Umeacha mambo ya msingi sana kuhusu Jenerali; ama kwa makusudi au kwa kutofahamu historia yake vizuri!!!
Kwamba, pamoja na Unyarwanda wa Jenerali/Twaha Ulimwengu (Twaha Ulimwengu or Jenerali Uimwengu) ambao ulioneshwa na serikali ya Mkapa lakini Mzee Khalfani Ulimwengu; Baba mzazi wa Jenerali/Twaha Khalfani Ulimwengu alikuwa ni mmoja wa watu walioheshimika sana miaka ya 1940's huko Mkoa wa Ziwa Magharibi; nchini Tanganyika!!!!!
Likewise, huyu Jenerali/Twaha Khalfani Ulimwengu, nae alizaliwa Tanganyika hii hii huko Ngara na kusoma Tanganyika hii hii ambapo, eilimu yake ya awali aliipatia Kamachumu na middle school Katoke tangu miaka hiyoooo... hata kabla ya uhuru!!!
Hata elimu ya sekondari, aliipatia Tanzania hii hii huko Nyakato na Tabora Boys kabla hajaenda JKT na hatimae UDSM!!
Lakini pamoja na yote hayo, miaka 54 baadae ndipo serikali ya Mkapa ikamuona eti sio Mtanzania!!!!!
Bado nina kumbukumbu ya Makala ya mwisho kabla Ulimwengu hajapigwa ban!!! Heading ya makala ile ilisomeka: Akina Jefferson na Magazeti!!
Kwamba, hapo kabla Rais Jefferson wa Marekani alijifanya ni mpenzi kweli kweli wa magazeti kwa sababu tu walikuwa wanamwandika vizuri! Lakini magazeti yale yale yalipoanza kuandika mabaya ya serikali ya Jefferson, Rais Jefferson akageuka kuwa mbogo na mkali kweli kweli dhidi ya magazeti!!!
Hivi ndivyo Mkapa alikuwa!! Mwanzoni alijifanya ni rafiki wa media jambo ambalo watu halikuwashangaza kwa sababu nae alipata kupitia huko hapo kabla! Lakini media zilipoanza kuandika maovu ya serikali ya Mkapa; Ben akageuka kuwa mbogo.... AKINA JEFFERSON NA MAGAZETI!!