Wasabato ujumbe wenu huu hapa

Status
Not open for further replies.

Mnafiki ni wewe farisayo wa kisabato usiyeyafahamu maandiko. Warumi 10:9 inasema nini kuhusu kuokoka? Ok kama hufahamu hili soma zaburi 16:3 inasemaje kuhusu watakatifu walioko duniani? Ndio maana Paulo akaandika habari hizi mapema kwenye
2 Timotheo 3:5 , " wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao." kuwahusu watu kama nyie mnaojidai mnamjua KRISTO huku mkikana nguvu zake yeye. Narudia tena usabato ni dini ya kishetani yenye kujificha chini ya mwavuli wa BWANA YESU.Okokeni leo maana neema ipo bure.
 
Wasabato si ndo wale wanaotaka kwenda marejani kuhubiri bila visa,pasport tena bila nauli.?

Kanisa la kweli ni katoliki tu,mengine makelele tu.

Marejani ndo kule anakoishi mungu wenu papa??
 

Kuna tofauti kati ya neno UTAOKOKA na UNAOKOKA,katika warumi 10:9 imesema UTAOKOKA that's means ni future tense

Pia neno linasema atakayevumilia mpaka mwisho Ataokoka...wokovu 2lionao kwa sasa ni ule wa kifo cha Yesu ambayo ni NEEMA tu ambayo kila mwanadamu anaipata

Barikiwa
 
Mtoa mada mwenyewe anaonekana ni msabato so yuko akifanya ile research ya namna ambavyo wasabato vile wanaeleweka katika society thats why baada ya kutoa mada ka-run away bila ku-turn back
 
Swali zuri na lina majibu mengi, lakini niongee kidogo.
Huyo Yesu ingawa alikuja kimwili kabisa hawakumwamini hats kipindi hicho,na walimuita mchwawi soma
Yohana 9 yote na hii yote ni ile miujiza aliyotenda.
Sisi tunaitaji mafundisho zaidi na nguvu zaidi kwani Yesu ilitabiri maajabu zaidi baada yake.
Hebu soma habari za Yesu na Thomas utajua suala la imani hata kwa wale waliomona kwa macho na kushuhudia miujiza yake hawakumwamini.
Mimi na wewe bado tunajifunza tu
 
Zipo lakini niliamua kutumia hiyo ya kiingereza maana hiyo inawezekana ku copy na ku paste wakati za kiswahili haiwezekani(kwa zile nilizonazo).

Zipo zinazowezekana

Unatakiwa ujue kuwa ujumbe unaouweka hapa ni wa watu wa kawaida kabisa ambao wengi wao hiyo lugha ni tatizo

Hivyo ni bora ukawawekea lugha ambayo wanaifahamu vyema

Halafu kutumia lugha ya watu wengine ni wakati yako ipo sio sawa kabisa

Hii hapa na utaweza kukopi: http://www.wordproject.org/bibles/sw/
 

Kwanza hata Yesu mwenyewe alishasema Aaminiye na kubatizwa ataokoka sasa kama umeshamkiri Yesu na ukabatizwa yanini usite au ukatae wokovu.
 

Asante. Ila natamani utafakari sura nzima ya 10 ya warumi, na uielewe. Ukianzia tu mstari wa kwanza utaona maombi ya Paulo juu ya watu wenye mfano kama hawa wasabato. Wokovu ni leo/sasa haijalishi kwamba utakufa lini, soma hili neno Yohana 5:24. Je hapo inakuwaje? Na tena soma hili waebrania 9:27. Yote ni kuthibitisha kuwa wokovu ni duniani na si mbinguni. Ningependa pia usemee zaburi 16:3 uone ukweli wake. Karibu katika wokovu neema bado ipo bure.
Asante.
 

nimekuelewa kiasi kwa uliloandika, ukipata wasaa jibu swali zima, likiwa na nyongeza ya dodoso uliyotoa litakaloonyesha kwa nini Yesu hakufanya ubatizo wa japo kundi dogo, japo alitabiriwa kwamba atabatiza.
 
Nitakutajia kwa uchache kwani tunajua kwa kiasi.
1.Mombi 2.Utakatifu na Haki
1.Unaweza ukawa muombaji mzuri sana ila nafsi yako imejaa madhambi kibao,dhambi sio lazima ufanye uonekane zipo dhambi kibao unatenda kwa nafsi,mpaka hapo Mbingu itaiona kwa kushika KWELI na sio maombi.
2.Utakatifu unatokana na kuishika KWELI
3.Haki ulikwisha kuhesabiwa iwe kwa mema au maovu..
 
Asante kwa majibu yako!

Je wasabato wanaabudu Siku au wanatambua Kua Siku zote ni za Bwana? Au wanamuabudu Yule alieziumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo na chemichemi za Maji?

Sio.siku zote ni za Bwana, bali siku sita alizitumia katika kuumba, kisha akachagua siku moja ya kukumbuka na kupumzikia uumbaji wake, ndio maana Yesu anasema yeye ni Bwana wa sabato.
 

Mkuu kabla sijaingia kwenye kukujibu hoja yako kwa kirefu naomba unijibu hili swali

Kabla ya Yesu kuja duniani Torati ilikuwa imehubiriwa sehemu nyingine za Dunia tofauti na Israel?
 
Teh teh teh tuwasubiri wenye dini yao... Ila me najiulizaga tu hivi wale Mitume walikuwa dini gani na Yesu mwenyewe je? Na wazazi/Walezi wake walikuwa dini gani.. Na hivi Mitume,manabii na Yesu mwenyewe walukuja kuleta dini?

Nimerudi mkuu. Yesu mwenyewe alisema hivi Msidhani nalikuja kuleta amani duniani, la sikuja kuleta amani bali upanga. Na pia akasema Nalikuja kumfitini mtu na ndugu zake. Na sehemu nyingine akasema alikuja kuleta mifarakano duniani. Yesu alikuwa anaabudu katika masinagogi na bila shaka alikuwa katika dini ya kiyahudi(lakini sijui kama alikuwa dhehebu la mafarisayo ama masadukayo). Lakini nadhani alifuata dhehebu la mafarisayo(maana waliamini katika uwepo wa malaika, na ufufuo wa wafu).
 
Sema nilitumia lugha siyo ila nilimaanisha ulikuwa sahihi ila Pomoja na hayo kuna Mengi yakupasayo baada ya kuokoka au kumpokea Bwana Yesu kuwa Bwana na mwokozi wako.Ndio nikakutajia hayo matatu.
Nikimaanisha maisha ndani ya wokovu
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…