Rosemerie nimeiona jazba katika ujumbe wako sasa hapa unanipa shida kukuelewa kuhusu huyo roho mtakatifu aliyekujaza. Anyway nimeona bora nikusaidie kwa maelezo haya:
Siyo vyema kuelekeza HASIRA zako kwa Wasabato maana wao wanapoongea na kusoma biblia wanafanya kwa tafakuri kubwa sana, hivyo ulitakiwa kuwajibu kwa ANDIKO kama kweli umejazwa na Roho Mtakatifu. Hebu tuangalie ulipojenga thread yako: Kujazwa na Roho Mtakatifu/upako na kuongea/kuomba kwa lugha.
Dadaangu maandiko yanasema hivi:
Matendo 2:1-11
[SUP]1[/SUP]Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja,[SUP]2[/SUP]kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliokuwa wameketi.[SUP]3[/SUP]Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.[SUP]4[/SUP]Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine kama Roho alivyowajaalia kutamka.[SUP]5[/SUP]Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu wataua,watu wa kila taifa chini ya mbingu.[SUP]6[/SUP]Basi sauti hii iliposikiwa, makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.[SUP]7[/SUP] Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya?[SUP]8[/SUP]Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?.....
Sasa ukirejea fungu la 3,4 utaona kwamba ni kweli walipojazwa na Roho Mtakatifu walijaaliwa kuongea lugha tofauti.
Fungu la 5-8 linakuelezea makabila au lugha tofauti zilizotumika kule Yerusalemu ambazo kila mmoja wa kabila au lugha zile aliweza kusikia kile kilichonenwa na hao mitume katika lugha yake! Ndiyo maana walishangaa wakisema hawa si ni kabila ya galilaya sasa mbona wanaponena tunawasikia kwa lugha yetu? Ukiendelea mafungu yanayofuata hadi la 11 kumetajwa maeneo yote na kabila zote zilizohusika pale. Maana ya unenaji wa lugha hizi si kupiga kelele kwa maneno yasiyoeleweka kwa kisingizio cha upako mtakatifu. Roho Mtakatifu anapomjaza mtu anayenena kwa lugha si kwamba yule mtu aliyejazwa ataongea maneno au lugha isiyoeleweka la hasha!! Nia hapa si kuongea maneno tu ila ni kufikisha ujumbe kwa wasikilizaji. Sasa huyo roho anapokujaza kuongea maneno/lugha isiyo eleweka anakuwa anamfundisha nani?
Mitume walipojazwa Roho Mtakatifu walitumia lugha ambazo hawakuwa wamejifunza hapo awali lakini zilieleweka kwa wale makutano.
Tujaribu kutofautisha kati ya mtu aliyejazwa na Roho Mtakatifu na yule aliyejazwa na roho mtakafujo!!!