Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,756
- 40,930
Serikali ya Tanzania inadaiwa iko mbioni kuleta washauri wapya wa Ikulu na Wizara mbalimbali. Washauri hao toka nchi za Scandinavia wanatarajiwa kuingia nchini wakati wowote ili kusaidia kutoa ushauri wa kuendesha Ikulu na Wizara mbalimbali.
Baadhi ya washauri hao wamewahi kufanya kazi na viongozi mbalimbali wa mataifa ya magharibi wakiwemo Mawaziri Wakuu, Marais na katika taasisi mbalimbali za Kimataifa.
"Unajua nchi yetu tumekuwa na matatizo katika uendeshaji wa mambo mbalimbali, na tumeona kuwa tusione haya kuomba ushauri wa kuendesha Ikulu" alisema mmoja wa watu ambao wanajua juu ya mpango huo.
"Huyu mjapani aliyekuja kutoa ushauri kwenye mambo ya viwanda ni mwanzo tu" alisema afisa huyo wa ngazi zajuu aliyekataa kutajwa jina lake kuwa si msemaji wa serikali.
Mtaalamu mwingine aliyeunga mkono mpango huo alisema kuwa "hatimaye serikali mefanya kile ambacho watanzania wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu; kutafuta ushauri kwa watu wasio na maslahi binafsi".
Mpango huo wa kuleta wataalamu wa kuendesha serikali toka nje endapo utafanikiwa inadaiwa utafuatwa na nchi nyingine mbalimbali za kiafrika zenye migogoro ya ndani. Baadhi ya nchi zinazofuatilia mpango huo wa Tanzania ambao umebatizwa jina la "Rent a Leader-Lend a Hand Project 2008" unaungwa mkono na Watanzania wengi hasa baada ya viongozi wengi wa kizalendo kuonekana kuwa ni wabangaizaji ambao miaka zaidi ya 45 baada ya uhuru hawajajua jinsi ya kuongoza nchi.
Semina ya kwanza itakayoendeshwa na wataalamu hao ili kuweza kujua kiini cha tatizo la uongozi nchini, inatarajiwa kufanyika kwenye Hoteli ya Ngurdoto, Mkoani Arusha mapema mwezi wa nne.
Habari hizi hata hivyo hazijathibitishwa na kiongozi yeyote wa serikali kwani hadi tunakwenda mitamboni hakuna hata mmoja aliyeweza kupatikana kwa sababu sikumtafuta.