Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,255
Katika hesabu hii kokotoa mtu wako akipata zaidi ya sita ya huu wasifu basi jua yuko hatarini au tayari keshaibwa.............
1) Kama ana hulka ya kuiba basi kurudia inakuwa siyo kazi kubwa kwake...........
2) Kama hana shughuli za kumshughulisha basi kuiba vya wengineo inakuwa nayo ni shughuli inayohitaji mipango na muda wake.........
3) Kama ana moyo wa kuthubutu basi kudokoa humpa changamoto ya kujaribu.............aone kulikoni au hivi anakosa nini kule?
4) Kama ni teja wa kumiminiwa "misifa" basi atanaswa hukohuko....bila ya masihara.
5) Kama anahusudu mali basi wenye nazo watamvuta naye atavutika...............
6) Kama jamaa yake anamwachia mapovu tu na hampandishi vilima vya usambara basi ujue kiu yake itamtuma amtafute yule ambaye atamfikisha atakako kufikishwa...........................
7) Kama ana historia ya kuwa na wengi na hachagui basi baadhi yao "zilipendwa" wakibisha hodi itabidi awafungulie mlango.................wakati mwingine ni kwa ajili ya kukumbushia tu maana kuna kusahau hata ilikuwaje........enzi zao!
8) Kama starehe za bwerere hazimpiti kando basi hukohuko atavuna alichopanda.....
9) Kama kwa vikali ni mwenyewe basi akilegea na masharti atayalegeza.............bila ya zengwe lolote lile...........
10) Kama kila wakati huchangamkia urafiki na wale wa "opposite sex" ujue kuyamaliza pia yawezekana.............
11) Kama ana sababu lukuki za kutokuwa na wewe basi ujue analake jambo........
12) Kama kila wakati hupenda kujibu maswali ambayo hujamuuliza elewa anafukia mashimo huyo ili ukisikia udhani kuwa hakuna ishu maana tayari mwandani wako alikwisha kukujuza........................kumbe ni geresha zake tu za kukuhadaa udhani hakuna ishu kumbe ipo na imechachamaa........
N.B:- wa kwako kama amepata zaidi ya sita ujue uko hatarini......chukua hatua acha kulalamika.........lol