KWANZA KABISA
Mkuu, ninaomba utambue kuwa kuna aina kadhaa za nyimbo.
kuna wimbo wa kuelimisha, wimbo kama huu hutoa mafunzo mbalimbali juu ya yanayoendelea katika jamii, mfano starehe Ferooz
kuna wimbo wa Kufurahisha/kuburudisha huu ni wimbo ambao hauna maudhui ya kutoa fundisho ila ni inaburudisha hadhira, mfano kanyaga ya mond,nyegezi nk
kuna wimbo wa masikitiko, huu ni wimbo unaotokana na jambo fulani la kusikitisha kwa mfano ule wa Mond na Mjomba kuhusu yale mabom ya mbagala
Mkuu, ninaomba anza kutambua aina ya wimbo huo kabla ya kuutolea maoni mabaya,
halaf wasanii wengi wanadesturi ya kutarget Hadhira wao, yaan wanatoa wimbo huu ili kusudi wakiwa kwenye show ndyo wimbo wa amsha amsha ya mashabiki pale jukwaani.
Mkuu, ninaamini sijakukera.