Warioba Anataka Nini Hasa?

Warioba Anataka Nini Hasa?

Mleta mada, nimesoma bandiko lako lkn sikumaliza, uneishia kumtuhumu Warioba kama CCM wanavyofanya. Umeshindwa kujenga hoja, mbaya zaidi, umeshindwa kujibu hoja za Warioba hata moja! Warioba, ameshajibu hoja zenu zote, na akauliza maswali saba ambayo si Jk, Pinda, Shein, wala Dk Migiro na wajumbe wote wa BLMK ambaye amejibu hata swali lake moja.

Tangu lini mwana ccm akawa na uwezo wakujenga hoja? Hao ni vichwa panzi wamekaririshwa na mwenyekiti wao. Kuanzia Lumumba mpaka kule chamwino dodoma hakuna mwenye akili na uwezo wakujibu yale maswali7 ya warioba.
 
Unajua neno Ilala asili yake ni nchi gani?Limetokea Malawi lakini mbona tunalitumia kama jina la moja wapo za Wilaya za Dar esa salaam

Huu ni uwongo Ilala ni kifupi cha la ila ilala wa wasiojua wakapaita ilala lakini ni kifupisho cha neno lefu na ilimaanisha zamani maeneo ya boma kuja mpaka karibu na buguruni ni sehemu iliyokuwa makazi ya waarabu na wasomali na waswahili.
 
Kisoda Hakuna aliyesema Tume iwahoji watu wote Acha Akili Za Pumba! mnadanganya watu tu!
Watoe HESABU SAHIHI KWA HAO HAO WALIOHOJIWA BAASI!
Walihoji Watu 371000 wote kama Muundo wa Muungano ungekuwa ni Tatizo la KIKATIBA wangeuzungumzia tuuu, UHURU huo walikuwa nao NDIO kuwa Hawakuuzungumzia Ina Maana Kwao Haukuwa Jambo la Kusumbua Akili AMA Kikwazo Kwao !
Iweje Leo watu 17000 waliotoka Serikali 3 Kati ya 371000 na zaidi ULIOWAHOJI UTWAMBIE ETI NI ASILIMIA 60% HESABU ZA KIMWINYI hizo kama alilosema NYERERE 1+1=3

Nyie mnaotaka serikali mbili mmewahoji wangapi na hesabu zenu ziko wapi?
 
Siku zote ulikuwa wapi toka alipowakilisha.hayo maoni ya watanzania?wote ni watanzania na tupo tanzania sasa usilete hoja zako baada yakusikia mijadala ya watu huko nnje
 
Kabla hujaandika yote hayo ungejibu kwanza maswali yake saba vinginevyo usitafute huruma ?
Unajua watanzania ndivyo tulivyo. Mtu akizungumza ukweli anaonekana mbaya. Hivi Warioba kaongea nini kibayaaaaaaaa jamani. Hivi kama usemavyo mbona hata akina NAPE, Le mutuzi na huyu diwani hawajibu hoja zake ipasavyo? Wajibu waache kuleta porojo hapa jamvini
 
  • Thanks
Reactions: jme
Nimekaa na nimetafakari hasa ni kitu gani huyu warioba anakitafuta na nimekuja kugundua kuwa anachokitaka hasa si chochote ila ni kuvunja muungano.Ukifuatilia kwa makini kazi yake rasmi ilishakwisha wakati wa tume ilipowasilisha ripoti kwa rais lakini ni kwa nini yeye amekuwa ndo kihelehele haswa kushinda wengine kutaka kujibishana na kila mtanzania dhidi ya upotofu wa mawazo yake na kutaka kila mtanzania afikiri kama anavyofikiri yeye!! hii inamaanisha kuwa akiwaambia watanzania kuwa bangi ni nzuri tu iruhusiwe basi anataka wazazi wote wamkubalie na atakaye pingana naye basi ujue ni ugomvi!! ndio mambo anayotaka kutuletea huyu mzee hapa kwetu na hizi pilika pilika zake za kutaka kuvunja muungano sa sijui ana ndoto za kugombea urais baadae kwa hii publicity stunt anayoifanya sasa??
Anakasirika sana pale anapoambiwa kuwa mawazo yake siyo yale ya watz kwani kwenye ripoti inaonyesha kuwa zaidi ya 60% ya watz wote waliopiga kura hawakuzungumzia suala la muungano hii inamaanisha kuwa walilidhika nao na ni % chache tu waliotaka serkali 3 na ya mkataba sasa hawa waliowengi ambao wameridhika na mfumo uliopo mbona unawalishia maneno ambayo hawakuyasema??
Kwa kweli huyu mzee mi ananichefua kabisa na hizi itikadi zake wakati mwingine nasikia tetesi kuwa eti anataka salim awe ndo rais wa muungano baada ya kukosa mwaka 85 kiti hicho kwa hiyo anataka kumpa kiti hicho kupitia mlango wa nyuma,maajabu ya musa haya!!
Pia anatabia ya kuwasemea waznzbr mi nachotaka kumwambia kuwa mi ni mbara lakini nimekaa znznbr miaka 6 na nimerudi mwaka jana tu nataka nimweleweshe kuwa waznzbr ambao hasa ni waunguja wao wanataka muundo huu uliopo bali uboreshwe tu hao anaowasema yeye wanataka serkali 3 ni wapemba wa kwao huko pemba ila wanaishi pale znzbr na ndio wanaopiga makelele na ndio ambao kwao ni masikini kushinda wote,na umasikini wao haukusababishwa na bara huku bali ni wakihistoria kwani wao waliyakataa mapinduzi na adhabu yao karume aliyowapa ndio hiyo ya kutokuwaendeleza sasa kikwete kaja kawapa rais mpemba,makamu wa rais,umeme labda wataridhika lakini wapi!! kumbe ni kweli yale maneno yasemwayo na waunguja kuwa hata umtendee wema mpemba kiasi gani hana shukrani.
Kwa hiyo warioba aache polojo zake waunguja ambao ni wengi na ambao asili yao ni bara wanataka muundo huu uendelee ila uboreshwe tu bado wanawataka ndugu zao wa bara hao wapemba kwanza wengi wao walishaukana uafrka na wanajiconsider wao ni waarabu ndo wanaotaka kujitenga wajiunge na nchi za kiarabu kwa hiyo warioba dont be pawn in a chess game which you dont even know father.
Warioba na wajumbe wenzake wa tume wameleta maoni na mapendekezo ya wananchi. Aliyewatuma ni rais. Acha kupiga porojo wenzako wamefanya utafiti kisayansi. Hao waunguja ulikutana nao wapi na unatakwimu zozote kuthibitisha hilo?
 
Tume ya Warioba ni tume ya tatu. Tume ya kwanza ilitoa mapendekezo ya wananchi kuwa ni serikali tatu, Chama tukakataa, tukaunda tume ya Pili, nayo pia ikaja na maoni yaleyale ya serikali tatu, chama tukasema HAPANA. tumeunda tume ya tatu, nayo pia inasema maoni ya wananchi ni serikali tatu. Chama hatuwezi kukubali kwa kuwa hawakusema tunachotaka. Katiba hii ni ya chama au ya wananchi?
 
Utanganyika utakupatia tonge? Tanganyika ni jina tu kwa taarifa yako Tanganyika ni jina la kimanyema na wamanyema asili yao Congo kwa hiyo Tanganyika ni jina la Kikongo ndiyo maana kule Kigoma waliongoza kwa kudai Serikali tatu
Confused!
 
Nimemleta ili wana JF walio Waislaam waelewe jinsi Waislaam wanavyotazamwa kwa mtazamo upi na Wakristo waliopo madarakani.

Ikiwa William Lukuvi ana hofu na Zanzibar kwa kuwa tu ni Waislaam, vipi wa hapa Tanganyika? hana hofu nao?

Sasa huyu mwehu ndo anakupa shida zote hizo!!
ukimsikiliza toka mwanzo unajua kabisa hilo DEBE TUPU aloimba Sabaha Muchacho!!
"Jina la Tanganika lililetwa na Wajerumani hivyo hatupaswi kulidai, je Zanzibar nani alilileta?
Unazungumzia suala la Rasimu ya katiba, GESI inaingiaje na gharama za umeme kupungua??
Shame on you CCM pupets!!!
 
Mtu mzima kama Warioba nakuja na hoja kama vile hakwenda shule eti:-
-Wewe ni mtanzania ila kama sio mzanzibar huwezi kupata aridhi znz pia huwezi kupiga kura znz
Ila kwao wakija tanganyika ni kinyume chake

-Takwimu ni za kweli ni kwanini kwa nyalali na kwa kisanga hawakusema twakimu ni za uwongo?

-anasema kipindi cha nyuma wanajeshi walikuwa choka mbaya lakin hawakufikir kupindua nchi kwa hiyo hoja ya kupindua nchi kwa sababu ya serikal tatu haitakuwa na fedha ya kuwalipa haina mashiko
-Wasizungumzie takwimu au gharama watafute majibu ya hoja na maswali
-Warioba amesema mwalimu akirudi ghafla akakuta maraisi wawili wanapigiwa mizinga 21 angeshangaa sana"

kwani uwongo, ktk huu muungano hakuna mzanzibari na mtanzania?.
 
Mtu kama wewe unaweza ukawa unafiri kwa kutumia 0655, mwambie aliyekutuma tunahitaji Tanganyika yetu hakuna Mzanzibar anayejiita Mtanzania, hafu bado unataka sisi Watanganyika yukae kimya

Ni wewe ndo unayeutaka utanganyika siyo sisi wote mtoto soma ndo mana ukaambiwa msome msisubiri kina tundu lissu wawasomee matokeo yake ndo haya sasa kila wanachokisema mnaona ni kweli tu kama wao miungu,unaongea maneno hayo sembuse hata miaka 38 hujafikisha halafu unang'aka ooh naitaka tanganyika we uliiona hiyo tanganyika?? je kama tanganyika ni jini je likija likakumeza we utajuaje? ndo mana mkaambiwa msome vijana sio polojo tu kisa dr.slaa kasema mkipingwa kidogo mnasema oo huyu katumwa oo huyu CCM!! katumwa gani basi nyinyi ndo madikteta wakubwa mana mtu akiwapinga kidogo tu kwenye mtazamo mnamwita mamluki mnataka kila m2 na kila mwanachama wa chadema afikirie kama kile anachofikiria dr.slaa na tundu lissu sasa kama ni hivyo mungu alikuumba na ubongo wa kazi gani wewe dogo??
fikiri kabla hujaongea zito kaja na hoja za uzalendo kawasifu ccm pale wanapopatia mnasema kibaraka!! mbona marekani leo hii kuna republican wengi tu walimwunga mkono obama kwenye obamacare na walimpigia kura kwenye congress?? sasa na wale ni wasaliti?? huo ndio maana ya uzalendo kwa nchi yako dogo sio unakurupuka tu ukadhani wote tuko sawa wenzako tunafikiri na kuumiza kichwa kabla hatujaandika!! umeshaambiwa wanaoshabikia kuvunjwa muungano wote ndo hao hao wanaotaka serkali 3 pia znzbr haina mapato mengi kuweza kutoa kama tsh.bilioni 5 kwa serkali ya muungano ila bara uwezo tunao sasa serkali ya znzb ikishindwa kupeleka fungu lake kwa serkali ya muungano miaka mi 4 tu muungano haujafa huo?? tumia akili zako dogo.
 
Kwa hili swali lako linajibika hii mbona ipo kwenye moja ya kero za muungano na linaweza kutafutiwa ufumbuzi,muwaonee huruma wenzenu wa pemba jamani waliopoteza ujana wao kwenye nchi ambayo si yao siku muungano ukivunjika sisi tutawafukuza na rais kahakikisha hilo huoni tutawatia umasikini jamani maana kauri ya rais si ombi ni amri,cha ajabu waunguja wanaoutaka muungano hajajenga bara bali wale wapemba wasioutaka ndo kama kwao sasa hivi hawa kweli wana akili sawasawa si wako sawa na mtu anayekata tawi au kuti alilokalia?? walioba zinduka!! WHY THAT MY FATHER?? WE GAVE EVERYTHING U NEED NOW UR TURNCOAT!!

Nina wasiwasi na uelewa wako. Hivi nani anasema anataka Muungano uvunjike? Hivi Warioba kwenye rasimu ya katiba hilo nalo aliliweka? Sasa kama Warioba hakuna mahali aliposema Muungano uvunjike wewe mbona unajaribu kumlisha maneno? Warioba alizungumzia muundo wa serikali 3 ambazo CCM hawazitaki na hawana sababu za msingi za kuzikataa hizo serikali 3 mbali ya kusema tukiwa na serikali 3 jeshi litapindua nchi. Haya mawazo yako peleka kwenye vijiwe vya kahawa huko labda watakuelewa lakini sio hapa JF.

Ningekuwa MODS, huu uzi ningeufuta kwani unatujazia Server bure.

Tiba
 
Mtu mzima kama Warioba nakuja na hoja kama vile hakwenda shule eti:-
-Wewe ni mtanzania ila kama sio mzanzibar huwezi kupata aridhi znz pia huwezi kupiga kura znz
Ila kwao wakija tanganyika ni kinyume chake

-Takwimu ni za kweli ni kwanini kwa nyalali na kwa kisanga hawakusema twakimu ni za uwongo?

-anasema kipindi cha nyuma wanajeshi walikuwa choka mbaya lakin hawakufikir kupindua nchi kwa hiyo hoja ya kupindua nchi kwa sababu ya serikal tatu haitakuwa na fedha ya kuwalipa haina mashiko
-Wasizungumzie takwimu au gharama watafute majibu ya hoja na maswali
-Warioba amesema mwalimu akirudi ghafla akakuta maraisi wawili wanapigiwa mizinga 21 angeshangaa sana"

kwani uwongo, ktk huu muungano hakuna mzanzibari na mtanzania?.kila mtz anaweza piga kura zanzibar?.
 
Kwa hili swali lako linajibika hii mbona ipo kwenye moja ya kero za muungano na linaweza kutafutiwa ufumbuzi,muwaonee huruma wenzenu wa pemba jamani waliopoteza ujana wao kwenye nchi ambayo si yao siku muungano ukivunjika sisi tutawafukuza na rais kahakikisha hilo huoni tutawatia umasikini jamani maana kauri ya rais si ombi ni amri,cha ajabu waunguja wanaoutaka muungano hajajenga bara bali wale wapemba wasioutaka ndo kama kwao sasa hivi hawa kweli wana akili sawasawa si wako sawa na mtu anayekata tawi au kuti alilokalia?? walioba zinduka!! WHY THAT MY FATHER?? WE GAVE EVERYTHING U NEED NOW UR TURNCOAT!!

sawa ni kero,lakini litatatuliwaje?mbona wako watanganyika wengi znz wamejikuta zaidi ya mika 7 wanaishi maisha ya kupanga sababu hakuna fursa za kuwa na kwako. na hii ni kero mama maana kama watanganyika wangeruhusiwa kuishi znz yaani kuwa na makazi na waznz kuruhusiwa bara kusingekuwa na kuvunja muungano au utz na uznz. lakini sasa kihalali znz ni ya waznz na hao watanganyika walioko huko ni wapangaji tu.
 
Big respect babu yangu warioba, ur a true hero for our country, naamini lazma muheshimiwa jk anajuta kukuchagua kwenye hiyo tume, ila kuna watu zero brain kama huyu ambae hajui hata asili yake!!!!
 
Hakutumwa kukusanya maoni ya wanaccm bali maoni ya wananchi na amekuwa threat kwenu kwa kuwa mko against wananchi...
Pamoja na exposure uchwara uliyonayo bwana Willium huqualify haka 0.00001% kum criticize, kumkejeli ama kutamka mambo yasiyo na hiyana kwa Mzee Warioba! Ni muda sasa wa kuwashauri wakubwa zako kwenye chama chenu kubadilisha maana ya unaoitwa mchakato wa maoni ya wananchi kwenye katiba mpya na badala yake uwashauri tittle iwe mchakato ya maoni ya wanaccm kwenye amendment ya katiba ya 1977 ambayo kimsingi pia ni katiba iliyoundwa kuisuite CCM!
 
hongereni ccm kwa kupewa mtazamo sawa wa serikali mbili kiasi kwamba hampingani,kuliko unavyosema chadema kuna wenye mitazamo tofauti,sasa tofautisha hapo nani ni machizi?,wenye mitazamo tofauti na wakapingana au wale wenye mtazamo sawa kundi zima?.
 
Warioba anataka serikali tatu kama mwananchi mwingine anayetaka.
Ko asishambuliwe kisa alikuwa mwenyekiti wa tume.
 
Waliopo madarakani au waliopo CCM?
Bado kitambo kidogo mtaelewa tu waasisi wa siasa za chuki za kidini na kikanda ni wahttps://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/649641-warioba-anataka-nini-hasa-20.html#post9399582kina nani.
Mlikuwa mnajifanya kupiga kelele ya mfumo kristo....ngoja ndo mtauelewa ndani ya serikali yenu ya CCM.

Nimeshakwambia tena, kamwambie JK wakati mkipata kikombe cha chai kwamba Lukuvi aondolewe. kama hata wewe bibi wa Kariakoo unashindwa kusemezana na JK na akakusikia itakuwa kelele za JF?

Waliopo madarakani, kumbuka kuwa mimi ni mwana CCM toka siku iliyoanzishwa mpaka hii leo na mawazo yangu ni tofauti na mawazo ya William Lukuvi aliyoyahubiri kanisani. Upo hapo ulipo?

Kuhusu kumwambia Kikwete, nimefata ushauri wako na nimemuleza, pitia hii: https://www.jamiiforums.com/katiba-...lliam-lukuvi-ameutia-dosari-utawala-wako.html
 
Back
Top Bottom