Washauri wapya

Tatizo sio ushauri tatizo ni ufisadi na wizi. Hao jamaa watakachokuja kushauri ni kuwa viongozi waache wizi na ufisadi, na wakisema hivyo watapewa siku moja kufungasha na kuondoka na mchezo ule utaendelea palepale. Ni vizuri tuki-import mawaziri, makatibu na wakurugenzi, maana huko ndio kumeonekana kuwa na mafisadi, na ni huko ambako kuna loop holes za ufisadi.
Na kama lengo ni kuleta efficiency, kama hao jama wanaweza kukubali hata kututafutia rais itakuwa bomba tu, bora atuletea maisha raha na mazuri.
Kwa ufupi ni wazo la kujinga kuleta mtu ambaye hajyui utamaduni wako wala situation yako kuja kukushauri!

Ufisadi na wizi hauna kabila wala taifa. EL? NK?
 
Kaka Fundi,

kwenye ile mada ya MKJJ "R&D" nilisema DR. James Watson alikuwa sahihi kuhusu sisi waafrika,sasa Rais wetu anapoamua kuleta "washauri" wa uchumi na kuendesha nchi unataka kuniambia nini tena?Niambie ni lini China,India,Malaysia,Korea Kusini,Latin America in general (sihitaji kuongelea Europe and North America) walihitaji washauri wa namna hii kufika walikofika?Je pale Mlimani UDSM kuna wale watu wanaojiita "maprofesa" na "madokta" mabingwa wa uchumi, sayansi ya utawala/uongozi,tech,engineering, etc ambao kazi hii imewashinda/ingewashinda?kwanini JK aamue kuwaita hawa wazungu na huyo mjapani waje kwetu?

Je hatuna "maprofesa" na "madokta" katika serikali hii mpaka tuagize hao watu?Dr.Ballali alikuwa nani?Professor Msolla alikuwa nani?Dr. Ngasongwa alikuwa nani?Prof. Kapuya ni nani?Prof. Maghembe ni nani?Prof. mwakyusa ni nani?
tuna wabunge,manaibu mawaziri na makatibu wakuu wa wizara wangapi ambao ni "madokta" na "maprofesa"?Je ndo wameshindwa kabisa kufanya hayo mambo mpaka wageni waje?

Was James watson wrong?

Mwanakijiji na Koba hebu mnisaidie hapo kaka zangu.
 
Hivi tunaweza kuwa na Makatibu wa Kuu toka Ulaya maana ndio watendaji wizarani?

Nakuambia tunakoelekea ni kule kule kwa aliyosema Ian Smith wa Rhodesia kuwa waafrika hawawezi kujitawala au kutawala yeyote bila msaada wa wazungu na naona Kikwete na serikali yake ya ccm ndiko wanakoelekea.
 
Tony Barclay wa DAI management atatusaidia sana akikabidhiwa management ya TRA, anauzoefu katika nchi za africa na anaushawishi mkubwa katika jumuia za kimataifa. DAI management ndio iliyoitoa NMB icu.
 
Kaka Fundi,

kwenye ile mada ya MKJJ "R&D" nilisema DR. James Watson alikuwa sahihi kuhusu sisi waafrika,sasa Rais wetu anapoamua kuleta "washauri" wa uchumi na kuendesha nchi unataka kuniambia nini tena?Niambie ni lini China,India,Malaysia,Korea Kusini,Latin America in general (sihitaji kuongelea Europe and North America) walihitaji washauri wa namna hii kufika walikofika?Je pale Mlimani UDSM kuna wale watu wanaojiita "maprofesa" na "madokta" mabingwa wa uchumi, sayansi ya utawala/uongozi,tech,engineering, etc ambao kazi hii imewashinda/ingewashinda?kwanini JK aamue kuwaita hawa wazungu na huyo mjapani waje kwetu?

Je hatuna "maprofesa" na "madokta" katika serikali hii mpaka tuagize hao watu?Dr.Ballali alikuwa nani?Professor Msolla alikuwa nani?Dr. Ngasongwa alikuwa nani?Prof. Kapuya ni nani?Prof. Maghembe ni nani?Prof. mwakyusa ni nani?
tuna wabunge,manaibu mawaziri na makatibu wakuu wa wizara wangapi ambao ni "madokta" na "maprofesa"?Je ndo wameshindwa kabisa kufanya hayo mambo mpaka wageni waje?

Was James watson wrong?

Mwanakijiji na Koba hebu mnisaidie hapo kaka zangu.

Ibabambasi,

Watetezi wa ufisadi na ukoloni kama Dar es salaam (memba wa JF) watakuambia kuwa kwa vile Nyerere (miaka 45 iliyopita) alikuwa na msaidizi wa kizungu basi na watanzania leo wanahitaji msaada wa wageni kuendesha nchi yao.
 
Mi naamini MMK kuna nchi za kiafrika zinazohitaji maraisi toka Ulaya, achilia mbali hao makatibu wa wizara.

na kama mwendo ndio huu basi kuna haja ya wananchi kujiandaa kufanya vita ya mapinduzi ya kuuondoa ukoloni maana naona wenzetu sera yao (ccm) ni kurudisha ukoloni kwa mara nyingine huku wakiusifia.
 
Ibabambasi,

Watetezi wa ufisadi na ukoloni kama Dar es salaam (memba wa JF) watakuambia kuwa kwa vile Nyerere (miaka 45 iliyopita) alikuwa na msaidizi wa kizungu basi na watanzania leo wanahitaji msaada wa wageni kuendesha nchi yao.

Dada Mwafrika heshima kwako,

hebu muulize huyo Dsm atueleze mazingira yaliyosababisha Nyerere kuwa na mshauri wa kizungu enzi hizo na huyu JK kuwahitaji watu hao kwa sasa,pia mkumbushe DSM asome lile tamko la Nyerere wakati anakifungua UDSM na kusomesha "wasomi", alisema wasomi ni kama wamepewa chakula katika nchi ya njaa ili waende wapi kufanya nini?je ni lazima kuwa na washauri hawa wakati "wasomi" tunao?Je niwasomi wa "kubumba" (feki kwa maana ya wakazi wa kanda ya ziwa)?what a shame on DSM/huyo mtu anazidi kuprove how damn right Dr. Watson,Ian Smith na wazungu wengine wanavyotuona sisi wesusi...so angry grrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!

Ah ngoja nikapoze tu frustrations zangu na mafisadi hawa kwa kutazama Ze Comedy who are doing far even better than the so called intellectuals of TZ katika kuwaamsha wadanganyika na waetezi wa mafisadi kama huyu jamaa Dar es Salaam.
 
Ufisadi unajigeuza sura-hii ni hila tu.Msingi wa matatizo yetu ni ufisadi sio ushauri mbovu au kukosa ushauri.Hapana. Sasa ni mbinu mpya ya kuhamisha fedha kwa kushirikiana na hao wanaoitwa washauri.
Kwanza Ngurudoto ni ya nani hata iuwe taasisi ya serikali ya mikutano ya kimataifa ya AICC iliokaribu na Ngurudoto.Je hivi serikali gani safi inayoweza kuhamisha kwa makusudi mikutano kwenye taasisi yake na kupeleka mapato kwa mtu binafsi?Chunguzeni limo FISADI kubwa tena.Hatutaki,TUMECHOKA WATANZANIA KUIBIWA.SERIKALI INAFANYA NINI??
 
Dada Mwafrika heshima kwako,

hebu muulize huyo Dsm atueleze mazingira yaliyosababisha Nyerere kuwa na mshauri wa kizungu enzi hizo na huyu JK kuwahitaji watu hao kwa sasa,pia mkumbushe DSM asome lile tamko la Nyerere wakati anakifungua UDSM na kusomesha "wasomi", alisema wasomi ni kama wamepewa chakula katika nchi ya njaa ili waende wapi kufanya nini?je ni lazima kuwa na washauri hawa wakati "wasomi" tunao?Je niwasomi wa "kubumba" (feki kwa maana ya wakazi wa kanda ya ziwa)?what a shame on DSM/huyo mtu anazidi kuprove how damn right Dr. Watson,Ian Smith na wazungu wengine wanavyotuona sisi wesusi...so angry grrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!

Ah ngoja nikapoze tu frustrations zangu na mafisadi hawa kwa kutazama Ze Comedy who are doing far even better than the so called intellectuals of TZ katika kuwaamsha wadanganyika na waetezi wa mafisadi kama huyu jamaa Dar es Salaam.

Pole sana mwenzangu. Slow down maana haya mambo yanaweza kupasua kichwa chako (hasa yanapofanywa na watu waliosoma kama maprof na madokta kwenye serikali ya Kikwete).
 
Some body please stop me from thinking and reading JF, I want to live a life!!

I hear you loud and clear my brother. This thing can ruin lives. For real.

Mkjj:
Nimepata fununu pia, kwamba mipango inakamilishwa na serikali kuwaleta wananchi kadhaa wa huko Netherland watakaosambazwa vijijini kusimamia mipango ya maendeleo ya wananchi. Haya yote yatakapokuwa yamekamilika, sina shaka Tanzania tutakuwa tumeondokana kabisa na matatizo ya umaskini wetu huu.
 
Hivi nani aliyewaambia kwamba tatizo letu ni kukosa washauri? Ni tafiti ipi inayoonyesha kwamba tukipata washauri wa kigeni (Wazungu& Waasia) tutapata maendeleo?

Kidonda cha city water na Net group solution bado hakijapona!!!
uumh kichwa cha mwendawazimu, kila mtu anajifunzia kunyoa, anayekosea anakiacha ili mwingine aendelee kujifunza.

JK vipi?
 
I hear you loud and clear my brother. This thing can ruin lives. For real.

Mkjj:
Nimepata fununu pia, kwamba mipango inakamilishwa na serikali kuwaleta wananchi kadhaa wa huko Netherland watakaosambazwa vijijini kusimamia mipango ya maendeleo ya wananchi. Haya yote yatakapokuwa yamekamilika, sina shaka Tanzania tutakuwa tumeondokana kabisa na matatizo ya umaskini wetu huu.

Kalamu nadhani hilo pia ni kweli maana wanaamini kwamba tukichanganya "wananchi wa kizungu" na wa "kiafrika" basi kuna kauwezekano kuwa wananchi wetu na wenyewe "by osmosis" wataweza kupata hali ya kuwajibika na kupenda kudumisha vitu vizuri. Kwa vile huko nyuma Nyerere aliwahi kuwa na msaidizi Mzungu (was it mama Robinson?) ni vizuri sasa kila kijijini kitenge eneo kidogo la kukaribisha wazungu watuoneshe jinsi ya kuishi "kizungu"..
 
Kuna mtu hapa anaweza kusema Ian Smith alikuwa wrong? hebu angalieni Mugabe anavyofanyia watu wake. Tanzania tunahitaji kuwa na timu ya consultants kutoka nje kwa kila wilaya. Nadhani bora lawama kuliko fedhea.

Leo hii nimesoma thread moja hapa JF kwamba wale wanachi waliondamana kufurahia kuaporomoka kisiasa kwa Dr. Ngasongwa sasa hivi wanasakwa ili wakamatwe na kujibu mashtaka ya kumdhalilisha mbunge wao. DC anayefanya hiyo shughuli ya kamata kamata ni Dokta. Sasa ebu niambieni watu wenye upeo kama huo ndio wanakuwa viongozi wetu, unategemea nchi itaendelea kweli?

tunahitaji kusaidiwa tangu wizarani hadi wilayani
 
Ni wapi tunaweza kupata washauri wa kizungu ambao wana rekodi nzuri na watatusaidia kuendesha vitu kama Benki Kuu n.k.. sitaona ubaya hata tukiomba washauri wa Usalama wa Taifa...

China. Kwa nini kwenda kwingineko na huku hawa ndio 'hot' wa wakati huu!

Afterall, wapo wengi, na tukitaka kila mTanzania (40mil. of us) tutapata mwambatani mmoja mmoja.
 
Kuna mtu hapa anaweza kusema Ian Smith alikuwa wrong? hebu angalieni Mugabe anavyofanyia watu wake. Tanzania tunahitaji kuwa na timu ya consultants kutoka nje kwa kila wilaya. Nadhani bora lawama kuliko fedhea.

Leo hii nimesoma thread moja hapa JF kwamba wale wanachi waliondamana kufurahia kuaporomoka kisiasa kwa Dr. Ngasongwa sasa hivi wanasakwa ili wakamatwe na kujibu mashtaka ya kumdhalilisha mbunge wao. DC anayefanya hiyo shughuli ya kamata kamata ni Dokta. Sasa ebu niambieni watu wenye upeo kama huo ndio wanakuwa viongozi wetu, unategemea nchi itaendelea kweli?

tunahitaji kusaidiwa tangu wizarani hadi wilayani

Huu unaweza kuwa ni ukweli lakini kuna tofauti gani kati ya ukoloni na unachosema?
 
Ni vizuri serikali ikafanya utaratibu wa kuwatafutia makazi hawa wataalamu katika sehemu kama hizi...

Josiah+Manzese.jpg

Manzese+6.jpg

BongolandIIpic7.jpg

...Kwa kuishi ktk mazingira kama haya, pengine wanaweza kutoa ushauri mzuri wa ku"manage"rasilimali zetu
 
Tatizo Tanzania sio kwamba hatuna ushauri, tatizo ushauri haupokelewi.Tumeona hili kwenye Richmond na sehemu nyingine.Swali ni kwamba wakija washauri wa nje wakashauri objectively lakini wakiwaambia wanasiasa wasichotaka kusikia wanasiasa hao watakubali au ndiyo mambo ya kuwa-pressure yataanza? That is if the external advisors will be objective at all.
 
Mfa maji haishi kutapatapa.

Wataalam tunao, tena wengi wamejaa kila kona ktk nchi yetu, tatizo ndugu zanguni ni ngozi yetu nyeusi hivyo na mawazo yetu ni meusi pia. sisi tunaaofanya kazi na weupe tunayaona haya. mawazo yetu hata kama ni ya maana hayasilikilizwi.

Inasikitisha sana sasa kuona serikali yetu nayo yenye watu weusi kama sisi kugeukia kule kule tulikokukataa enzi za kutafuta uhuru. Labda tulikurupuka kudai uhuru, labda tulikuwa hatujastaarabika bado. kama hivyo ndivyo haya na tuwarudishe tena hao wakoloni waje watufunze upya.

Hili la Ngurudoto ???? (Nasikia redio mbao zikimtaja BWM kama mmiliki) wanampa tafu mzee na kuifisadi AICC
 
Back
Top Bottom