka Rais Kikwete aende Uarabuni kusimamia kupanda bei za mafuta?"

"Mafuta ni kila kitu, sasa yakipanda si Tanzaia tu hata mataifa mengine ni hivyo. Hata ukienda China hivi sasa kuna mfumuko wa bei, ni wazi pia hata wanaotumia bidhaa za China, bei itakuwa juu kwa sababu dola imepanda."

Wassira alikishambulia Chadema akirejea kauli ya Rais Kikwete kuwa kinatumia vibaya nafasi na haki yao ya kuandamana kwa kueneza chuki kwa wananchi juu ya serikali yao.

"Dola ina mipaka yake ya kuvumilia. Uvumilivu ukizidi itatumika lakini kama wataendelea kupandikiza chuki, watawahadaa wananchi na kuwatia hofu, wananchi wanataka kuishi bila hofu...wakitaka tukae tuzungumze, bei zinapanda tufanye nini, huku tukidumisha amani."

"Hatuwezi kukaa kimya kuona eti kwa kuwa ni wapinzani wafanye wanavyotaka. Kuna mipaka yake, wakiendelea watakutana na mkono wa dola na wasije wakatulaumu."

Akinukuu vifungu vya Katiba, alisema: "Ibara ya 20 ya kifungu cha Katiba, inampa nafasi na haki kila mtu kukutana na yeyote na kutoa mawazo lakini, si kutumia nguvu kufikia malengo ya kisiasa. "Huku (kutumia nguvu) ni kuvunja katiba na hatutakuwa wavumilivu katika hili."

Wassira amekishauri Chadema kutulia akieleza kuwa watu hawakihitaji sasa kwa kuwa si muda mrefu wananchi wamepiga kura na kila mmoja ameona matokeo.

"Tuliingia wote katika mapambano ya ubunge na urais, zilipigwa kura na wananchi hao hao ndiyo walioamua. Sasa hawa wameshindwa kwa njia ya demokrasia, wanataka kutumia nguvu, hiyo haikubaliki...haikubaliki."

"Sawa, leo wanasema wanaizungumzia Dowans, kwanza iko mahakamani, halafu watakuwa na kipi kipya? Kama huyo Slaa (Dk Willibrod, Katibu Mkuu wa Chadema) siku zote, kampeni zote ameimba Dowans, ufisadi kasema sana lakini watu wakampa kura Kikwete..."

"Tunachotaka ni amani na umoja. Hii ya kusema nguvu ya umma inatoka wapi? Kama nguvu ya umma basi iko CCM kwa sababu wamepiga kura watu milioni tano, CCM wakapata milioni tatu wao (Chadema) milioni mbili, sasa nguvu ya umma ni nani hapa?"

Kwa mujibu wa Waziri Wassira, Serikali haitazuia haki ya mtu au kikundi kuandamana lakini, haitavumilia wanaotumia vibaya fursa hiyo... "Ni wazi Chadema wanatuonyesha wao ni washari, wanawatia hofu wananchi, tunawaambia waache kufanya hivyo.

"Katiba iko wazi, kuna vikao halali vya kuwasilisha yao na zaidi ni Bunge, tena uzuri bungeni unasema unavyotaka ilimradi usivunje sheria, sasa kuwakusanya wananchi na kuwaeleza unayotaka ni kuvunja sheria. "Kuna Sheria ya Usalama wa Taifa, kutangaza kutaka kuiondoa serikali madarakani ni kuvunja Sheria ya Usalama wa Taifa, hapo dola haitavumilia," alisema Wassira.

Alisema wananchi wanataka kuishi kwa amani kwani hawajui vita... "Vita wanayoijua ni ile ya Kagera mwaka 1978 na ilipiganwa katika mkoa mmoja wa Kagera, labda haya mabomu ambayo yamelipuka katika kambi za jeshi kwa bahati mbaya. "Upinzani si vitisho, ni hoja, kama wana hoja wasubiri kikao cha Bunge la Bajeti Juni, waje na mawazo yao, waje na hoja za upinzani lakini si vitisho."

Kauli ya Kilango
Akizungumza na gazeti hili jana, Kilango alitaka chama hicho kisiendelee kupandikiza chuki kwa jamii akieleza hasara yake kuwa ni kuleta maafa na kuua taifa. Alisema inasikitisha kuona viongozi wa Chadema wanatoa kauli za kuhamasisha vurugu badala ya kushinikiza Dowans isilipwe kama ilivyodai awali.

Alisema kama kweli Chadema kinataka Dowans isilipwe, kingeongeza nguvu za wanasheria ili kuhakikisha kesi iliyofungunguliwa mahakamani na wanaharakati inafanikiwa na si kuzunguka nchi nzima kumtaka Rais ajiuzulu.

“Najua ndugu zangu wa Chadema hawataki kusemeshwa lakini, mimi kama kiongozi nimeona ni vyema niwaambie ukweli. Kauli kama kumtaka Rais ajiuzulu hazifanani na lengo la kushinikiza serikali isiilipe Dawans,”alisema.

Aliongeza “Nilikataa, ninakataa na nitakataa serikali ya CCM kuilipa Dowans na si wabunge wa CCM tu, ambao wanakataa hilo, bali hata wanaharakati wa haki za binadamu, lakini kwa nini tutake Rais ajiuzulu badala ya kukazania dai la msingi?"

Alisema Chadema wasifikiri kuwa wao tu ndiyo ambao hawataki Dowans isilipwe, bali huo pia ni msimamo wa wabunge wa CCM katika azimio lao walilolipitisha wakati walipofanya kikao Februari mwaka huu na mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete.

Kilango alisema kuwa ni muhimu Watanzania wakajiuliza kama kweli Chadema kuzunguka kwao ni kwa ajili ya kushinikiza serikali isiwalipe Dowans au la.

Kwa mujibu wa Kilango, kauli zinazotolewa na viongozi wa Chadema katika maandamano yao kama Kikwete ajiuzulu au iwe kama Misri na Tunisia, inaonyesha kuwa nia yao si Dowans isilipwe, bali malengo yao ni kutaka Rais ajiuzulu.

“Katika ulimwengu wa hekima na busara, binadamu yeyote yule angetazamia wote wanaopinga Dowans kulipwa wangeunganisha nguvu pamoja kuwasaidia wale ambao wamelichukua jambo hili kisheria na hasa tukijua wazi kwamba takriban Watanzania wote hawataki kodi zao zitumike kulipa Dowans,” alisema Kilango.

Kilango aliitahadharisha serikali kutopenda kufanya vitu kwa dharura na badala yake iwe inachukua tahadhari katika kutatua matatizo ya kitaifa likiwamo suala hilo la umeme.

Ameishauri kutengeneza mabwawa makubwa yatakayosaidia kuhifadhi maji na kuondoa adha ya kupungua kwa maji katika mabwawa yanayotumika kuzalisha umeme nchini.

“Lazima serikali nayo iangalie hili kwani mfumo wa kuhifadhi maji ya akiba kama uliopo nchini Marekani kule Tenessee, ungeweza kusaidia kipindi kama hiki cha ukame,” alisema.

Alisema gharama inayotumika kukodi mitambo ya dharura kila wakati tatizo linapotokea, zingeweza kutengeneza “Stigller’s gauge” kuzalishia umeme na gharama yake ni dola za Marekani 400 milioni tu.

“Wasiwasi wangu ni kwamba fedha nyingi zinazotumika kwa dharura ambazo zingeweza kutengeneza “Stigller’s gauge” ambayo iko sehemu za Chita katika Bonde la Kilombero,”alisema Kilango.

Mrema naye akerwa

Naye Mbunge wa Vunjo, Augustino Mrema ameonya kuwa kuiondoa serikali iliyoko madarakani bila kufuata njia za kikatiba kunaweza kuzalisha matatizo makubwa na kuliangamiza taifa.

Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) alikuwa akizungumzia hali ya kisiasa nchini hususan maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na Chadema.

Alisema licha ya kwamba hapingi maandamano hayo kwa kuwa yako kwa mujibu wa sheria, yakizidi yanaweza kuing’oa serikali iliyoko madarakani kama ilivyotokea Madagascar.

“Mimi siitetei CCM wala serikali ya Kikwete kwamba wasiondolewe madarakani kwa sababu wao hawana hatimiliki ya kutawala nchi hii, lakini njia za kikatiba zitumike kuwaondoa madarakani,” alisema Mrema na kuongeza:

“Maandamano ya Chadema ni halali lakini, tukiwazoesha watu maandamano kila kukicha tutafikia mahali kama wenzetu wa Misri, Somalia, Libya na Madagascar.”

Alisema ufisadi na matatizo mbalimbali yanayolikumba taifa sasa hayawezi kumalizwa kwa maandamano na kwamba njia za mkato zinaweza kuleta maafa makubwa nchini. Mrema alisema wapinzani wana kazi nyingi za kufanya ikiwamo matumizi ya fedha za umma katika halmashauri na Chadema wanatakiwa kubuni njia mbadala ya kufikisha ujumbe wao huo badala ya maandamano.

“Japokuwa mwaka 1995 niliandamana na kupigwa mabomu lakini, tunajifunza kwa sababu tunaona yanayotokea katika nchi nyingine,” alisema.

Alisema serikali ikiondolewa kwa njia ya nguvu za umma ambayo ni maandamano, vurugu na mambo mengine, itasababisha katiba ya nchi kufa na kuifanya nchi isiwe na katiba.

Huku akionyesha vitabu vya takwimu za hesabu za serikali, Mrema ambaye ni Mwenyekiti wa wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa alisema, wapinzani wamepewa kazi nyingi badala ya kukimbilia kwenye maandamano na mikutano tu.

“Wapinzani tumepewa na Bunge kazi ya kupambana na ufisadi hivyo, tutumie fursa hizo tuwakamate, ufisadi hauwezi kuondolewa kwa maandamano,” alisema.

Alisema kama serikali ikiondolewa madarakani kutakuwa na ombwe la uongozi na jeshi linaweza likachukua nchi wakiona inaingia kwenye migogoro.

Ataka Chadema wakamatwe
Katika hatua nyingine, Balozi wa amani wa taasisi ya Universal Peace Federation, Risasi Mwaulanga ametaka viongozi wa Chadema wakamatwe na kufunguliwa mashitaka ya uhaini kwa kile alichosema kuwa wanavuruga amani ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwaulanga alisema Chadema kinatumia fursa ya maandamano kumkashifu Rais Kikwete kitu ambacho ni uvunjifu wa amani.

“Hakika huu ni uhaini wa wazi ambao Chadema inaufanya, kwani umma unapokasirika na kupata hamasa mbaya, matokeo yake ni kuzigomea sera na kuwafanya wananchi kuacha kushiriki shughuli za maendeleo,” alisema Mwaulanga na kuongeza:

“Mwenyekiti wa Chadema na Katibu wake Mkuu wanapaswa kukamatwa, kufunguliwa mashtaka ya uhaini. Bunge linapaswa pia kutoa onyo kali kwa wabunge. Hali kadhalika, Msajili wa Vyama vya Siasa aangalie vifungu vya Katiba yake kuona uwezekano wa kukisimamisha au kukifuta chama hicho kwa usalama wa Taifa.”

“Vyama vya siasa vina haki ya kuandamana, ila ikitumiwa vibaya itavuruga amani. Kwa mfano, Chadema wanatumia maandamano kumpinga Rais Kikwete, huu ni uhaini kabisa.”

Mwaulanga pia alitumia nafasi hiyo kumpiga vijembe bila kumtaja jina Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa akidai kuwa amekuwa akitumia vyombo vya habari na majukwaa ya kidini kuikosoa CCM huku akitolea mfano kauli yake ya hivi karibuni kutaka mishahara ya watumishi wa umma ipande.

“Sasa mtu unataka wafanyakazi waongezwe mishahara, Rais atazitoa wapi fedha hizo?” alisema Mwaulanga.

Kwa mujibu wa Mwaulanga, kutumia majukwaa ya dini kupinga mipango au upungufu wa Chama na serikali kwa viongozi wa siasa si sahihi hata kidogo.

“Wanapokaribishwa na viongozi wa dini wanachopaswa kufanya ni kupinga mipango mibaya ya shetani kwa binadamu kumuasi Mwenyezi Mungu na siyo kuiponda serikali” alisema.

Habari hii imeandikwa na Ibrahim Bakari, Boniface Meena,Nora Damian na Elias Msuya
Chanzo: Mwananchi 3 Machi, 2011.

Kwa kweli nadhani kuna haja ya kutoa elimu kwa viongozi wote wa CCM ya maana ya siasa za ushindani. Kazi ya chama cha ushindani ni kuipinga na kuikosoa serikali iliyoko madarakani kwa upande mmoja, na kutaka kuitoa madarakani kwa upande mwingine. Kitendo cha Chadema kuandaa na kufanya nchi nzima ni moja ya njia za kuikosoa serikali na kuwashawishi wananchi waiunge mkono. Kitu kingine ni kuwa ibara ya 18 inatoa haki ya uhuru wa kujieleza ikiwa ni pamoja na kudai raisi ajiuzulu kwani wananchi ndio waajiri wake. Sasa hapo Chadema wamefanya kosa gani? Kwa kweli CCM na vitimbakwiri wao wako mtero inabidi choo kiwe karibu.
 
Wewe na wapuuzi wenzako ndio mnahitaji kukombolewa kifikra.

Mmepumbazwa na kuleweshwa pumba za mazezeta, wahuni wa kisiasa.

Mnataka kuleta ustaarabu wenu wa porini katika Tz ???

Kamwe, kamwe kamwe. Wazalendo wa kweli hatutakubali upuuzi huu. Tupo hapa kuilinda tz kwa gharama yeyote.

Mtashindwa kabla hamjaanza, wataka shari wakubwa nyie.

Muda si mrefu hizo fyoko zenu zitawarudia.

Acheni ulimbukeni, siasa haziendeshwi hivyo!!!
Na wewe tunakupuuza tu hatukujibu.
 
Kama Wassira haktaki kumjibu, je mwanakijiji wa kawaida mtamjibu?

Kumbukeni kuwa Wassira ni mtanzania (mwananchi) na akihoji jambo anapaswa kusikilizwa na kupewa majibu kama yao.

Kutokumjibu maana yake ni aidha kudharau mawazo ya wananchi au kutokuwa na majibu.
Ndiyo tumemsikiliza lakini tumempuuza sura ka dume la ngedere.

13wasiraleo.jpg
 
Watu hawa wanaogopa nguvu ya CHADEMA. Ina maana kuwa CHADEMA ndicho chama chenye nguvu kuliko vyote kwa maana kisingekuwa na nguvu ni dhahiri hakuna ambaye angekisikiliza.

Mrema naye asiwe kigeugeu. Alipokuwa akitoa mabovu ndani ya NCCR huku tukiwa tunamsukumia gari, je alikuwa naye anahatarisha amani?
 
Ni mbabe sana yule mkurya, aNAONGEA UTADHANI NDIYE RAIS!
Nimaamuzi mazuri sana kumdharau, ili ajifunze kwamba alipoteza wakati wake, na wenye akili wamemdharau...alaaa!

dah.,kumbe nawe una point za kitoto.dah,anyway acha kuzuga wasira ana bonge la personality WE..anavoongea hata mkapa cha mtoto ,ata likipea nchi hilo linacontrol poa,hatamjibu lakini ajue CDM iko hatarini KUFUTWA KWENYE DAFTARI LA TENDWA,jamaa wanakusanya evidence sasa mkuu mbowe akiona hawawekwi ndani anafikiri wanaogopwa.
hebu HARAKISHENI BASI HIYO PEOPLE POWER nna hamu sana ya kushiriki timbwili la dizaini ya Tripolitania NAONA KAMA MNACHELEWA MMEKALIA MANENO TU ,si kambi za jeshi mwazijua ama?
 
Watu hawa Cwanaogopa nguvu ya CHADEMA. Ina maana kuwa CHADEMA ndicho chama chenye nguvu kuliko vyote kwa maana kisingekuwa na nguvu ni dhahiri hakuna ambaye anmgekisikiliza.

Mrema naye asiwe kigeugeu. Alipokuwa akitoa mabovy ndani ya NCCR huku tukiwa tunamsukumia gari, je alikuwa naye anhatarisha amani?

Mrema yuko kimaslahi sio mtetezi wa wananchi wa Tanzania. CCM wangehofia ufisadi kama wanavyoihofia CHADEMA ufisadi ungekuwa msamiati TZ. Kikwete inabidi abadilike na awatumikie wananchi sio mafisadi na aelewe kwamba watakao muondoa madarakani ni wananchi sio CHADEMA. CCM kumbe madaraka mnayapenda ila kufanyakazi kwa maslahi ya Taifa hamtaki watu wa ajabu kweli nyie.
 
wassira kaamua kudanganya umma eti bei ya pipa la mafuta linakaribia $ 150, wahandishi nao hawafanyi checking wanareport kama ilivyo tu. Vyombo vyetu vya habari vina safari ndefu sana.
Pipa la mafuta sasa hivi ni $ 101.
CRUDE OIL PRICE: Oil | Energy | Petroleum | Oil Price | Crude Oil Charts | Oil Price Forecast

Wasira kasema uongo mwingine tena. Asijishikize kwenye mafuta: mbona Kenya inapaa (according to the World Bank) na mafuta wananunua kama sisi? Muongo huyo!

Vilevile, ni haki ya kikatiba kwa chama cha upinzani kudai serikali ijiuzulu. Kutumia maandamano kudai hivyo ni haki ya kikatiba. Kazi kuu ya upinzani ni: oppose, oppose, depose!

CCM will not be in power much longer. The momentum that is being built by CHADEMA will soon sweep that evil organisation into the dustbin of history. Who could have imagined that a skilled election stealer like Mubarak could have been swept aside in a matter of days?

Mie ningependa Kikwete ajaribu kuhutubia mikutano ya uma. Atazomewa.
The over-exploited, over governed and underserved people of Tanzania might heckle him and even chase him away. Enough is enough.
 
Huyu Wassira wala si wa kumjibu kabisa maana anataka kuendekeza malumbano ili kutupandisha hasira ambapo mwisho itakua ni kumwaga damu. Anajua fika CCM ingefanya kazi nzuri kwa miaka yote ambayo amekua kati ya viongozi wakuu ndani ya serikali ya CCM, wala tusingekua hapa tulipo na umasikini huu na bila hata chembe ya matumaini. Kupanda kwa bei ya mafuta leo isiwe kisingizio cha kushindwa kwao miaka 50 ya uhuru.

Serikali mbovu ya CCM ndio chanzo cha vurugu na kutupotezea matumaini, hata katika maisha ya kawaida familia ya wazazi wavivu/wazembe/wasiojiheshimu/wasiowajibika, mara nyingi watoto hua vibaka. Ni vema CDM wakawasha moto zaidi katika kazi wafanyayo ili kutujengea matumaini zaidi baada ya CCM kushindwa kufanya hivyo - matumaini yanaleta amani na kuepusha umwagaji damu.
 
Wewe na wapuuzi wenzako ndio mnahitaji kukombolewa kifikra.

Mmepumbazwa na kuleweshwa pumba za mazezeta, wahuni wa kisiasa.

Mnataka kuleta ustaarabu wenu wa porini katika Tz ???

Kamwe, kamwe kamwe. Wazalendo wa kweli hatutakubali upuuzi huu. Tupo hapa kuilinda tz kwa gharama yeyote.

Mtashindwa kabla hamjaanza, wataka shari wakubwa nyie.

Muda si mrefu hizo fyoko zenu zitawarudia.

Acheni ulimbukeni, siasa haziendeshwi hivyo!!!

Ajabu na kweli!!! Wewe ndio unajiita mzalendo? Kwa lipi? Inaelekea uelewi maana ya uzalendo!!! Kama uko kazini, niwie radhi kwani lazima utafute unga wa watoto!!!!

Tiba
 
WASIRA: PUMBA, KILANGO: PUMBA, MREMA: PUMBA. Sijaona aloeleza yenye maana.Wananchi tunapata shida ndo mana ata CHADEMA wanapata support ya Watu kwani wanaelekeza mambo ambayo yaweza tekelezeka.Angalieni mfumo wenu wa MBOGAMBOGA(kijani:CCM) ama sivyo shughuli pevu Wananchi tumechoka kudanganywa
 
Hapo Ngoma Inogile. CCM naona wamestukia kitumbua chao kimetiwa mchanga.........

NAWAKUBALI CHADEMA JAMANI KAZI NI MOJA TU KWA SASA.........KKUELIMISHA UMMA TU. Mambo mengine yatafuatia, mwache kikwete na wapambe wake wazidi kuleta za kuletwa badala ya kusoma alama za nyakati............
 
wassira kaamua kudanganya umma eti bei ya pipa la mafuta linakaribia $ 150, wahandishi nao hawafanyi checking wanareport kama ilivyo tu. Vyombo vyetu vya habari vina safari ndefu sana.
Pipa la mafuta sasa hivi ni $ 101.
CRUDE OIL PRICE: Oil | Energy | Petroleum | Oil Price | Crude Oil Charts | Oil Price Forecast

Naomba mwongozo wa spika kuhusu hatua ya kumchukulia Waziri mwandamizi kama Wassira iwapo amtumia madaraka yake vibaya kwa kuudanganya umma wa watanzania.
 
Back
Top Bottom