Wasira asumbuliwa na maandamano ya Chadema

Huyu Wassira a.k.a Tyson ni mpuuzi kwelikweli.

Yaani CCM wanashindwa kuelewa maana ya UHAINI kweeeri mura???
Hivi KUIKOSOA SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI KWA MADUDU INAYOYOTUFANYIA WATANZANIA NI UHAINI KWEERI MURA TYSON???
Hivi kusema kuwa DOWANS wasilipwe ni UHAINI mura?
Kuhoji mambo ya UFISADI,MGAWO WA UMEME,MABOMU YA G/MBOTO,HALI NGUMU ZA MAISHA,KUDORORA KWA UCHUMI WETU ni UHAINI KWEERI MURA???

Mura Tyson hapa umechemka. Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atakayekubaliana na pumba zako hizi. Wewe huna tofauti na M/kiti wako Kiwete aliyekiri kuwa CCM tangu enzi za Mjomba wako Nyerere mpaka sasa mmeshidwa kumaliza matatizo ya Wananchi!

Kwa hiyo CHADEMA wanaposema CCM mmeshindwa kuongoza na hivyo mnapaswa kukaa pembeni msikasirike Mura.
Nakushauri mura Wassira ukakae na Kiwete mpange mikakati ya KUWAONDOLEA KERO WATANZANIA na siyo kupanga namna ya kuwadhibiti CHADEMA. Wananchi wanajua ukweli uko wapi. Kwa hiyo acheni longolongo na siasa za kizamani. Hii ni dunia mpya inayotaka mabadiliko na mageuzi ya haraka ili kufikia malengo na maendeleo waliyojiwekea watu.

Hatutaki ubabaishaji. Wazungu wanamsemo unaosema kwamba,nanukuu,''If you can't stand the heat, get out of the kitchen.'' CCM inaonesha kuwa joto limewalemea, hivyo tokeni jikoni maana hamtaweza kuendelea kuwapikia Watanzania chakula kilichoiva na kitamu. Mking'ang'ania kukaa jikoni mtaendelea kupika vyakula vibichi visivyokuwa na ladha!

Kuikosoa serikali mura sio uhaini na kama mh. Wasira alikusudia kumaanisha hivyo alikosea. Lakini kuipa serikali siku tisa kutekeleza matakwa ya chama cha siasa la sivyo itaondolewa na nguvu ya umma kwa maana yoyote ni maneno yanayoashiria uhaini.
 
unajua viongozi wa tanzania wanajua watanzania wanaogopa sana vita hivyo wamekuwa wakiutumia uoga huo kuendelelea kutawala mfano miaka ya mwanzo ya vyama vingi nakumbuka ITV iliwahi kurusha kipindi siku chache kabla ya uchaguzi kipindi kikionyesha vita ili watu waogope kuwachagua wapinzani eti wataleta vita.haya yanayoendelea ya kina kikwete 'wassira ,sofia ni majaribio ya kutaka wananchi waamini kwamba cdm wanavuruga amani ili wao waendelee kutanua na kuendelea kututawala hata kifkra na kwamba ni lzm tuwachague wao.

Ni kweli watanzania wengi sio tu kwamba tunaogopa vita bali hatupendi vita.

Ndio maana tumejiwekea utaratibu mzuri na wa kistaarabu wa kubadilisha serikali. Kila baada ya miaka mitano kuna uchaguzi mkuu. Bunge ambalo ni wawakilishi wa wananchi linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu hata Raisi kama linaona kuna ulazima wa kufanya hivyo. Vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla wamepewa uhuru wa kutoa maoni na kuikosoa serikali ili mradi wazingatie sheria. Baadhi ya wananchi pamoja na wananchama wa Chadema waliposema kwamba katiba yetu ni kiwazo cha maendeleo na demokrasia, serikali imeridhia kuwepo kwa katiba mpya na wananchi wamepewa nafasi kutoa mapendekezo yao ya namna katiba mpya inavyopaswa kuwa. Katika historia yetu yote hatuna utaratibu wa baadhi ya wananchi wasioridhika na serikali iliyopo madarakani kutumia mabavu kuing'oa hata kama wana nguvu kiasi gani. Nguvu zao zinaweza kuhalalisha kuiondoa serikali madarakani kwa njia ya kura katika uchaguzi
 
Muulizaji Gabriel Zakaria, anayejibu Stephen Wasira. Kama TBC ni darasa basi fahamu gumbaru.

Huyu muulizaji ana sura na umri unaomruhusu kusoma aongeze ufahamu. Lakini naona ni mvivu.
 
Back
Top Bottom