Kwahiyo ile tu kusema "...alikuja Tanzania as a migrant wakati akiwa na miaka 5...!" ndo tayari unaona ulichoongea ni sahihi na kwamba sio wewe ndie uliepotosha?! Akija mwingine akisema alikuja akiwa na miaka 10 utambishia?! Na utambishia kwa kutumia vigezo gani na vigezo gani utamtaka mtu akukubalie wewe uliyesema alikuja akiwa na miaka 5?!Nadhani sasa unaleta Siasa bila sababu. Twaha Khalifani alizaliwa Rwanda na alikuja Tanganyika kama migrant akiwa na baba yake wakati huo akiwa na umri wa miaka 5. Tusipende kupotosha, Serikali ya Mkapa ilim-pin down kwa kuwa kisheria Twaha Khalifani ni munyarwanda, ila ku-quaify uraia wa Tanzania alitakiwa kuwa amekana uraia wa Rwanda, jambo ambalo hadi 2001 wakati wa kunyang'anywa uraia hakuwa ametimiza takwa hilo la kisheria. Stories nyingine ni blah blah tu. Baba yake Twaha alizikwa Kamachumu. Dadake pekee wa Twaha anayeitwa Zainabu ni mjane wa Peter Claver Bakilana (1939-2012) [rip] aliyewahi kuwa CEO wa THA (sasa TPA), TRC (sasa TRL) na NTC. Twaha huwa haendi kwao kamachumu kwa sababu shamba la babake aliliuza.
Maandiko mbalimbali yanaonesha Jenerali Ulimwengu alizaliwa Ngara mwaka 1948. Pambazuka, hawa hapa:
Mtandao wa Suffrage-Universel unaripoti:JENERALI ULIMWENGU was born on 4th April 1948 in Ngara, Kagera Region of Tanzania. He went to school in Kamachumu, Katoke and Nyakato in Kagera and high school in Tabora from 1955 to 1968 and was a student of the then University of East Africa from 1969 to 1972.
Mimi nimetoa reference 2; nakuomba wewe utoe reference MOJA TU hata kama credibility yake inatia shaka... source inayosema Ulimwengu aliingia Tanzania akiwa na miaka 5!!!!According to the lecturers' memorandum, distributed to different organisations and media houses, Mr Ulimwengu was born in Ngara district on April 4, 1948, and went to school in Kamachumu, Katoke and Nyakato in Kagera region.
Remember, kwenye post za siku za nyuma ulisema ulimfahamu Ulimwengu Nyakato wakati akiwa sekondari!
Kwa maana hiyo, ni kwamba hufahamu utoto wa Jenerali Ulimwengu na kwahiyo; kama unasema alikuja akiwa na miaka 5 ni lazima itakuwa ni habari ya kusikia!For those of us who know him well right from Nyakato Secondary School to the University of Dar es Salaam, Ulimwengu is nothing but an accomplished exhibitionist opportunist whom no normal-minded person can trust - so his opium-orchestrated opinion.
Weka source yako hapa!!!!
Kwamba, serikali ya Mkapa ilim-pin down kwa sababu alikuwa Mnyarwanda.... unataka kuniambia kwa zaidi ya miaka 6 ya mwanzo ya uongozi wa Mkapa haikufahamu kwamba Jenerali ni Mnyarwanda lakini ikaja kufahamu pale alipoanza kuandika makala za kuikosoa serikali yake?! Au angeendelea kuishi kama "mhamiaji haramu" endapo tu asingeiandika vibaya serikali?!
By 2001, Ulimwengu alikuwa na umri wa +50 years. Na hata tuki-assume maelezo yako kwamba ni kweli aliingia akiwa na 5 years; ina maana aliishi 45 years akiwa "Mhamiaji Haramu" na wakati huo alikuwa tayari kahudumu serikalini na bado hawakujua kwamba si raia?!
Ni nini kiliupumbaza serikali isichunguze uraia wake kwa miaka yote hiyo lakini ikaja kuchunguza uraia wake wakati ameshakuwa mzee?!
Kwamba mengine yote ni blah blah.... ukweli ni kwamba blah blah ndo hizo unazoleta wewe!!!